Nacte mliangalie hili kwa makini

Joined
Jan 4, 2014
Posts
31
Reaction score
11
NACTE walipoyaacha mamlaka ya upokeaji wa maombi ya kujiunga na vyuo mbalimbali vya kati hasa vile vya Private (colleges) nadhan walikua na nia njema, lakin hawakupanga ni namna gani watadhibiti upandishwaji wa ada ya maombi ya udahili (applibation forms). Wakati TCU inayadhibiti haya nimefika ktk chuo kimoja hapa Dar es Salaam nikiwa na sh. 30,000/- ya maombi ya koz ya pharmacy kama nilivoelekezwa ktk simu na wahudumu wa chuo hiko. Nakutana nao kwa kujiamin na kuiomba fomu hiyo, kabla sijapewa nikaambiwa inatakiwa sh.40,000/=(nikachoka). Nikaamua kuulizia ada kama nilivowauliza ktk simu, nikajibiwa ni Tsh.2,500,000/= badala ya Tsh.1,680,000/= nilioambiwa wiki 3 zilizopita na iliyoandikwa ktk GUIDE BOOK ya NACTE. Napo nikachoka kabisa.
Lakin si chuo hiki pekee chenye ada ya udahili isio eleweka, Pia vipo vingi sana na vinavyochukua mpaka Tsh.60,000 kwa fomu.
USHAURI: NACTE jaribuni kulisimamia hili kwa umakini. Uhuru mlowapa hawa watu wanautumia kujinufaisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…