Nabii Frank Kilawa unatutishia maisha!

Nabii Frank Kilawa unatutishia maisha!

Jumong S

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
7,427
Reaction score
10,749
Huyu jamaa simuelewi elewi! Anahubiri kibabe sana na vitisho vitisho vya kishirikina. Anasema anaponya magonjwa tote mpaka ukimwi.
Changa cheche:
1. Kwa wanaomjua, ile Huduma ya kuombea kwa kusukuma na vitisho kaagizwa na nani?
2. Wale walinzi wake anawalipa sh ngapi? Hivi wewe ni mtumishi wa Mungu, walinzi/mabodigadi wa nini? Yaani kila mahali mpaka kanisani mnaboa!

Manabii wengi Usiku hizi Huduma zenu hatuzielewi aisee.
 
Bado sijaelewa ...huyu ni yule wa kimara. . Anayepiga watu makofi akitoa pepo? Hadi mdau akaja kulalamika JF
 
Siku za mwisho hizi, watajitokeza wengi watajiita kwa jina lake (Yesu)...tumieni akili kabla ya kuanza kusali kwny hayo makanisa yaliyojazana mjini kama viosk vya M-Pesa
 
Yule jamaa ni msanii anatembea anahubiri na mabodigadi nyuma kama rais mbona yesu hakuwa na mabodgadi kama Yesu yupo ndani yake anaogopa nini?
 
huyo atakuwa tapeli,namuonaga ktk TV anaombea mapepo lakini yanagoma kutoka,na kuna siku mapepo yatakuja kumdunda
 
mimi bora nisali nyumbani kuliko kwenda kwenye makanisa ya ajabu ajabu kama hayo
 
Loh!!!! huyu shetani sijui katumwa na nani, mahubiri yake hayatofautiani na lamri, nimchonganishi hadi basi, nimeona jana star tv anamwambia mama mmoja ambaye alimpeleka mwanae aombewe, kwa mwonekano mtoto anaonekana anautindio wa ubongo, yeye akasema mtoto alitolewa kafara na marehemu baba yake yaani nilichoka zaidi kajikanyaga hajamwombea kasema nitamweka kwenye maombi yangu lol..... kila aliyeenda kuombewa kwake amerogwa, kwa kweli serikali iliangalie hili swala la wahubiri wapiga ramli.
 
Wajnga ndiwo mliwao huyo ni nabii wa nani ameteremka duniani na ktabu gani kueni na akli banaa
 
Back
Top Bottom