Naacha buku 15 daily nakuta ugali na dagaa

Naacha buku 15 daily nakuta ugali na dagaa

Habari zenu wana jf,
Nimevumilia vya kutosha hii tabia sasa naona itakua imefika kikomo,Naishi na mpenzi wangu hatujafunga ndoa tatizo nashindwa kumuelewa kila siku niendapo kazini na kurudi jioni lazima nimuachie elfu kumi na tano 15,000/-kusudi nikirudi jioni nikute mezani kumependeza nadhani mmenielewa cha ajabu jamani nakuta ugali na dagaa akibadili sana tembere kaomba kwa jirani.Huu ni ungwana jamani?kumuambia nashindwa naona kama takua naingilia mambo ya jikoni ambayo hayanihusu na nisipokula huo ugali ananuna sielewi nifanyeje wana jf


wewe ukirudi uliza chakula gani kimepikwa. kama ni matapu tapu unaenda kula nje. ukifanya hivyo mara nne ata badilika.
 
Acha u.b.w.e.g.e nenda sokoni nunua leta home...
Point taken,Hapo ukute ana vikoba,finca rejesho,mchezo 10000 kila baada ya siku kumi na bado hajamodoa madera kwa fundi issa,hao ndo wanawake wa daslam bwana!
 
Owa kwanza,kwan kule kwenye kununua ngono mbona mnatoaga zaidi ya hiyo?Sa wewe 15 unataka na chakula humo humo?
15 kubwa sana mkuu,nimevumilia vya kutosha now as the time for action
 
Hayo ni madhara ya MWANAUME PESA,na sio MWANAUME UZURI...Kwa kuwa kafata pesa hakuonei hata huruma.
 
1.Chungulia uvunguni mwa kitanda utakuta kibubu.
2.Ukihoji majirani lazima atakuwa anacheza mchezo wa buku 5 kwa siku (Upatu).
3.Kuna mahali anawekeza huyo.

Nini chakufanya.
1.Ingia sokoni nunua kila kitu kwa matumizi ya wiki au mwezi mzima.
Yaani Mchele, Unga, Maharage, Samaki wakavu kwa wabichi, Viungo vyote jaza kwenye friji, Nyama na Samaki wabichi unaweza ukawa unaleta jioni ukiwa unatoka kazini. Matunda Kwa Dar sio shida unaweza kuleta mwenyewe.
Ratiba ya chakula kwamba leo tule nini inabidi mupange asubuhi kabla hujaondoka na ikitokea umesahau mwambie kabla hajapika akujulishe au akuulize leo unakula nini. Bajeti ya chakula musichanganye na bajeti ya mavazi na mengineyo. Kama kila kitu kitakuwa ndani maisha yanakuwa rahisi sana. Kila kitu kikiwa ndani unaweza kuacha 5000 na ukakuta haijatumika. vitu kama juices jijengeeni tabia yakujitengezea wenyewe za matunda kuliko kununua hizi za supermarket. Jaribu kufanya hayo kisha ulete feedback.
 
Habari zenu wana jf,
Nimevumilia vya kutosha hii tabia sasa naona itakua imefika kikomo,Naishi na mpenzi wangu hatujafunga ndoa tatizo nashindwa kumuelewa kila siku niendapo kazini na kurudi jioni lazima nimuachie elfu kumi na tano 15,000/-kusudi nikirudi jioni nikute mezani kumependeza nadhani mmenielewa cha ajabu jamani nakuta ugali na dagaa akibadili sana tembere kaomba kwa jirani.Huu ni ungwana jamani?kumuambia nashindwa naona kama takua naingilia mambo ya jikoni ambayo hayanihusu na nisipokula huo ugali ananuna sielewi nifanyeje wana jf

Ngoja uwe ATM kwanini yeye naye asijishughulishe aone pesa ilivyongumu kutafuta?
 
1.Chungulia uvunguni mwa kitanda utakuta kibubu.
2.Ukihoji majirani lazima atakuwa anacheza mchezo wa buku 5 kwa siku (Upatu).
3.Kuna mahali anawekeza huyo.

