Nachoka baba yenu juu ya huyu workmate

Nachoka baba yenu juu ya huyu workmate

Umeshasema kuwa hana maajabu sasa
Sisi tuingie kwenye ubongo wake kuchunguza nini
 
Habari zenu wana JamiiForums,

Nimekuwa nikifanya kazi sehemu moja na msichana mmoja kwa miezi 3 sasa, hatufanyi majukumu sawa na Wala hakuna namna tunategemeana, lakini tangu siku ya kwanza tulipokutana, hajawahi kunisalimia yaan Ile "good morning" , "shikamoo" or whatever. Hata nikianza kumsalimia mimi sina hakika kama aliwahi kuitikia...maana Huwa simsikii...kiufupi hatujawahi kuongea hata kwa sekunde 2...ni ananikwepa vibaya mno.

Yaan yuko radhi ahame sehemu aliyokuwa amekaa akiniona nimesogea hapo na anapenda kama kunichunguza hivi ninapokuwa napiga stori na wengine huwa ni kama ananitazama kwa umakini sana akiwa mbali kidogo.

Kinachonishangaza zaidi wenzangu wengine anazungumza nao vizuri sana, anacheka, anasalimia, anashiriki mazungumzo. Demu mwenyewe Sasa hana maajabu...mfupi, nyama Hana yaan balaa tupu...anisamehe kwa majungu kidogo.

Ndugu zangu wataalam wa saikolojia naomba mnisaidie kuingia kwenye ubongo wa huyu dada mnifunulie kilichomo maana babq yenu ninachoka, ninachoka sana.
Natanguliza shukrani!..
Huwezi fungua mlango wa mwingine kama wako umekushinda kufungua...
 
Never date a workmate, baada ya hapo utaanza kutafuta uhamisho.
 
Sawa ni kufanya kazi mkuu...lakini ndio tusijali utu...tunawezaje kusonga mbele bila utu?😊
Utu pia ni pamoja na kutolazimisha watu wasiokupenda wakupende.

Kazini fanya kazi yako, hayo mambo ya ku socialize tafuta nje ya kazi.
 
Mkuu huyo demu simuelewi kabsa, sio kama hivyo...leo kapewa chakula aniletee kafika ame-drop off sahani ya msosi mezani kwangu nilipokuwa nmekaa bila "a" wala "e"...akapotea shwaaa
Mnakula msosi ofisini.. Wewe na boss wako mkatafute hela.
 
Utu pia ni pamoja na kutolazimisha watu wasiokupenda wakupende.

Kazini fanya kazi yako, hayo mambo ya ku socialize tafuta nje ya kazi.
Wewe umejuaje kama hanipendi/ananipenda au wapi nmesema ninamlazimisha anipende mkuu ndugu?
 
Wewe umejuaje kama hanipendi/ananipenda au wapi nmesema ninamlazimisha anipende mkuu ndugu?
Maandiko yako yote ni kulalamika kuwa hakupendi, hakujali.

Wewe mwenyewe huoni hilo?

Kama huoni hilo una tatizo kubwa zaidi.
 
Back
Top Bottom