Kwanza, msiingie ukichaa wa kutaka kuchagua timu ya kukutana nayo.
Pili, mnakumbuka msimu ule shafii dauda anawaita simba underdog walipoingia makundi, kwann walifuzu robo fainali huku wao wakiwa ni underdog wa kundi?
Tatu, unakumbuka mwaka ambao simba aliongoza kundi mbele ya al ahly, as vita na el mereikh, simba alimfunga vita nje ndani. As vita ile ilikuwa na moloko, mayele, juma shaban na wenzao ambao leo wote ni yanga
Hivyo; tatizo la yanga la kwanza kabisa ambalo wengi hamulioni ni kuhamisha as vita iliyojichokea mkaileta yanga af mkajipongeza kuwa mmesajili ili kucheza kimataifa
Hitimisho
Ukitaka kuwa mkubwa lazima uwafunge wakubwa, hapo ndipo nawe utaitwa giant na kuanzia hapo utakuwa unapangiwa timu za kawaida katika hatua za awali maana formula ni kibonde lazima apangiwe na giant na lazima aanzie kwake, yanga kimataifa bado anahesabika kuwa ni kibonde ndio maana anapangiwa na giant kama kanuni zinavyotaka, hakuna namna ya kuikwepa hiyo bali lazima uwazibue hao giant uongeze point ili ufikie ugiant utakaokupa sifa ya kupangiwa hao wamakonde unaowasema wewe