GE2025 Nabii Geordavie aichangia CCM Arusha milioni 50 ili kuwezesha kampeni za Samia

GE2025 Nabii Geordavie aichangia CCM Arusha milioni 50 ili kuwezesha kampeni za Samia

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
844
Reaction score
1,604
Nabii Mkuu wa Kanisa la Ngurumo ya Upako Dkt. Geordavie ametoa mchango wa shilingi Milioni 50 za Kitanzania kwa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha kwaajili ya kuwezesha Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania Samia anayetarajiwa kuwa na kampeni za Uchaguzi Mkuu Mkoani Arusha tarehe mbili mwezi Oktoba, 2025.

Geordavie amekabidhi fedha hizo kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Musa Matoroka kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa kwenye Ofisi za CCM Mkoani Arusha, akimtakia kheri pia Samia kwenye kampeni zake zinazoendelea kwenye Mikoa mbalimbali ya Tanzania pamoja na kukishukuru CCM kwa kumpa fursa ya kuchangia kampeni hizo!

1758800319521.jpeg


1758800351156.jpeg
 
Jamaa anaitegemea CCM, kumlinda kwa Biashara zake haramu.
CCM ni pango la wauza mihadarati
 
Sadaka za walalahoi ndiyo huyu tapeli kaamua kwenda kuzigawa kwa chama cha mapinduzi ili kiendelee kupata nguvu ya kuendelea kuyafanya maisha ya mtanzania kuendelea kuwa duni
 
Nabii Mkuu wa Makanisa ya Ngurumo ya Upako (N.Y.U), Dkt. Moses Kasambale Geordavie, ametoa wito kwa Watanzania kuhakikisha wanatumia haki yao ya kikatiba kwa kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa kuwachagua viongozi wa nafasi za Udiwani, Ubunge na Urais.

Dkt. Geordavie ametoa wito huo leo, Jumamosi Julai 5, 2025, jijini Dodoma, wakati wa hafla ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari katika masuala ya Uongozi na Huduma za Jamii pamoja na tuzo maalum kutoka Umoja wa Madaktari wa Falsafa na Maprofesa Tanzania (APDPT).

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Nabii Dkt. Geordavie amesisitiza kuwa kila Mtanzania ana haki ya kikatiba ya kuchagua au kuchaguliwa, hivyo ni muhimu kuitumia fursa hiyo kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

Aidha, ametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kazi kubwa anayoifanya kuongoza nchi, na kuwataka viongozi wa dini kuendelea kumuombea pamoja na Serikali anayoiongoza.

 
Back
Top Bottom