Naacha kazi serikalini

Ngedere, kabla ya kuacha tawi, HUWA ANAJUWA ANAKWENDA KUDANDIA TAWI LIPI. Maamuzi hayo ya kudandia tawi lipi huwa anayafanya kabla hajaachia tawi alilolishika wakati anafikiri....

Kwa mfano huu, andaa kwanza mazingira kabla hujaiacha hiyo kazi uliyonayo.... KUNA MSEMO UNAOSEMA, ACHA KAZI UONE KAZI KUPATA KAZI.... AU... KAZI MBAYA UKIWA NAYO

Asikushinde ngedere kwa kufikiri...
 
Pole sana mkuu, ningekushauri kabla ya kuacha uwe umeshaimarisha kipato chako na una njia nyingine mbadala ama sivyo utaitesa familia yako na wewe mwenyew
Hapo alipo anateseka na familia alafu unamwambia akiachakazi atateseka. Mimi namshauli kwamba kama ameweza kuvumilia maisha ya ualimu basi anaweza kufanya kazi yoyote akapata pesa. Acha hiyo kazi kwa vike uipendi na haina maslahi na anzisha biashara ya chapati, uji, chain sehemu zenye msongamano mwingi wa watu na hiyo kazi ifanye 24 hours uwe unalala hapo kwasababu wateja ndo hao hao watu wanaoingia na kutoka. Tafuta sehemu kama mbezi mwisho, tegeta nyuki, au mikoani nenda stendi za mabasi. Wasafiri wengi hawana hela ya lodge na chakula akipata chapati/uji ndo imetoka. Hii biashara inapesa ila wanaoifanya kwavile wamepiguka hawana malengo ela inaishia hivyo hivyo lakini nafahamu watu wenye uhakika was kuingiza hata 80,000 kwa siku kama umejipanga na huna aibu utaajili wadada jinsi kijiwe kinavyochanganya
 
Ushauri wa kweli kabisa usio hata chembe moja ya unafiki.
 
Binadamu gani aliyekifundisha kipele kumuota mtu asiye na kucha.
Nikutakie mwisho mwema mkuu acha hiyo kazi ukiwa sambamba na akili zako.
Hebu tikisa kichwa kwanza alafu sema chalk unanipa hela..

Ushauri wangu
Wakati unaendelea kufundisha fanya survey mtaani ujue ukitoka hapo unakwenda wapi na kufanya nini na kwa malengo gani
Sio unatoka mbio mbio kama sisi ambao sio wasomi utakwama mkuu walimu hampo hivyo
 
Good Mimi mwenyewe niliajiriwa na nilikula msoto na kuchoka kupangiwa chakufanya,muda,kipato nk.
Nilinunua counter book jipya,somo kuacha kazi,niandika plani ya kuacha kazi ile ndani ya mwaka,niliandika way forward,nilisoma vitabu vingi mf. retire young retire rich/get rich nk vilinibust saaaana.
Ndani ya huo mwaka nilianza biashara miezi saba kabla mwaka kuisha,biashara iliponoga nilianza kutega kwenda job nakomaa na biz...baada ya miezi 9 nikasimamishiwa mshahara,sikwenda job nkawambia sina nauli,baadae tukaachana saivi siohaba naenjoy biashara inakuwa mpaka ninawakopesha wale niliowaacha kule...Niko huru mmno nasafiri najifunza mengi mitaani badala ya kujifungia ofisini huku ukipelekeshwa!!
Chamuhimu wewe jipange kwanza,jiulize unachopenda kukifanya utapoacha hicho usichopenda...kisha kaking'ang'anie mpaka kiwe bila woga vingine vitaibukia huko mbele. All the best
 
Kuacha kazi si vibaya wengi walishafanya hivyo, ila swali la kujiuliza unaachaje kazi, yani umejipangaje??
Kama una biashara je imesimama?
Au hmunaacha kazi alafu unabaki nyumbani umelala??
 
Ki kwenye ugumu ndio kuna chance

We huoni wenzio wenye jicho la tatu wanaona gapes kibao

Badilisha mindset hio
 
Pole sana...

Tafuta kazi ndiyo uache kazi, kupata kazi wakati unakazi ni rahisi sana kupata kazi... ila kuacha kazi alafu utafute kazi wakati huna kazi ni kazi sana kupata hiyo kazi...



Cc: mahondaw
 
Kama kuupata mhimili kwasasa ni shida nakushauri usiache kazi. Ukiwa na kazi opportunities zinakuwa nyingi ila usipokuwa na kazi mambo yanagoma.
Cha kukushauri jaribu kutafuta namna ya kuongeza kipato ukiendelea na hiyo ajira yako ya sasa.
Naungana na wenzangu wanakushauri vizuri sana pia kwa kuzingatia hali halisi.Yaani wamesimama kana kwamba ni wao wanataka kufanya kama wewe.Nawapongeza kwa kukujali.

Langu ni hili Mwalimu.Mimi nilikuwa huko ila sasa sipo tena ila sio pa kuacha.Muda wangu ulifika nikaondoka.

Nakuomba sana weka Familia yako akilini kwako kabla hujatoa maamuzi.Ni vizuri ukatafuta kitu cha kukuingizia kipato ukiwa bado uko kazini.Kwa sababu ukifeli utachanganyikiwa na utaharibikiwa kabisa.Lazimisha sasa hivi kuipenda kazi hii unayoifanya,ili usipate stress ukaharibu kazi yako.

Bado una nafasi kubwa ya kufanya kazi nyingine ukiwa kazini kwani mara nyingi sana Mwalimu anafit sehemu nyingi sana.

Kama unataka kufanya biashara au kilimo inabidi kweli ujipange.Hali huku si nzuri kutoka na mzunguko mdogo wa fedha.
 
kama muuza mihogo,maandazi,kahawa,kashata,matunda,mitumba,chapati,mchicha,mahindi ya kuchoma,mshona viatu,muuza karanga n.k wanaishi,kwa nini wewe ushindwe mwenye kaujuzi kidogo;acha kazi, njoo uraiani tupambane,aibu weka chini ingia vitani.Hata vitani mwanajeshi anaenda,haijalishi atakufa ama atapona.
 
Badala ya kufikiria kuacha kazi fikiri nin unaweza kufanya ukaongeza chanzo kingine cha kipato. Andika kitabu cha somo unalofundisha, anzisha tuition center, kopa bodaboda asubuhi unatumia usafiri wa kazini jioni unafanya kazi ya bodaboda, kama upo mkoani angalia zao ambayo unaipata kirahisi huko na inasoko mjini kusanya safirisha ukirudi rudi na bidhaa adimu huko uishipo.
 
Shule ya msingi niliyosoma walimu walikuwa 33, wanne pekee walikuwa wanaume, hakukuwa na malalamiko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…