Mzungu mmoja ambaye sikuweza kufahamu jina lake aliamua kuvua nguo zake zote akiacha ya ndani tu baada ya wakaguzi wa uwanja wa ndege Dar kuwa na wasiwasi nae.
Katika tukio hilo la aina yake leo Jan 28 asubuhi, mzungu huyo aliona ni bora achukue hatua hiyo baada ya kila akipita ktk zile mashine za kukagulia wasafiri wa ndege hapo uwanjani kupiga kelele. Cha ajabu zaid hata pale alipovua nguo na kupita bado mashine ilitoa mlio, ambapo iliwalazimu wakaguzi kwenda kumkagua kwa undani ktk vyumba vya ndani hapo airport, ambapo hakugundulika na kitu chochote cha hatari badala yake ikagundulika mashine ya ukaguzi ilikuwa mbovu.
Watu wengi waliokuwa karibu na eneo hilo walishtushwa na hatua ya huyo mzungu lakin wakatoa lawama kwa uongozi wa airport.
Baadae mzungu huyo aliruhusiwa kuendelea na safari yake na ametishia lazima akaushitaki uwanja kwa Baraza la Viwanja vya ndege Duniani
Habari hii nimeikusanya mimi mwenyewe CPU nilipokuwa ktk eneo la tukio
Akashtaki kokote!
Kwani alilazimishwa kuvua nguo zote au alitaka mwenyewe kuvua? Mbona inapotokea kuwa mashine imetoka mlio unapopita wanakukagua bila kukutoa nguo zako! Mimi nashangaa hawa wazungu. Wakiwa kwetu wanataka wasipitie taratibu.Kitendo cha yeye " kuvua nguo zote" nakitafsiri kama dharau.Huko kwao tukienda mbona tunasumbuliwa hivyo hivyo tena kibaya zaidi wanaweza kuacha kila mtu wakakuchukua wewe mtu mweusi na kusema computer imeku pick randomly for thorough search..huwa hatupendi lakini kwa vile ni sheria za usalama basi huwa tunakubali.Tena wakati mwingine wanakulazimisha utoe viatu wavifanyie swabbing..vyote tunapambana navyo na hatujawahi kutishia kwenda kushtaki kokote.Hizi taratibu za ukaguzi ni za kimataifa..akashtaki popote!
angevua hata chupi. wao kwao mmatumbi ukiingia hata supermarket camera zote za ulinzi zinaelekezwa kwako.
Hivi chupi sio nguo??????????????????
umeongea vyema kabisa,ukiingia dukani atawaacha watu wote aje akuulize akusaidie nini?angevua hata chupi. wao kwao mmatumbi ukiingia hata supermarket camera zote za ulinzi zinaelekezwa kwako.
Mzungu mmoja ambaye sikuweza kufahamu jina lake aliamua kuvua nguo zake zote akiacha ya ndani tu baada ya wakaguzi wa uwanja wa ndege Dar kuwa na wasiwasi nae.
Katika tukio hilo la aina yake leo Jan 28 asubuhi, mzungu huyo aliona ni bora achukue hatua hiyo baada ya kila akipita ktk zile mashine za kukagulia wasafiri wa ndege hapo uwanjani kupiga kelele. Cha ajabu zaid hata pale alipovua nguo na kupita bado mashine ilitoa mlio, ambapo iliwalazimu wakaguzi kwenda kumkagua kwa undani ktk vyumba vya ndani hapo airport, ambapo hakugundulika na kitu chochote cha hatari badala yake ikagundulika mashine ya ukaguzi ilikuwa mbovu.
Watu wengi waliokuwa karibu na eneo hilo walishtushwa na hatua ya huyo mzungu lakin wakatoa lawama kwa uongozi wa airport.
Baadae mzungu huyo aliruhusiwa kuendelea na safari yake na ametishia lazima akaushitaki uwanja kwa Baraza la Viwanja vya ndege Duniani
Habari hii nimeikusanya mimi mwenyewe CPU nilipokuwa ktk eneo la tukio
Chukua na Kamera halafu utuwekee picha zako hapa JF ili tuzichakachue!!!ntaenda na mimi nikapite tu ili .....manake jua limezd jooooto mweeeee!!!
ntaenda na mimi nikapite tu ili .....manake jua limezd jooooto mweeeee!!!
Hahahah ni wa kiume bwana, ila alikuwa na mtalimbo haswaaaa teh teh teh