Nabii Frank Kilawa unatutishia maisha!

Nabii Frank Kilawa unatutishia maisha!

huyo atakuwa tapeli,namuonaga ktk TV anaombea mapepo lakini yanagoma kutoka,na kuna siku mapepo yatakuja kumdunda

Media hizo ziko tayari kurusha hewani watu wasio na huruma hata kidogo na watanzania kuliko kurusha vipindi vitakavyopelekea Tanzania kupata uhuru wa kweli na siyo wa magumashi iliopo.
 
...haaa...haaa...haa..! Yeye hana 'ramli chonganishi' ! :yo:....ingekuwa Vizuri mkamtumia kutambua wanao dhulumu Albino.

Wagalatia mna drama kama akina Lowasa ! kamagetac
[MENTION]Ally Kombo [/MENTION]Lowasa anakupa homa usipomtaja haujisikii na hadi ifike october utakuwa umebaki 2kg,back to the point,ukiitaji akuambie kuhusu wanaotumia viuongo vya albino atakuambia kama unavyo kwenda kupiga ramli kwa kupamba eti majini mazuri
 
Ukienda kwa Muislaam na kumuambia wewe ni Nabii, utapigwa tu.....maana hakuna jisi ni kupigwa tu ! :yo: christine ibrahim, Tabby, Ishmael, kalagabaho, Malyenge, Usoka.one, kamagetac

Kwa Waislaam hatuna shida ya kujua Manabii. Hawa hapa chini.

'Na tukamtunukia Ibrahim Is-haq na Yakuub. Kila mmoja tulimuongoa. Na Nuhu tulimuongoa kabla. Na katika kizazi chake tulimuongoa Daudi na Suleiman na Ayub na Yusuf na Musa na Harun. Na hivyo ndivyo tunavyo walipa wafanyao wema.

'Na Zakaria na Yahaya, na Yesu na Ilyas. Wote walikuwa miongoni mwa watu wema.

'Na Ismail na Al Yassa, na Yunus, na Lut'i. Na wote tulio wafadhilisha juu ya walimwengu wote.

'Na kutokana na baba zao, na vizazi vyao na ndugu zao. na tukawateuwa natukawaongoa kwenye njia iliyo nyooka (Uislaam)

'Hao ndio tulio wapa Vitabu na hukumu na Unabii.

Qur'an: 6:84-89.
Naona umemtaja Yesu hivi kumbe na nyie mnamuamini!!! katika Quruan yenu Ally Kombo
 
Last edited by a moderator:
Naona umemtaja Yesu hivi kumbe na nyie mnamuamini!!! katika Quruan yenu Ally Kombo

kamagetac

Yesu ni Nabii kwa Waislaam na Kitabu alichopewa ni Injil.

'Yesu akasema: Hakika mimi ni mja (binaadamu) wa Mwenyezi Mungu, Amenipa Kitabu (Injil) na amenifanya Nabii.

Na (Mwenyezi Mungu) amenifanya mbarikiwa popote nilipo. Na ameniusia sala na zaka maadamu ni hai.

Na (Mwenyezi Mungu ameniusia) kumfanyia wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, muovu.

Na amani iko juu yangu siku niliyozaliwa na siku nitakayo kufa na siku nitakayo fufuliwa kuwa hai.

Huyu ndiye Yesu mwana wa Maryam. Na hii ni kauli ya haki ambayo (Wakiristo) wanaifanyia shaka.

Qur'an: 19: 30-34.
 
Last edited by a moderator:
[MENTION]Ally Kombo [/MENTION]Lowasa anakupa homa usipomtaja haujisikii na hadi ifike october utakuwa umebaki 2kg,back to the point,ukiitaji akuambie kuhusu wanaotumia viuongo vya albino atakuambia kama unavyo kwenda kupiga ramli kwa kupamba eti majini mazuri

Huyo anafanya 'ramli chonganishi' na anafaa kufikishwa kw3nye vyombo vya usalama.
Kuhusu Tajiri Lowasa, kwa sasa anatetemeka......sasa sijui hiyo October atakuwa anayumba au !?
 
kamagetac

Yesu ni Nabii kwa Waislaam na Kitabu alichopewa ni Injil.

'Yesu akasema: Hakika mimi ni mja (binaadamu) wa Mwenyezi Mungu, Amenipa Kitabu (Injil) na amenifanya Nabii.

Na (Mwenyezi Mungu) amenifanya mbarikiwa popote nilipo. Na ameniusia sala na zaka maadamu ni hai.

Na (Mwenyezi Mungu ameniusia) kumfanyia wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, muovu.

Na amani iko juu yangu siku niliyozaliwa na siku nitakayo kufa na siku nitakayo fufuliwa kuwa hai.

Huyu ndiye Yesu mwana wa Maryam. Na hii ni kauli ya haki ambayo (Wakiristo) wanaifanyia shaka.

Qur'an: 19: 30-34.
Yesu alivyokuja duniani aliishi kama binadamu wa kawaida na ndio maana alizaliwa na mwanadamu wa kawaida(Mariam) na alikuwa na uungu wake,na hii yote Mungu alitaka wanadamu wamuamini zaidi.

Ila kwa mara ya kwanza nashuhudia Muislam kumtambua Yesu
 
Ukisoma maandishi yako utagundua kuwa kuna mungu wawili !....mungu Yesu na aliyemfanya mungu Yesu kuwa binaadamu.

