Na vijijini je? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Na vijijini je?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by St. Paka Mweusi, Sep 3, 2010.

 1. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,901
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu zoezi la kampeni na mbwembwe zote za wanasiasa.Mwaka huu inaonesha wapinzani kweli wamepiga hatua tofauti na huko nyuma.Swali langu kwa wana JF na wote wanaomsupport DR SLAA ni Je kampeni hizo ni kona zote za nchi au zinaishia makao makuu ya wilaya na mikoa tu. Maana kuna sehemu nyingi tu nchini kwetu wala hawajui kama kuna upinzani nchini na wanajua kuwa chama pekee ni CCM tu.Nasema hivyo kwa sababu binafsi nimekuwa mtumishi wa serikali kwa takriban miaka mitatu na nimeshiriki kusimamia uchaguzi wa 2005 na nilichokiona ni naona uchungu hata kukieleza.Na kama hawa watu hawafikiwi na kuelimishwa basi ushindi kwa wapinzani utachukua karibu miaka 500 kupatikana .NAOMBA KUWAKILISHA.
   
 2. m

  matambo JF-Expert Member

  #2
  Sep 4, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 728
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  hilo ndilo tatizo tunalojaribu kuwaelimisha wenzetu walioko uingereza ,marekani na dar es salaam kuwas ituation mnayoiona sio ukweli hata kidogo

  siku moja nilisoma post ya jamaa mmoja akadai aliposhuka tu airport akafanya ka survey kadogo kwa kuuliza watu watamchagua nani kati ya jk na slaa, kisha akapata majibu kuwa wengi watampigia slaa then jamaa akaconcludde kuwa mwaka huu CCM kazi wanayo, bonafsi nilisoma post ile nikafarijika kuona watu wako optimstic ila ukweli eapoti sio vijijini jamani, hivi nyinyi tanganyika masagati umbali wa km 200 kutoka wilaya ya ifakara wanamjua slaa?mahali kusiko na aina yoyote ya miundombinu?mahali ambako dawa na vifaa hupelekwa baada ya miezi sita kwa ajili ya uduni wa miundombinu?

  huku ndiko kwa kuanzia, pili ukienda na helikopta maeneo haya watu wanadai wewe hujui matatizo yetu ndo mana umekuja na helikopta, ungekuja kwa landcruiser au landrover wangeelewa kuwa umeona matatizo yao, so wanadai helikopta inakufanya usitambue matatizo yao

  just piece of advice to chadema gaweni teams nyingi zifanye mikutano vijijini ikibidi nyumba kwa nyumba ,kwa maana vijijini ni rahisi nyumba kwa nyumba kaMA MNA TIMU ILIYOJIPANGA VIZURI
   
 3. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #3
  Sep 4, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,901
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Haya ndio na mimi najaribu kuwakumbusha ndugu yangu MATAMBO maana wasione mkutano una watu 10000 wanasikiliza ukasema mgombea wetu amefunika wakati kuna zaidi ya watu laki tano katika eneo hili hawajamsikia mgombea na wala hawamjui.USHINDI SI MIJINI BALI NI VIJIJINI WALIKO WATANZANIA HALISI WALIOKATA TAMAA NA MAISHA.Huko ndiko karibu 75% ya raia walipo na ni hao ambao wanamfanya JK atambe kuwa atapata ushindi wa Tsunami msipoliona hili subirini kilio na kushikana uchawi .NAOMBA KUWAKILISHA
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Sep 4, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Si kweli kabisa. Mimi binafsi nimepita vijijini huku niliko na nilishangaa sana. Watu wengi wanamfahamu vizuri sana Dr Slaa. Wengi wako tayari kumpa kura zao kabisa. Ingawa nilipita jimbo moja huko vijijini wakaniambia kweupe kuwa wao walimuhitaji zaidi mgombea wa sisi m katika ubunge lakini wakasema ni makosa kumpa urais Kikwete. Tena ilinishangaza sana.

  Tuendelee kuwapa elimu kwa mbele huku tukijua kuwa na wao wanajua. Tusidhani mambo yanaishia mjini tu. Nani alijua kuwa Tarime hadi vijijini wanaifahamu Chadema? Inawezekana.
   
 5. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #5
  Sep 4, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,901
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Ndugu yangu Mchukia Fisadi ni vizuri umeangalia huko Tarime lakini naomba ujijibu Tarime ni % ngapi ya wapiga kura na naomba ujaribu kupitia sehemu kama Shinyanga Tabora Mwanza Rukwa ikibidi na Singida isiwe mjini ila toka kama km50 tu toka wilayani au mkoani kisha unijibu.Maana mkoa ulionitajia wana mwamko mzuri tu sawa na kilimanjaro na Arusha lakini asilimia kubwa ni kama nilivyoeleza NAOMBA KUWAKILISHA
   
 6. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #6
  Sep 4, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  PM nimetaja Tarime kama mfano lakini nilikopita na kuona nilichoandika sio Tarime bali mkoa mwingine tu tena mbunge wao aliyekuwepo alikuwa ni wa CCM akapata katatizo kadogo ka Richmonduli akasagwa na greda.
   
Loading...