Mzumbe Sec Waandamana

Mzumbe Sec Waandamana

Mchumia Rungu

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2013
Posts
1,439
Reaction score
826
Hii leo wanafunzi wa Mzumbe Sekondari wanaandamana kuelekea bungeni Dodoma kimakundi makundi. Wana shida ambazo uongozi aw shule umeshindwa kutatua bila shaka!

Kundi moja limezuiwa na kundi kubwa la Polisi maeneo ya Kasanga hapa hapa Morogoro. Picha na habari zaidi mtaletewa wadau.
 
Kasanga au Sangasanga?

Ni matatizo gani wanapeleka Bungeni? Je, mbunge wao wameshindwa kumwambia?
 
usije ukashangaa siasa za majitaka zina mkono wake ndani..
 
Wanaandama hadi bungeni Dodoma? au hii si Mzumbe Sec ya Moro!
 
Hawa nao hamnazo yaani wanandama kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine kwa miguu kweli siku hiz demostration imekuwa kama vituko vya wema na Diamond
 
Kasanga au Sangasanga?

Ni matatizo gani wanapeleka Bungeni? Je, mbunge wao wameshindwa kumwambia?

Ni nyuma kidogo ya Kasanga, Maliasili. Matatizo yao ni mengi. Ujue shule ya Mzumbe ni ya siku nyingi, imechoka! Na Headmaster, Njawa, ni kijana na hana uwezo wa kuwavuta wakubwa huko serikalini ili waendelee kujali shule hiyo. Hivyo matatizo yaliopo Mzumbe ni makubwa kuliko umri wa huyo headmaster. Na serikali inataka kuziweka shule zote kuwa za kata kwa ukata! Inaumiza hata shule zake za wanafunzi wenye vipaji?! Bogus government!
 
usije ukashangaa siasa za majitaka zina mkono wake ndani..

Atakayesema hivyo, atakuwa haijui Mzumbe na wanafunzi wanaosoma hapo. Kiasi fulani wanafunzi waliopo hapo huwa kama watu wazima vile! Lakini wasemaji huwa hawakosi la kusema.
 
Haaaa vipaji maalumu kipekee kiakili from moro to dom.

Hicho nacho ni kipaji. Wako waliotembea kuliko umbali huo na wako katika vitambu vya kumbukumbu. Ila sema hawa wanafunzi sijaona kubeba masurufu! Labda masurufu yao ni kila mmoja hela mfukoni.
 
Wanaandama hadi bungeni Dodoma? au hii si Mzumbe Sec ya Moro!

Mkuu ndiyo hiyo. Na wote wako ndani ya uniform wanataka kuonyesha kuwa tendo la kuandamana ni sawa tu kuwa wako darasani.
 
Hawa nao hamnazo yaani wanandama kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine kwa miguu kweli siku hiz demostration imekuwa kama vituko vya wema na Diamond

Hakuna jipya hapo Mkuu. Kama ni kutembea kwa miguu, wako waliotembea zaidi ya mkoa hadi mkoa na tunasoma habari zao katika vitabu vya historia.
 
Mtasema CHADEMA wamewahamaishaa !

Mbegu ya CHADEMA inafanya kazi. CHADEMA wametufundisha kutokuwa waoga na Watanzania walio wengi sasa wana moyo wa kihivyo. Na tutakuwa tumepiga hatu kuwa na taifa la watu majasiri wanaoweza kusema HAPATA na kuamua waonavyo wao.
 
Mkuu ndiyo hiyo. Na wote wako ndani ya uniform wanataka kuonyesha kuwa tendo la kuandamana ni sawa tu kuwa wako darasani.

Dodoma ni mbali sana kutokea Mzumbe mkuu, nadhani hawatafika hata hapo Moro mjini watakuwa washazuiwa na Polisi...
Watafute namna nyingine ya kuwakilisha matatizo yao.
 
Mbegu ya CHADEMA inafanya kazi. CHADEMA wametufundisha kutokuwa waoga na Watanzania walio wengi sasa wana moyo wa kihivyo. Na tutakuwa tumepiga hatu kuwa na taifa la watu majasiri wanaoweza kusema HAPATA na kuamua waonavyo wao.

Na hili ndilo linalowawia vigumu ccm kuiongoza nchi kwani awali ilikuwa ikiongoza waoga na wajinga na sasa ni wasomi na wajanja mtaacha kutoka madarakani kweli?
 
Du embu tusikie baadae wangapi watadondokewa na vitu vyenye ncha kali
 
Back
Top Bottom