Suprise
JF-Expert Member
- Nov 2, 2012
- 2,696
- 1,063
wewe mleta mada ndio mdini....kama ulimpenda sana kwa nini wewe hukubadili?
ni kutojielewa na kufanya maigizo kubadili dini ili upate umpendaye, no way
wewe mleta mada ndio mdini....kama ulimpenda sana kwa nini wewe hukubadili?
wasabato na wayahudi ni mbingu na ardhi. kwanza wayahudi hawaamini kama yesu alikuja duniani. halafu pia sisi wakubwa zetu ni wakatoliki, kwa kua tulitoka katika ukatoliki... tukaitwa waasi na kuwindwa ulaya nzima, wengine kadhaa wakiuliwa kikatili na wengi wakikimbilia amerika ambayo ilikua na misingi ya uhuru wa kuabudu. tatizo hujasoma na kuvichambua hivi vitu, vipo wazi katika biblia na katika vitabu vya historia
foolish age... wow!
e
tatizo sio dini, tatizo ni true love
@Fidel80. Katika agano jipya Yesu anasema ktk Mathayo 5:17 Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii la sikuja kutangua bali kuitimiliza. Yesu hajaja kubadilisha chochote,Biblia ni Agano lake + jipya bila hivyo haijaitwa Biblia,wasabato wanasimamia maandiko ya Biblia sio watakavyo wanadamu.
Wasabato na Wakatoliki wapi na wapi? Labda unatafuta tu credits kwa kujiambatanisha. Nyinyi ni Wafarisayo na Yesu alipata shida sana na nyinyi. Kama mliamua kuishi kama Walawi, mbona basi nisione mkitoa sadaka za kuteketeza?
Wakatoliki tunakula Kambale na Kitimoto
@ mwana!
Hujui ulisemalo nakuombea kwa jina la Yesu ufunguke ujue maandiko kama wasabato! Haya maandiko yako agano la kale?
YESU ALIAMURU PEPO WAWAINGIE NGURUWE, KWELI NGURUWE HAWAFAI!
Mathayo 8:28-32, marko 5:1-20, luke 8:26-39 Walipofika pwani ya nchi ya wagerasi inayoelekea Galilaya alikutana mtu mtu mmoja mwenye pepo hakuvaa nguo siku nyingi na hakukaa nyumbani ila makaburini,alipomwona Yesu alipiga kelele akasema kwa sauti kuu nina nini nawe Yesu,mwana wa Mungu aliye juu? Nakusihi usinitese,Yesu akamwuliza jina lako nani? Akasema jina langu Jeshi,wale pepo wakamsihi asiwaamuru watoke kwenda shimoni,wakamsihi awape ruhusa kuwaingia wale nguruwe,basi Yesu akawaamuru pepo wakatoka kwa mtu Yule wakawaingia wale nguruwe,nalo kundi la nguruwe liliteremka gengeni kwa kasi ,wakaingia ziwani wakafa maji.
I hate people wa hivyo wote mnaabudu Yesu mnatofautiana madhehebu tu nao ni tatizo.
Am sorry to say this dini/imani haina nafasi kwangu zililetwa na wazungu na waarabu kugawa watu.
Leo hii mimi amu muislam sababu nimezaliwa dar pwani ila ningezaliwa Mbeya au Bukoba ningekuwa mkristo.
Siku zote mahusiano ni uamuzi wa mtu those excuses are just rubbish
Lakini nyie mmejikita kwenye agano la Kale
Ha ha ahaa haa mkuu umenifurahisha sana nyama wanakula ila sio zote hasa hasa yule mnaomwita noah .ni najisi!!Kusema ukweli Sabato ni Wakristo, lakini kidogo mna mambo magumu , na ndiyo maana mnahisi kubaguliwa.
Mambo kama yafuatayo ni ishu sana:
-Kutokula nyama
z
-Kutokunywa soda
-Kutokula baadhi ya samaki.
-kutokunywa chai na kahawa.
-kutopika wala kugusa chochote jumamoc.
-chakula cha jmosi kupikwa ijumaa.
-jua likizama ijumaa sabato ishaanza.
-mambo ya lesoni, pathfinderz, makambi etc
-hakuna sikukuu zozote za kikristo.
-hakuna vipindi maalum vya kanisa kama vile Majilio, Kwaresma, Ijumaa kuu na Jumatano ya majivu.
