Kwanza kabisa mniwie radhi kama post hii hapa sio mahala pake na Mods mnisaidie
Utakuta unaenda ofisi fulani ili uhudumiwe, alafu unakuta mhusika anaanza kujishebedua, mara anakuambia useme shida yako, mara aseme bosi yuko bize, mara njoo baadaye na mengine mengi. Sasa wakati huo kwanza hajakufahamu wewe ni nani na una title gani. Wengine hatupendi kujisema sema, kwa mfano mtu kujieleza kuwa yeye ni mkurugenzi kitengo fulani mahali fulani.
Sasa huyo mhusika anakuja kugundua baadaye sana kuwa wewe ni bosi fulani mahali fulani, anaanza kujinyenyekeza na kujifanya ana adabu kama nini anakuwa kama piriton. Anachomekea maswali ya kijinga jinga tuu..... "ooh, karibu sana, habari za huko, mnatuzidi nini huko, fulani hajambo... ngoja basi nimwambie bosi akuhudumie etc. bla bla bla bla bla kibao. Jamani hii inanikera na kunichefua.
Ni hayo tuu kwa leo