'......hii ndio kauli ya haki ambayo (wakiristo) wanaitilia shaka.
Q: 19:34.
 
Ukisoma maandishi yako utagundua kuwa kuna mungu wawili !....mungu Yesu na aliyemfanya mungu Yesu kuwa binaadamu.

'......hii ndio kauli ya haki ambayo (wakiristo) wanaitilia shaka.
Q: 19:34.
Huwezi ukaelewa kwa kuwa umekaririshwa hicho unacho kitafsiri
 
Huyu jamaa simuelewi elewi! Anahubiri kibabe sana na vitisho vitisho vya kishirikina. Anasema anaponya magonjwa tote mpaka ukimwi.
Changa cheche:
1. Kwa wanaomjua, ile Huduma ya kuombea kwa kusukuma na vitisho kaagizwa na nani?
2. Wale walinzi wake anawalipa sh ngapi? Hivi wewe ni mtumishi wa Mungu, walinzi/mabodigadi wa nini? Yaani kila mahali mpaka kanisani mnaboa!

Manabii wengi Usiku hizi Huduma zenu hatuzielewi aisee.

Na wewe ulienda kutafuta mini kwa huyo tapeli?
 
Yesu alivyokuja duniani aliishi kama binadamu wa kawaida na ndio maana alizaliwa na mwanadamu wa kawaida(Mariam) na alikuwa na uungu wake,na hii yote Mungu alitaka wanadamu wamuamini zaidi.

Ila kwa mara ya kwanza nashuhudia Muislam kumtambua Yesu

Ukisoma maandishi yako utagundua kuwa kuna mungu wawili !....mungu Yesu na aliyemfanya mungu Yesu kuwa binaadamu.

'......hii ndio kauli ya haki ambayo (wakiristo) wanaitilia shaka.
Q: 19:34.

Huwezi ukaelewa kwa kuwa umekaririshwa hicho unacho kitafsiri
kamagetac

'Na wao (Wakiristo) ati husema kuwa Arrahmann Mwingi wa Rehema ana mwana !

Hakika m'meleta jambo la (kuchukiza) kuchusha mno !

Zinakaribia mbingu kutatuka kwa hilo, na ardhi kupasuka, na milima kuanguka vipande vipande

Kwa kudai kwao kuwa Arrahmann Mwingi wa Rehema ana mwana.

Hapana yeyote aliyemo mbinguni na ardhi ila atafika kwa Arrahmann Mwingi wa rehema kuwa ni mtumwa wake.

Hakika yeye amewadhibiti (viumbe wake wote) na amewahisabu sawa sawa.

Na kila mmoja katika wao atamfikia siku ya Kiama peke yake

Qur'an: 19:88-95

'Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwa na mwana, Subhanahu, Yeye ametakasika ! Anapo hukumu jambo basi huliambia tu: Kuwa ! (mara) Likawa.

Qur'an: 19:35
 
Last edited by a moderator:
kombo wewe ni mlevi wa dini

Nina akili timamu, ila tuna waonea huruma ndugu zetu katika Adamu, maana manabii wengine wanapika ramli chonganishi, wengine wanatoa vipigo. Sasa mpo kwenye dhiki kubwa. Hii yote ni kwakuwa hamtaki kusoma dini.

Kwa Waislaam Manabii wako wazi wazi bila kificho. wengi wao ni Waisrael.

'Na mtaje katika Kitabu (Qur'an) Ibrahim.Hakika yeye alikuwa mkweli, Nabii.

'.................tulimpa (Ibrahim) Is-haq na Yakuub, na kila mmoja tukamfanya Nabii.

'Na mtaje Musa katika Kitabu (Qur'an). Hakika yeye alikuwa ni mwenye kuchaguliwa, na alikuwa Mtume, Nabii.

'Nasi kwa rehema zetu tukampa nduguye, Harun, awe Nabii.

'Na mtaje Katika Kitabu (Qur'an) Ismail. Bila shaka yeye alikuwa ni mkweli wa ahadi, na alikuwa Mtume, Nabii.

'Na mtaje katika Kitabu (qur'an) Idris. Hakika yeye alikuwa mkweli, Nabii.

'Hao ndio alio waneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii katika uzao wa Adam, na katika wale tuliowapandisha pamoja na Nuhu, na katika uzao wa Ibrahim na Israil, na katika wale tulio waongoa na tukawateua (Waislaam). (Hao) Wanaposomewa Aya za Mwingi wa Rehema huanguka kusujudu na kulia.

Qur'an: 19:41-58
 
kamagetac

Yesu ni Nabii kwa Waislaam na Kitabu alichopewa ni Injil.

'Yesu akasema: Hakika mimi ni mja (binaadamu) wa Mwenyezi Mungu, Amenipa Kitabu (Injil) na amenifanya Nabii.

Na (Mwenyezi Mungu) amenifanya mbarikiwa popote nilipo. Na ameniusia sala na zaka maadamu ni hai.

Na (Mwenyezi Mungu ameniusia) kumfanyia wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, muovu.

Na amani iko juu yangu siku niliyozaliwa na siku nitakayo kufa na siku nitakayo fufuliwa kuwa hai.

Huyu ndiye Yesu mwana wa Maryam. Na hii ni kauli ya haki ambayo (Wakiristo) wanaifanyia shaka.

Qur'an: 19: 30-34.

Hicho kitabu cha injil alichopewa Yesu kinapatikana wapi? Je kwenye maduka ya vitabu vya kiislam au misikitini kinapatikana?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom