Na wewe ulikuwa unaudhika kama mimi?

muuza ubuyu

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
3,511
3,477
Wakuu salama?

Kuna kitu kidogo sana huwa kinaniudhi (hasa zamani). Kwa utamaduni wa kitanzania unapokutana na mtu bila kujali kama unafahamiana naye, salamu huwa ni kitu cha msingi na kiungwana.
Kwa kawaida salamu yetu ya kiswahili inaambatana na maswali ya kujuliana hali. Sasa, mimi huwa natarajia nikimsalimia "shikamoo" mtu anayeenizidi umri naye ataitikia "marahaba" na pia kuulizia hali yangu kwa maneno kama "haujambo, habari za huko utokako"? Na maneno mengine yatafuata kutegemea na kufahamiana/kuzoeana kwetu.

Kimbembe kinakuja mtu mzima unamsalimia kwa heshima "shikamoo", yeye anajibu kwa mkato "marahaba" halafu anauchuna. Enzi nikiwa kijana nilikuwa nakasirika sana kwani naona jamaa anapenda sana shikamoo yangu badala ya salamu/kujuliana hali.

Ujana bwana!
 
mi sipendi kusalimia hadi leo

yani ile "shkamoooo" au "za saizi" yani sipendi

Natamani tu tukikutana tupite tuuu
 
Back
Top Bottom