Kijakazi
Platinum Member
- Jun 26, 2007
- 10,603
- 18,244
Hili swala la hawa wanaoitwa Waisrael huko Palestina mpaka leo hii nashindwa kulielewa, kwa maana unakuta Mtu ukimuangalia ana macho ya bluu kabisa na nywele za rangi ya njano au sijui blond kama zinavyojulikina kwa wenyewe Wazungu lakini anakwambia ya kwamba kwao ni Palestina/Israel, sasa nikifikiria Palestina kijiografia iko Mashariki ya kati na ni Jangwa ama Jangwani sasa watu waishio au wenye asili ya jangwani na macho ya bluu na nywele blondi wapi na wapi?
Yaani kama kweli hao jamaa (Wayahudi) hiyo ni ardhi yao ya asili Je, Macho ya bluu na nywele za Bond walizipata wapi? Kwa maana asili ya watu wa hivyo ni Ulaya huko kwenye baridi ndiyo utakuta kuna Watu wana macho ya bluu na nywele blond lkn SIYO Jangwani Mashariki ya kati!
Ni kama mimi ukiniangalia ni mweusi nina nywele ngumu hivyo asili yangu ni hapa hapa kwenye ardhi ya TZ sasa siwezi leo hii kwenda kwenye milima ya Bhutani huko Asia nikasema mimi asili yangu ni Bhutani hata watu wa huko watanishangaa kwa maana sifanani nao, sasa hawa Wazungu Wayahudi macho ya bluu na nywele Blondi walipata wapi kama asili yao ni Jangwani?