Nini chakufanya.
1.Ingia sokoni nunua kila kitu kwa matumizi ya wiki au mwezi mzima.
Yaani Mchele, Unga, Maharage, Samaki wakavu kwa wabichi, Viungo vyote jaza kwenye friji, Nyama na Samaki wabichi unaweza ukawa unaleta jioni ukiwa unatoka kazini. Matunda Kwa Dar sio shida unaweza kuleta mwenyewe.
Ratiba ya chakula kwamba leo tule nini inabidi mupange asubuhi kabla hujaondoka na ikitokea umesahau mwambie kabla hajapika akujulishe au akuulize leo unakula nini. Bajeti ya chakula musichanganye na bajeti ya mavazi na mengineyo. Kama kila kitu kitakuwa ndani maisha yanakuwa rahisi sana. Kila kitu kikiwa ndani unaweza kuacha 5000 na ukakuta haijatumika. vitu kama juices jijengeeni tabia yakujitengezea wenyewe za matunda kuliko kununua hizi za supermarket. Jaribu kufanya hayo kisha ulete feedback.
nimekuelewa vizuri
 
ongeza hela mkuu. 15,000 ni hela ya ugali dagaa kweli.
hapa natafuta sababu ili nimpe notice ujinga ctaki kabisa mfano angekuwa na mtoto cndo atamkondesha kabisa
 
Acha uongo nahisi huachi 15000 bali 1500. Vinginevyo mwanaume unailiza. Kwani ni haki yako kula mlo uutakao kwa uwezo wako. Khaaaaaaa??????
 
mambo mengine haya hitaji ushauri MKUU. achana na hao wanaokwambia uoe kwanza hiyo ni point nyingine kbs .

MKUU hiyo 15 nikubwa sana mm nakulaum sana kwakushindwa kumhoji na inaonekana ww huyo mwanamke ww ndio umependa kwa sana/ kakushika tawala ndio maana hupumui kwake.
huo sio uwanaume hata kidogo.
kama hufanyi kazi mpaka week end siku moja ongozana nae mpaka sokoni chukua ile ile 15 nunua vitu vyakupika utakavyo mf samaki mbogamajani viungo mchele kilo 1 na matunda uone mtatumia kiasi gani??

nunua unga kiroba mchele debe mafuta ya kupikia Lita 5 maharage hata kilo 10 samaki wakutosha wiki nzima vitunguu kisado karoti zakutosha wiki bamia nyanya n.k then kila unapotoka asubuhi mwachie 5 elf.

ujue unaweza ukawa unamraum mkeo kumbe ww mwenyewe ndio mwenye matatizo au ndio ulijitengenezea hilo bom ww kila Siku unaacha 15 kwaajili ya msosi then ukirudi unakutana na matapu tapu ya ajaabu ajabu hata huulizi ww unakandamiza 2 kesho tena unatoa 15 lazima mwanamke akuone na kukufanya msukule.
mwisho wa siku unakuja kulalamika na kulialia hapa JF tena kwakusema eti naogopa kumuuliza hivi kweli ww nimwanaume timamu kweli??
ukiambiwa nunua vitu ooo atakuona mbahili.
sasa unataka ushauri gani??
nenda basi kamsemee kwa mama yako au kwa mama yake ili amseme..

hivi ukichapiwa utalalamika?? wanawake wanapenda wanaume wenye msimamo na wenye maamuzi imara yaliyo nyooka sio legelege kama mlenda.
kashakuona hueleweki mwanaume suruali huna msimamo hujitambui ndio maana kila siku anakulisha ugali dagaaa na tembele.
 
Nakushangaeni.....

Mnashindwa nini kwenda sokoni weekend mnunue vitu vya kutosha? Nyabya hohi karoti mvhele mahatlrage matunda? Then muende feri mnunue samaki wa kutosha?

Nyama mnaweza nunua fresh kila leo.

Kisha acha 10 per day

Na huyo gf mwanzishie hata biadhara ya kuuza barafu

Na mahitaji yake mengine uyajave
na mimi nakushangaa unapodhani sisi sote tuna mafriji ya kuvitunza hivyo vitu!umeme wenyewe tunanunua wa rejareja,tunawasha wakati wa kuingia kulala na kuzima mara moja!!hiyo 15 wengine haipo in bulk kwa wiki nzima inaingia kila siku ujue...
 
Back
Top Bottom