Na Malisa G J

Na Malisa G J

selemangrace346

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2018
Posts
468
Reaction score
639
Wakati wa JPM alishtakiwa kwa uhujumu uchumi akasota rumande miaka minne. Mwaka jana akaachiwa kwa NOLE. Aliporejea nyumbani akakuta biashara zake zimekufa. Mke ana mtoto mwingine aliyezaa nje ya ndoa. Mke anadai hakuplan ku-cheat ila changamoto za maisha zilimlazimisha. Baada ya kila kitu kuvurugika na maisha kuwa magumu alimpata "Sponsor" aliyekubali kulea watoto wawili wa jamaa akiwa jela.

Ni "sponsor" huyohuyo aliyelipia gharama za mawakili waliomtetea jamaa hadi kuachiwa huru. Sponsor alitunza familia ya jamaa, akamlipia mawakili, akahakikisha watoto wake wanaendelea kusoma English Medium na hawarudi shule za Kayumba. Akamfungulia mke wa jamaa biashara ya saloon ili aweze kujikimu kwa mahitaji madogo, akamnunulia gari.

Jamaa alipotoka alipata depresion ya maisha, ndoa, uchumi etc. Washkaji zake tulijitahidi kumrudisha sawa lakini it was a locomotive process. Mke alijitetea kwamba yaliyotokea hakukusudia. Aliahidi kukatiza mahusiano na "sponsor" na badala yake watawasiliana kwenye malezi ya mtoto tu. Lakini somo hilo lilikua gumu kwa jamaa.

Jamaa alikua muongeaji sana kabla ya kufungwa. Lakini baada ya kutoka jela akawa mtu mkimya na asiyependa kutoka. Mara zote hujifungia ndani akiwaza na kusoma vitabu. Washkaji zake tuligundua yupo kwenye msongo. Kuporomoka kwa uchumi na kuyumba kwa ndoa yake vilimuumiza sana. Tukaweka utaratibu wa kumtembelea mara kwa mara, kumtia moyo na mara chache kutoka nae out japo kwa kumlazimisha.

Kuhusu mtoto tulimwambia kitanda hakizai haramu. Kuhusu uchumi tulimwambia ajipe moyo atarecorver kwani hayo ni mapito tu. Tulikua tayari kumchangia mtaji kidogo ili aanze kujipanga upya.

Jana nikapata taarifa kuwa ameanguka bafuni. Inadaiwa alipata stroke na mishipa ya kichwa kupasuka. Damu ikavilia kwenye ubongo, akapoteza fahamu. Akakimbizwa hospitali lakini alipofikishwa, madaktari wakasema si yeye bali ni mwili wake tu. Malaika Israel alimtwaa njiani kabla ya kufika hospitali.

Nimeumia sana. Pumzika kamanda. Siku zako nje ya jela zimekua NGUMU SANA kuliko ulipokua jela. Naamini umemsamehe mkeo. Naamini pia umemsamehe JPM aliyevuruga maisha yako na familia yako. Lala salama mwamba. Tutaonana baadae.! [emoji24][emoji24]
 
Ningependa kumjua mtu huyu, maana code iliyotumika kuivumbua mpaka elimu ya Cuba ihusike
 
Hakuna kitu kinauma na kisichosahaulika kwa mwanaume ulie kamilika kama kugongewa na hasa kikawa wazi kwa jamii. Naweza sema hicho kimechangia sana jamaa kumtoa kwenye form.

Kuanguka kiuchumi ni changamoto kama changamoto nyengine katika maisha ukiondoa niliyoitaja hapo ya kimpenzi ila hii unaweza ukalomaa nayo na ukarudi kwenye form cha kuzinga6ia tu umri na viungo vyako kamili unavyo unaweza ingia mtaani kuisaka hela na ukafanokiwa.

R.I. P Bro ila wewe uliyelipia watoto shule, mawakili kumtetea jamaa na mengineyo work done is equal to zero. Bora hata hizo hela ungenywea bia umechangia kuondoka kwa jamaa.
 
Wengine walikuwa wezi kweli, hayo ndo malipo yake.

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
Ulichoandika kina ukweli ndani yake
Ingawa umetumia lugha kali kidigo"malipo yake" coz anayehukumu KIROHO ni MUNGU pekee

Ingawa njia alizotumia magufuri hazikuwa sahihi katika kuwahukumu na kuwafungulia mashitaka
Lakini ukweli MAGUFURI kwa wafunga wa kisiasa wengi aliwaonea

Lakini ukija kwa mafisadi na wakwepa KODI 90% walikuwa WEZI wakwepa KODI wapiga DILI Ukweli usemwe tu

Historia ya JAMAA inasikitisha inahuzunisha
Hili ni FUNZO kwa sisi VIJANA
kila mmoja ajifunze kutokana STORY ilivyo
Ni story kwa uchache lakini Ina MAFUNZO mengi
 
Hakuna kitu kinauma na kisichosahaulika kwa mwanaume ulie kamilika kama kugongewa na hasa kikawa wazi kwa jamii. Naweza sema hicho kimechangia sana jamaa kumtoa kwenye form.

Kuanguka kiuchumi ni changamoto kama changamoto nyengine katika maisha ukiondoa niliyoitaja hapo ya kimpenzi ila hii unaweza ukalomaa nayo na ukarudi kwenye form cha kuzinga6ia tu umri na viungo vyako kamili unavyo unaweza ingia mtaani kuisaka hela na ukafanokiwa.

R.I. P Bro ila wewe uliyelipia watoto shule, mawakili kumtetea jamaa na mengineyo work done is equal to zero. Bora hata hizo hela ungenywea bia umechangia kuondoka kwa jamaa.
Inauma sana tena watu wanajua unaweza kujishtukia kila ukiona watu wamekaa kwamba wanakudiss ni hatari sana kwa afya ya mwanaume.
 
Aseeeh, kitu nilichojifunza kama Mwanaume ni kwamba siku zote niwe na back-up plan haijalishi nitakua stable kiasi gani.

Pili nimejifunza kua watu unao waamini sana ndio siku zote hua chanzo cha kuanguka kwako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata uwe na back-up plans buku usiombe watu wenye mamlaka wakakufanyia figusu.

Kwa hii situation ya mhusika kitu cha kujifunza ni kua maisha yako yanaweza vurugika at any moment.
 
Hata uwe na back-up plans buku usiombe watu wenye mamlaka wakakufanyia figusu.

Kwa hii situation ya mhusika kitu cha kujifunza ni kua maisha yako yanaweza vurugika at any moment.
Kua na back-up plan, maana yake nishaamini na kutambua kua maisha yangu yatavurugika siku moja.

Mfano: kama unamiliki gari na unaamini ipo siku utapata ajari ni lazima utalipa bima bila kusita na hautofanya mchezo kabisa, na hata ikitokea umepata ajali haitukua stresed kwa kua back-plan yako ilikua kwa kulipa bima.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom