"....na mimi natafuta mtu wa kunipa raha" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"....na mimi natafuta mtu wa kunipa raha"

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by ngoshwe, Jan 13, 2012.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Nilianza kumfahamu wakati huo nakwenda sana alipokuwa akifanyia kazi ambapo nilikuwa nikitaka huduma za "Internet" akaanza kuniita kaka....


  Baada ya kupoteana kwa muda, wakati fulani nilikutana nae akanijulisha "kaka naolewa karibuni" nikamwambia jambo la busara, nikampa mchango wa send- off.

  Hatukuwahi kuonana tena kwa muda wa zaidi ya miezi kadhaa..

  Hivi majuzi akanitumia, "heri ya mwaka mpya, ..yaaani sijui kwa nini nimekukumbuka"

  Nikamjibu "nawe pia...Mambo ya Mungu, Mungu kakukumbusha, salamu Mzee bhana"

  Akanirejeshea: "yaani ninyi wanaume balaa..sina raha kabisa na Ndoa yangu"
  Nikauliza "kwa nini??"

  Akanitumia: "Huyu mwanaume mwenzio kaanza vurugu..anarejea nyumbani usiku wa manane...na mimi sana nataka nimwaonyeshe kuwa mwanamke naweza ku- revenge, na mimi natafuta mtu wa kunipa raha ":

  Nilitafakari sana nikaona, moyo unanisukuma niache kutuma ujumbe, yawezekana upande wa pili nawasiliana na mwanaume mwenzangu akinitega...baadae nikaamua kutwanga na akapokea huyo dada akanieleza meengi lakini kwa umakini mkbuwa nilimsihi aendelee kuwa mvumilivu kwani ndoa ni ndoano, kutoka nje ya ndoa kwa mwanamke sio suluhu ya mamatizo ya ndoa. Ilinichukua kama dakika ishirini hivi kueleweka akasema nitaangalia kaka.

  Baada ya kumaliza maongezi hayo, akanitumia ujumbe mfupi: "Nashukuru sana kaka umenipa ushauri mzuri sasa najisikia amani ..nipo nakunywa wine..." nikamjibu: "Ndio suluhu...asante".

  ..akajibu: 'vipi wewe?...nikualike lini kwangu..."

  Mh:....nikajibu "nitakujulisha''


  Leo nimepokea ujumbe,ananiambaia " ..yaani kaka mambo yamekuwa makubwa sana . jamaa amenipiga sana usiku..sasa nifanyeje??"

  Nilishindwa kujibu huo ujumbe...moyoni bado natafakari ni nini hii....??
   
 2. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Huyo yupo directly anatafuta mwanaume wa kujivinjari naye kwa muda ili asahau shida zake kwa muda. na katika kuchanganua hapa na pale ameona akushike wewe, na nakueleza ukiendelea kujimeseji meseji ooh sijui hivi na vile lazima akunase na hapo ndo utajikuta kwenye dimbwi la ulimwengu mwingine...wajanja wengi, hapo kakueleza tu kupigwa sijui anarudi usiku wa manane , bado za chumvi , sukari, mafuta etc
   
 3. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mwambie awajulishe ndugu wa mumewe pamoja na ndugu zake watamwambia cha kufanya kwa sasa. Awaite pia wasimamizi wake wa ndoa watamsaidia!
   
 4. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Kaa mbali nae vinginevyo na wewe utasema "Kwa herini wana JF wenzangu" kama TMK DAR.
   
 5. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  asssuming ni ndoa ya kikristo..........! pole chief endelea kumsaidia uwezavvyo!
   
 6. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  :lol::lol::lol:

  Dah!
   
 7. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  hawana wazazi????

  au watu wakubwa kwao wenye busara wakawashirikisha????

  mana mkuu ukihusika hapo jumba bovu litakuangukia na utaonekana ka source ya yote.
   
 8. F

  Fmewa JF-Expert Member

  #8
  Jan 13, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 294
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hapo wewe hujajua tu. Huyo dada anakutaka kimapenzi ila ameona atumie njia hiyo labda utamhurumia. Mie ninavyofahamu mambo ya ndoa huwezi kumwambia kila mtu ilikuwaje wewe hujaonana nae kwa muda mrefu mmetumiana msg za mwaka mpya halafu ghafla analeta mada za matatizo ya ndoa? hapo kaka unaombwa gemu kaa chonjo wewe mwanaume.
   
 9. Mrembo

  Mrembo JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2012
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 392
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  huyo mwanamke anakutaka. Dah! wanawake wa siku hizi si wavumilivu kabisa kwenye ndoa.
  wana vimbelembele vya kuolewa, maranyingine hata hawajamfaham mwanaume vizuri, inasikitisha sana!

  unapoingia kwenye ndoa inabidi huingie na miguu yote na umwambie mungu wako upo tayari kwa lolote na umuombe akusaidie na uhaidi kuwa muaminifu. Ivi hizi ahadi watu wanazitafakari kweli??? mara nyingine tunajilaani wenyewe kwa kusema uongo mbele za mungu.
  whatever happens in marriage you should never ever think of cheating because it is never a solution.
   
 10. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #10
  Jan 13, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,981
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  kijana changamkia tenda bana....nothing beats the feeling u get wen u sleep with anada mans woman....ila usijedakwa tuu
   
 11. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #11
  Jan 13, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,671
  Trophy Points: 280
  Ushauri mzuri!
   
 12. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #12
  Jan 13, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  alert kwa wanaume mnaopiga waake zenu...
   
 13. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #13
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,302
  Likes Received: 10,339
  Trophy Points: 280
  Usiwe mjinga!!!!!
   
 14. fabinyo

  fabinyo JF-Expert Member

  #14
  Jan 13, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  ......hata picha huelewi?kaa mbali,hana wazazi?
   
 15. Chris_Mambo

  Chris_Mambo JF-Expert Member

  #15
  Jan 13, 2012
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 597
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mnh!..! Sasa nimeshafahamu kwa ninh ukimwi unashambulia sana walio kwenye ndoa!
   
 16. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #16
  Jan 13, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mahusiano yaliyohalalisha kuto tumia kondomu.
   
 17. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #17
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...usijali kaka...amekukumbuka ila nawe jitahidi usimkumbushe mengineyo.
  Achana nae haraka iwezekanavyo!...
   
 18. The Bleiz

  The Bleiz JF-Expert Member

  #18
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 7, 2012
  Messages: 3,643
  Likes Received: 2,113
  Trophy Points: 280
  Ucje ukathubutu kufanya hilo lililokusukuma mpaka kuja kuomba ushauri huku..
   
 19. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #19
  Jan 13, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  eti eeh?? Mdanganyeeee, na zali lote litamuangukia!! Mchezo!!!!
   
 20. T

  TUMY JF-Expert Member

  #20
  Jan 13, 2012
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaa pembeni mapema, kumbuka ni mke wa mtu huyo.Utakuja kuweka mikono kichwani
   
Loading...