Nabii T.B Joshua alilia hadharani

Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Jan 30, 2012
1,988
1,175
Ilikuwa wakati wa kihemko mnamo Septemba 8, 2019 katika ibada ya Jumapili ya moja kwa moja kutoka SCOAN, ambapo Nabii TB Joshua chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu alikuwa kwenye jukwaa na wana kwaya wa SCOAN.

Mtu wa Mungu anayesifiwa ambaye ameamua kutozungumza lakini kuelezea hisia zake na zile za Waafrika wenye nia moja na ulimwengu kwa jumla kupitia utenzi wa wimbo maalum akiitaka Afrika iungane kwa upendo na mshikamano. Dhima kuu ya huu wimbo ikiwa ni tuache mauaji, tukaribishane sisi kwa sisi. "Afrika tuungane!"

Taswira ya wimbo huu imewagusa wengi sana kwani haijawahi kutokea Nabii TB Joshua kuonekana kwenye Emmanuel TV akimwaga machozi. Tukio la wimbo huu wa halaiki limefanyika kwa sababu ya machafuko ya hivi karibuni nchini Afrika Kusini na Afrika kwa jumla. Katika huu wimbo wa halaiki, tunaweza kuona bango alilobeba Nabii TB Joshua Joshua huku machozi yakitikisa katika macho yake wakati akiendelea kuiimba:

Ili kutokupunguza uzito wa huu wimbo wa halaiki, naomba nikuwekee beti za huu wimbo kwa Kingereza. Beti za huu wimbo ni kama zifuatazo:-

Africa unite
Africa let us unite
We need each other
We need one another to grow
Africa unite

Africa unite
The South cannot do it alone
The West cannot go it alone
The East cannot do it alone
The North cannot go it alone
We need each other
We need one another to grow

See the killing
Over drug misuse
See the fight
As a setback
To Africa
Come together
Oh Africa
Don’t let fellow Africans
Feel unwelcome to our land
Africa unite

Tuungane afrika – Hebu maneno haya yapate kibali moyoni mwako na sala zako tunapojiunga na Nabii T.B. Joshua katika maombi kwa Afrika

Unaweza kuungalia huo wimbo wa halaiki kupitia

lazima alie kuna gorofa lake afrika kusini na kanisa, hapo analilia mali zake zilizopo huko sauzi

Mkuu Laki Si Pesa sio kila jambo unatakiwa uingize mzaha. Hivi Mkuu hilo ghorofa lipo mji gani huko SA? Mkuu hebu uangalie huo wimbo tena uone kama hutarudi hapa hapo baadaye na ushuhuda.
Ahsante
 
Utapeli wa hawa manabii wa uongo huko South Africa ni moja ya vitu vilivyochangia wenyeji wajawe na hasira.

We mtu kama Bushiri yule katoka Malawi apeche alolo kachuma South anapiga mipicha na migari na mijumba, halafu Wazulu wamelosti, unafikiri wanafurahi?

Lazima TB Joshua alie. Anaona watu wanaanza kustuka.
 
Bado miaka hii kuna watu wanamsikiliza TB Joshua?
yaani juzi tu Gwajima alikuwa anaendesha utapeli wa kufufua watu
hadi akatangaza kumfufua Amina Chifupa...na bado watu wanamuamini

T B Joshua si ndo aliemuhakikishia Lowassa urais?
na bado tu watu hawajifunzi kitu?
 
Asante Mimi ni muumini wa huduma ya scoan.hata sasa naangalia.
Ila nakupa pole wewe kwa mawe unayotupiwa kutoka kwa wale wasojua msaada wa Mungu.
Asante kwa Uzi mzuri.
Huenda twaweza tusithamini Walla kujua mpaka yatakapotukuta.
Tuumbee ufalme ili Mungu aupe moyo wa kusikia ili haya mabaya yasitukute nchi yetu.
 
Dini moja sababu kubwa waafrika wengi masikini.
Hii generation inabidi wafe bila kuambukiza upuuzi huu kwa the next generation labda wao wanaweza chomoka. Sadaka mnazowapa hawa manabii mngepeleka kwenye mambo mengine ya msingi
 
Hizi dini zinachangia sana umaskini kwa waumini wao.... maana hakuna nabii maskini.

Nilimwelewa Mzee wa Upako aliposema kufa maskini ni ufala.
 
Nyie wapagani acheni kuwadhihaki watumishi wa Mungu naona tu mkiitafuta radhi na taratibu mtaipata.
Stop blaspheming.
 
Utapeli wa hawa manabii wa uongo huko South Africa ni moja ya vitu vilivyochangia wenyeji wajawe na hasira.

We mtu kama Bushiri yule katoka Malawi apeche alolo kachuma South anapiga mipicha na migari na mijumba, halafu Wazulu wamelosti, unafikiri wanafurahi?

Lazima TB Joshua alie. Anaona watu wanaanza kustuka.

Mkuu Kiranga naambiwa wewe humwamini Mungu sasa unawezaje kuwapambanua au kutambua watumishi wa Mungu wa ukweli?

Ahsante
 
Utapeli wa hawa manabii wa uongo huko South Africa ni moja ya vitu vilivyochangia wenyeji wajawe na hasira.

We mtu kama Bushiri yule katoka Malawi apeche alolo kachuma South anapiga mipicha na migari na mijumba, halafu Wazulu wamelosti, unafikiri wanafurahi?

Lazima TB Joshua alie. Anaona watu wanaanza kustuka.
 
Kila siku mabaya yanatukuta,bado huyaoni tu kiongozi?

Back
Top Bottom