N CARD mnatuangusha.

N CARD mnatuangusha.

billgate

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2021
Posts
378
Reaction score
500
Wadau,

Nawasalimu.

Kwa masikitiko makubwa napenda kulalamika juu ya kadi zinazotumika kuvuka kwenye pantoni maarufu kama N CARD,tangu Ijumaa wiki iliyopita kumekuwa na sintofamu kwa wateja waliokuwa wameweka pesa kwenye card zao unakuta card ina pesa ya kutosha lakini kila ukichanja inakwambia NO ENOUGH BALANCE 😕

Wananchi tumepata usumbufu usiopimika kila kona ilikuwa ni malalamiko na kuna ambao tumeanza kuwa na mashaka juu ya card hizo na tunafikiria kurudi kwenye old way ya kulipa 200 daily kila unapovuka, kwa sababu haya matukio yanatokea sana,unaweza kuweka 5000/= ukavuka siku 4 unaambiwa pesa imeisha.

Mamlaka zinazohusika tusaidieni wananchi tunateseka.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom