Na hili la sakata la kina Jairo na Ngeleja linahitaji kujipima au kamati kujivua magamba?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Na hili la sakata la kina Jairo na Ngeleja linahitaji kujipima au kamati kujivua magamba?!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Japhari Shabani (RIP), Dec 6, 2011.

 1. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #1
  Dec 6, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sasa unakaribia mwezi baada ya tume ya bunge kutoa taarifa kuhusu sakata la Jairo na wenzake kukusanya pesa kinyume cha sheria(Ufisadi)Ushahidi uliaanishwa wazi na mapendekezo ya hatua ya kuchukuliwa kwa wahusika.Ni mategemeo ya wengi yalikua kwa wahusika waliotajwa watajiuzulu au kufukuzwa kazi na kufikishwa vyombo vya sheria,lakini mpaka sasa hakuna chochote kilichotokea watu hao wanaendelea na shughuli zao kama kawaida,au na wao wanapashwa kupewa muda wajipime na kuchukua hatua?Au wanahitaji kuudiwa kamati ya kuwalazimisha kujivua nafasi zao?! Hii inatoa picha na funzo lipi kwa jamii?Kwanza ni mfano upi kwa wizara na taasisi za serikali zinazofanya ufisadi?Je pesa iliyotumika kwa kamati iliyoundwa kwa kuchunguza sakata hilo imepotea bure?!Kwani kuunda kamati ambayo maamuzi yake hayatekelezwi ni ufisadi juu ya ufisadi na kuwabebesha walipa kodi gharama zisizo na tija.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 2. ntogwisangu

  ntogwisangu JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 516
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  hii ndo Tanzania tuijuayo!acha gubu!!!!wenzenu wakila kazi kuwafuatilia!!!!!mliwachagua wa nini sasa!!!laumu akili yako kushindwa fanya maamuzi au pindua uongozi kama unaweza kama walivyofanya Sadam Hussein na Muamar Ghadafi!!!!!!vinginevyo jinyonge!!!!
   
 3. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #3
  Dec 6, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Inamuwia vigumu Kikwete kuwachukulia hatua stahiki hawa mafisadi kwasababu moja kubwa nayo ni kwamba matendo yote ya Jairo na Luhanjo yalikuwa na baraka zake!! Sasa kuonesha jeuri yake kwa wananchi waliomchagua, anakaa kimya na kuwaruhusu hawa jamaa wafikishe umri wao wa kustaafu halafu waondoke na kiinua mgongo na pension juu ya hizo walizokwiba. Ingekuwa amri yangu ningewafungulia wote walioko jela wawe huru kwani Rais wetu anawalinda wahalifu wakubwa na kuwafunga waiba kuku tu!!
   
 4. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #4
  Dec 6, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lowasa amesema wazi kuwa 'DILI LA RICHMOND' hakuwa peke yake, sasa wewe unadhani 'DILI LA JAIRO' yuko peke yake? Rais anajua akiamua kuchukua hatua atafagia wizara nzima. :canada:
   
 5. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #5
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Tanzania ni zaidi ya uijuavyo si ajabu kusikia rais kaunda tume nyingine.
   
 6. l

  limited JF-Expert Member

  #6
  Dec 6, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 300
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  under ccm ruling? no way
   
 7. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #7
  Dec 6, 2011
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Serikali iko busy na MIAKA 50 YA UHURU kuawaalika watu wakimaliza ndio watawafukuza endelea kusubiri
   
 8. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #8
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Hivi nani alishawahi kufukuzwa kazi kwa kuboronga hapa bongo zaidi ya kuhamishiwa sehem nyingine akaboronge zaidi
  May be yule mkuu wa wilaya aliyechapa walimu viboko
  Ila hawa wengine wanahamishiwa tuu sehem nyingine wakafanye madudu zaidi

  tanzania zaidi ya uijuavyo
   
 9. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #9
  Dec 6, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  bado wapo katika mchakato; mchakato ambao hautaisha hadi Jairo na Katibu Mkuu Kiongozi muda wao muafaka wa kustaafu utumishi wa umma utakapofikia (ref. Mnyika case vc Richmond). that is made in Tanzania only!
   
 10. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #10
  Dec 6, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hakuna hata mmoja ambaye atajiuzulu maana hata wakubwa wao walipewa pesa hizo na walikuwa wanajua kila kinachoendelea.
   
 11. m

  matawi JF-Expert Member

  #11
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Luhanjo anastaafu december mwishoni tunaona tuvute muda atoke akiwa mstaafu badala ya kufukuzwa. Ni dingi yangu samahanini sana
   
 12. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #12
  Dec 6, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kwani hujui kuwa hizo ripoti zatume huwa ni kiini macho,hapo ndo ishatoka.
   
Loading...