Mkuu, naomba ufikiri zaidi. Unafikiri kuitwa shule ya wanafunzi wenye vipaji maalum kuna halalisha serikali kutoijali shule hiyo? Walisema walimu ni WITO na wakatumia kigezo hicho kuwakandamiza walimu mpaka walimu walipokuja kushituka sasa hivi nao wanaipigia kelele serikali. Najua, Mkuu wewe huwa unaitetea serikali huenda una hisa zako huko, lakini muhimu utambue kuwa pamoja na vipaji lakini hao pia ni watu sawa na watu wengine, wote huhitaji yote ambayo wengine wanayapata. Mpaka wamefika hapo bila shaka wamechoka.
Tatizo mnaongea kiuanaharakati.
Hapo ulipo hujui mimi personally ninafanya jitihada gani kuhusu kuboresha Mzumbe. Kwa hiyo shutuma zako ziweke akiba kwanza.
Ukisoma vizuri na kuweka uanaharakati pembeni utaelewa ninachosema. Ila kama lengo lako ni kupindisha taarifa ili kuhalalisha uanaharakati basi endeleeni, lakini kuweki aware kuwa HAMTAFANIKIWA kwa njia mliyochagua.
Ninachosema ni hiki:
1. Matatizo ya miundombinu ni matatizo ya muda mrefu. Je, ni kwanini wanafunzi wamesubiri mpaka kipindi cha mitihani ndio waamue kuandamana?
2. Je, tathmini iliyofanywa na wanafunzi hao inaonyesha kuandamana kutawezesha vipi kutartua matatizo ya miundombinu?
3. Je, ni jitihada gani zimeshafanyika mpaka kufikia uamuzi huo wa kuandamana? Mwali Msuka wa Mzumbe aliwafundisha wanafunzi siku zote kwa ukifanya mambo kwa kufuata "right channel" utafanikiwa. Je, ni channel ipi mmefuata?
Hawa wanafunzi mimi ni wadogo zangu, na wewe kama ni miongoni mwao basi ni mdogo wangu na ni vema mkawa watlivu kusikiliza ushauri tunaowapa.
Mwanafunzi wa sekondari anatumia kati ya miaka 2 na 4 shuleni. Kwa kipindi hicho ni muhimu sana kubalance vipaumbele.
Kufanya maandamano kwa mguu mpaka Dodoma kwanza kunaashiria tatizo la fikra na pili inaashiria kushindwa kupanga vipaumbele ipasavyo. Kipindi cha mitihani ni kipindi maalum ambacho wanafunzi hata muda wao wa kula na kulala unategemewa kubadilika, huu sio muda wa kuandamana kwa matatizo chronic.