N

twende kazi

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,517
1,500
Yeyote anayeteseka na roho hii na umetamani sana kuacha, Kwanza kabla ya yote, tafuta kujua kwanini unataka kupiga punyeto? Inakuathiri vipi kwenye maisha yako? Na hii tabia chafu umeitoa wapi? Nk na baada ya kupata ufahamu kuhusu tabia hii chafu unayotaka kuiacha, ufahamu wako utakurahisishia, utakupa nguvu ya kuweza kuacha. Sasa, tuone Neno la Mungu kuhusu punyeto.

Mwanzo 38:9-10 Onani mtoto wa Yuda alimwaga mbegu zake nje, kwa sababu hakutaka kumpa uzao yule mke wa ndugu yake. Mungu alimuua Onani sababu tu, alimwaga mbegu zake nje….
Mambo ya Walawi imeandikwa sura ya 15:16-17 “Na mtu yeyote akitokwa na shahawa yake, ndipo ataoga mwili wake wote majini, naye atakuwa najisi hata jioni. Na kila nguo, na kila ngozi, ambayo ina shahawa, itafuliwa kwa maji, nayo itakuwa najisi hata jioni”

Mtu yeyote anayetoa mbegu zake nje, au anayetoa kwenye mazingira machafu. Mtu huyo ni najisi.
Marko 1:23 “Na mara palikuwapo ndani ya sinagogi lao mtu mwenye pepo mchafu; akapaza sauti…..
Pepo wachafu wanaozunguka kwenye hewa wakimtafuta mtu gani wa kumwingilia, wanatafuta mtu anayewaza uchafu na wanafanya lolote lililo nje ya Neno la Mungu. Kuanzia kwenye ufahamu wako mpaka unafanya halisi.

Kwahiyo wanaopiga punyeto pepo wachafu wanamvaa mtu huyo kwa sababu anawaza mambo machafu na kujikuta anafanya kituko hicho kichafu, sasa baada ya kufanya hivyo (kutoa mbegu, shahawa au kufanya ngono) pepo wachafu wanapata uhalali wa kumvaa mtu huyo na kumvika tabia chafu sugu.
Ili utoke kwenye kifungo hiki, inabidi kuwaza mawazo masafi, kufuata, kujifunza kanuni za utakatifu. Kwasababu kinyume cha najisi/uchafu…ni utakatifu. Kuishi maisha ya utakatifu na kuachana na uchafu wote.

Marko 1: 27 “Wakashangaa wote, hata wakaulizana, wakisema. Nini hii? Ni elimu mpya! Maana kwa uweza awaamuru hata pepo wachafu, nao wamtii”
Masturbation ni kitendo kichafu kinacho shawishi kukuingiza kwenye uwepo wa hali ya kufanya mambo machafu (kwasababu kupitia masturbation watu wanatoa mbegu zao nje kwenye uwepo wa roho chafu. Sasa hizi roho zinapata uhalali wa kukumilikisha tabia nyingine chafu) hautaishia kwenye kupiga punyeto tu!!!

Kitu kinachotakiwa kwako, ni kupata mafundisho kutoka watumishi wa Mungu ambao watakusaidia uache tabia hiyo, watumishi wanaoishi maisha yenye utakatifu, ukisikiliza mafundisho yao, na kumtii Mungu. Ule utii utakupa uwepo mtakatifu kwenye maisha yako ambao utaondoa tabia chafu ya kufanya masturabation.

Kumbuka kutubu kwenye maombi yako na utamke tatizo hili, pia kataa mazingira yaliyoifunga nafsi yako kukuunganisha kwenye maisha yako na kupiga punyeto.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom