Mzushi anatabiri obvious | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzushi anatabiri obvious

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lutala, Feb 25, 2011.

 1. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #1
  Feb 25, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Sheikh Yahya Hussein: Serikali zisizotimiza ahadi kuangushwa

  Mnajimu maarufu Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein

  Mnajimu maarufu Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein, ametabiri kuwa serikali ambazo hazitatimiza ahadi kwa wananchi zitaangushwa na kwamba siri nyingi za serikali zitavuja.
  Kadhalika, amesema ndani ya miaka saba kuanzia Machi 13, mwaka huu, kutatokea machafuko, maandamano, uasi, maasi na kupinduliwa kwa serikali mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania.
  Katika taarifa iliyosomwa jana jijini Dar es Salaam na mtoto wake, Hassan Yahya Hussein kwa niaba yake, ilisema mambo hayo yatatokea kuanzia mwezi huo na yataendelea ndani ya kipindi cha miaka saba.
  Sheikh Yahya alisema mambo hayo yatatokea baada ya kuja kwa sayari ya Uranus ambayo itaingia katika nyota ya Punda (Aries).
  Alisema sayari hiyo huzizunguka nyota zote kwa miaka 84 na hukaa ndani ya nyota hiyo kwa kipindi cha miaka saba.
  Alitaja mambo mengine yatakayojitokeza baada ya kuja kwa sayari hiyo kuwa ni mabadiliko ya ghafla ya kisiasa na kijamii, kuwepo kwa msukumo wa ghafla wa kufanya jambo, kuzinduka kwa watu kifikra na kutaka kujua ukweli na uwazi wa mambo yaliyojificha.
  Mengine ni watu kudai haki zao kwa nguvu ambapo wataungana pamoja kupinga serikali na taasisi kubwa ambazo zitakuwa zinawatungia sheria na kanuni na kuwawekea vikwazo.
  Alisema hilo litasambaa katika siasa na kwenye midahalo mbalimbali.
  Pia alisema kuanzia Julai, mwaka huu kutatokea mapinduzi ambapo polisi watafumaniwa kwenye maboma yao.
  Alisema kutokana na ujio wa sayari hiyo ametabiri mwaka huu kutakuwa na mafanikio katika ugunduzi wa mambo ya afya ambapo wataalamu watavumbua dawa mpya ya kutibu magonjwa mengi.
  Alisema wanasayansi watafanikiwa kugundua mbinu mpya za kutibu magonjwa yasiyokuwa na tiba kama Ukimwi na kansa.
  Sheikh Yahya alisema kuanzia Januari 23, mwaka huu sayari ya Jupiter imeingia katika nyota ya Punda ambapo utabiri wake unaonyesha kuwa kutasikika habari nyingi kuhusiana na masuala ya michezo na wanamichezo.
  Alisema wakati utabiri wake ukimuonyesha kuwa watu hao watapata mafanikio na umaarufu, kutasikika habari za vifo vya wanamichezo, wasanii na waandishi wa habari maarufu hapa nchini.
  Alisema sayari ya Jupiter itaingia katika nyota ya ng'ombe Juni 4, mwaka huu ambapo itakaa huko hadi mwishoni mwa mwaka.
  Alisema utabiri wake unaonyesha kutakuwa na mafanikio makubwa kwa watu wanaofanya biashara ya kujenga majumba na kuyauza au kuyapangisha kutokana na soko lao kuongezeka.
  Sheikh Yahya alisema Aprili 4, mwaka huu sayari ya Neptune itaingia katika nyota ya Samaki ambapo utabiri wake unaonyesha kuwa kutakuwa na mabadiliko mengi ya hali ya hewa sehemu mbalimbali duniani.
  Alisema kwa upande wa Tanzania wananchi wategemee kusikia habari za ukame na ukosefu wa maji kuanzia mwezi Aprili hadi Agosti mwaka huu.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kazee kamechoka kweli sasa hivi

  yaani kalikuwa kanatabiri uwongo wake huku kana kigugumizi

  kanatia huruma kweli
   
 3. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Analeta stori za utabiri wakati mziki ushaeleweka huko nort afrika na dunia ya kiarabu. HILO NI JAMBO DHAHIRI AMABALO liankuja na halihitaji utabiri
   
 4. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #4
  Feb 25, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Kweli ndugu Mageuzi Kizee kimechoka vibaya
   
 5. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #5
  Feb 25, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hakina sera sasa hivi kimeamua kitoke wakione bado kipokipo ndugu yangu lutala
   
 6. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  JK sijui kapata utabili huu bcs ndo mkuu wake huyu wamambo ya ulinzi!
   
 7. Muro

  Muro Senior Member

  #7
  Feb 25, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 168
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Amechoka lakini mkumbuke kuwa utabiri ni taaluma kama taaluma nyingine huyu ameenda shule ya mambo hayo kutokana na imani ya dini yake hakuna sababu ya kumbeza,hata hivyo mengi aliyotabiri yametokea hata hapa TZ,kama ninakumbuka alitabiri kurudi kwa kishindo kwa lowasa katika anga za siasa si mumeona wenyewe bunge lililopita kwa kishindo kachaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya bunge ya Ulinzi na Usalama tena hata wabunge wa upinzani walimkubali,hiyo ni ishara tosha kuwa hata hiyo 2015 katika CCM akipeleka jina kuna hatihati akarudi kama mgombea,ni vizuri kusoma alama za nyakati na hata haya mageuzi huko ughaibuni aliwahi kuyataja.:mullet::A S 13:
   
 8. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #8
  Feb 25, 2011
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  ...Suala ni Kusoma alama za nyakati na sio hadithi za sijui Nyota ya venus imekaa kushoto kwa Mars blah blah blah...!
   
 9. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #9
  Feb 25, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Alitabili kuwa uchaguzi ungeahilishwa na kweli hatukuwa na uchaguzi bali uchakachuaji mwaka jana!!
   
 10. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #10
  Feb 25, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  deen ile kumbe imekaa kitabiri tabiri???
   
 11. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #11
  Feb 25, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kazee kamekosa sera
   
 12. M

  Marytina JF-Expert Member

  #12
  Feb 25, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Kanafanana na Makamba au mnasemaje?
   
 13. matungusha

  matungusha JF-Expert Member

  #13
  Feb 25, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  mmmmh!! JK atam fire kama alivyomfanyia Tido!!! yangu maskio
   
 14. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #14
  Feb 25, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Huyu mzee amekorofishana na CCm nini!!
   
Loading...