-masharti kama kutokutengeneza nywele kwa mwanamke, wakati mnajua MWANAMKE NYWELE.
-Kutumia na kuamini zaidi agano la kale kuliko jipya.
Kweli mdada anahitaji maamuzi magumu kabisa kuamua kuachana na mambo aliyozowea na kuwa msabato.
Dadaangu wa tumbo moja akiamua kuwa msabato nitamkubalia, lakn nitalia sana na machozi yataenda tumboni.
salaam wanajamvi,
Leo nimeamua kuandika kuelezea umma namna udini na ukabila ulivyojengeka nchini, hususani katika mapenzi. Mimi ni mhandisi mhitimu wa chuo kikuu nina miaka 28. Mara ya kwanza kujihusisha na mahusiano ilikua mwaka 2006, wakati huo nikiwa form 6. Nakumbuka ilikua Dodoma, nilipokutana na mpenzi wangu huyo wa kwanza katika maisha yangu. Tulipendana sana, na tuliwekeana malengo na mipango mingi ambayo kwa asilimia kubwa tuliweza kkuitimiza.
Matatizo yalianza kuzuka mwaka 2007 huyu binti alipoenda chuo kusoma na mimi nikachagua kufanya kazi kwanza, kampuni flani hivi ya madini. Vikaanza visa kila kukicha , japo nilijaribu kumtimizia kila alichohitaji.....hatimaye aliamua nimwaga rasmi mwaka 2009
Nakumbuka nilimwaga machozi na kuchanganyikiwa. wakati huo nilikua nimejiunga na chuo , niko mwaka wa kwanza.... tulikua katika mitihani...nilifeli karibu nusu ya mitihani yote. ilinichukua miaka miwili kusahau kidogo kilichotokea.
Binafsi, sikuweza kuanzisha mahusiano na binti yoyote kwa kua katika nafsi yangu nilikua nampenda x wangu tu. wapo waliojaribu kunitega, relationships zingine zilivunjika ndani ya usiku mmoja.
Wakati nakaribia kumaliza mwaka wangu wa mwisho chuoni, mpenzi wangu wa zamani alirudisha mawasiliano na akanieleza sababu zilizosababisha aniache. akaniamabia ni kwa kua mimi ni mtu wa musoma , kwao sikubaliki. ati kuna dada yake aliwahi kupata mchumba mtu wa msoma akamsumbua sana, tangu siku hiyo ikawa nongwa kwao. sababu ingine akaniambia pia kwa kua mimi ni msabato.... ati kwao wasabato wanawachukulia kama walokole na wenye imani kali. akaniambia yuko tayari kurudiana na mimi iwapo tu nitaamua kubadili dini na kua mkatoliki kama yeye... ishu ya kabila atanitetea kwa mama yake na dada zake wawili (tena wote wahandisi, wasomi) ambao kila kukicha wamekua wakimpa semina za kutafuta mwanaume ambae ni mkatoliki na asiwe mtu wa musoma
Iliniuma sana, zaidi hata ya aliponipa kibuti mara ya kwanza. kwa kweli japo nampenda sana .. ishu ya kubadili dini nilimkatalia na ndio ikawa nimemkosa milele.
Baada ya miezi kadhaa, nilikutana tena na binti wa kichaga... mwanachuo, mhandisi wa fani sawa na yangu. katika urafiki wetu uliodumu kama miezi 6 , nikajikuta nimezama katika penzi lake na hapo ikabidi nimwambie ukweli mwanzoni mwa mwezi huu nia yangu kwake. yes , nilijua kuna kupata na kukosa.. na ni kweli, alikataa...akadai anafurahia sana urafiki wetu wa kawaida ..na nilipojaribu kumdadisi kama kuna kinachomzuia...story ikawa ile ile...kabila langu na dini yangu kwao havikubaliki....
uchungu niliopata siku hiyo siwezi simulia...nakumbuka nilienda slip way nikasimama na kushangaa bahari huku machozi yananitoka kwa zaidi ya masaa 6...
dini yangu, kabila langu imekua jinamizi kwangu.....nakereka zaidi na kauli kua nisubiri wangu anakuja.
nawashauri wote ambao mnabagua kwa udini na ukabila muache hizo mambo.. mnaumiza sana wengine. mpenzi wa kweli na mwenza wa maisha anapimwa kwa tabia na sio vigezo hivyo.
sina uhakika kama nitakuja kupenda tena, ni ubaguzi ... ubaguzi tu:shut-mouth: