Nabii TB Joshua awasili nchini Tanzania, Afanya Mazungumzo na Kikwete, Lowassa na Magufuli

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Kuelekea siku ya kuapishwa kwa Rais Mteule wa awamu ya tano, Dkt. John Magufuli, wageni mashuhuri wameanza kuwasili nchini, mmojawapo ni Nabii TB Joshua

Jana aliwasili na kufanya mazungumzo na Rais Kikwete, Rais mteule John Magufuli, pamoja na aliyekuwa mgombea Urais Ndg. Edward Lowassa

====

T.B Joshua Amebeba Ujumbe Muhimu Kwa Magufuli na Lowassa

Mhubiri maarufu kutoka Nigeria, T.B Joshua jana aliingia nchini akiwa na ujumbe muhimu na kupokelewa na rais mteule wa serikali ya awamu ya tano, Dkt. John Pombe Magufuli kisha kukutana na aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa.

Ujio wa T.B Joshua nchini unaaminika kuwa na lengo kuu la kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Dkt. Magufuli zitakazofanyika kesho ambapo watu wengine mashuhuri duniani pamoja na viongozi wa nchi mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria.

Muda mfupi baada ya kuwasili, mtumishi huyo wa Mungu aliyeambatana na mkewe, alifanya mazungumzo na Dkt. Magufuli na Mkewe Janeth na kisha kumtembelea Lowassa nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam.

Ni dhahiri kuwa, T.B Joshua alibeba ujumbe muhimu wa amani na maridhiano kwa ajili ya viongozi hao hususan katika kipindi hiki ambacho Lowassa ameendelea kupinga matokeo ya uchaguzi. Huenda ujumbe wa T.B Joshua utaweza kupenya moyo wa Lowassa na kukubali kuwa yaliyopita si ndwele.

T.B Joshua pia alipata nafasi ya kuonana na rais Jakaya Kikwete na kuzungumzumza.

Awali, T.B Joshua aliwahi kuwa mwenyeji wa Lowassa alipoenda Nigeria na kufanya ibada katika kanisa lake la The Synagogue Church of All Nations. Vivyo hivyo, Dkt. Magufuli na familia yake waliwahi kupata huduma ya maombezi kutoka kwa T.B Joshua.
 
hahahahaha ndio basi tena.. lowassa atahudhuria magufuli akiapishwa ... wacha huyu muhuni akampe neno dawa itamuingia atatia timu uwanja wa taifa ...

hapakazi tu!
 
Waswahili hujuana kwa vilemba mimi siasa sitaki siasa zina wenyewe hili picha tuwaachie wenyewe
 
Kuelekea siku ya kuapishwa kwa Rais Mteule wa awamu ya tano, Dkt. John Magufuli, wageni mashuhuri wameanza kuwasili nchini, mmojawapo ni Nabii TB Joshua
-Jana aliwasili na kufanya mazungumzo na Rais Kikwete, Rais mteule John Magufuli, pamoja na aliyekuwa mgombea Urais Ndg. Edward Lowassa

Huo "unabii" wake unatokana na vitabu vipi vya Biblia?
 
Duh siasa kweli inawenyewe...Nabii kamuweka sawa EL aachane na maandamano akubali yaishe heheheheheee.....kesho unaweza muona EL upande wa kushoto wa magu dah..!!!
 
bibilia ilishasema watakuja manabii wa uwongo msiwafuate sasa joshua sio nabii ni mganga wa kienyeji
 
Siku Sio Nyingi Watu watakaa kimya na kutoamini kitakachotokea.. Lowassa Ni Yule Yule Wa Ccm....
 
Lowasa ni vyema ukamsikiliza nabii wako kama unavyo msikiliza Ngwajima! tii sheria bila shuruti...
 
TB JOSHUA ni mpango Maalum inaelezwa ameongea na Lowassa Kwa muda Mrefu kuanzia said 12 jioni ...hadi baada ya saaa 3 usiku ...akiwa ameonana na Kikwete na Magufuli
Inaelezwa kuwa JK na Magufuli binafsi hawana ugomvi na Lowassa ...ujapata kuona wanadhalishana ....ukiacha wapambe hata kwenye kampeni kikwete ,Lowassa na Magufuli ni Mara chache Sana wamesemana ..Tena Kidogo

KATIKa mazungumzo binafsi na TB ..JK alimueleza juu ya uhusiano binafsi alionao na Lowassa ambao umevurugwa na Siasa ...jambo ambalo anapoelekea kustaafu angependa kumaliza tofauti zao Ili warudi marafiki Kama zamani wote wakiwa wastaafu

Ni Suala la muda Kama tb kafikisha ujumbe wa jk Kwa rafiki yake Lowassa ....huenda muda si Mrefu wakapatana na kumaliza Maisha Yao ya uzee KATIKA uhusiano Wao wa zamani ambako inaelezwa kuwa walishare kila Kitu hadi vichunchuda...

Rafiki mwingine wa Karibu wa Kikwete na Lowassa ni Abdulrahman Kinana ( ambao Wao humuita Abduuuu ) ....ambaye naye kwenye kampeni za urais zilizoisha alikuwa na wakati mgumu Sana kumuongelea Lowassa Kwa ubaya .....mtu ambaye wamefahamiana toka wakiwa na miaka 17 Kama vijana wa Chama MKOA wa Arusha ..Kinana akiwa kijana maarufu pale mjini Kati ...Kabla Yao Kwa pamoja kufahamiana na JK wakiwa na miaka 20 + hadi Sasa wamekuwa pamoja Kwa miaka 40
Kati Yao Kinana anaeleweka kuwa KATIKA Yale "Maisha" ya ujana alikuwa strict kuliko hawa ...ukiacha Suala la Kusaga mirungi kidogo ...mambo ya ugongaji alikuwa kivyake
 
Back
Top Bottom