Singida ndio home
JF-Expert Member
- Feb 23, 2012
- 3,192
- 3,353
Hakunaga ubaguzi mbaya kama ule wa kujaribu kufanya kitu tofauti kionekane sawa na vingine vilivyofanana. Ni ubaguzi mkubwa kwa kukifanya hiki Chuo cha Mzumbe kionekane sawa na vingine wakati kuhalisia Chuo cha Mzumbe hakijafikia kitaaluma kama vingine.
Hapa sizungumzii maneno matupu naongea kwa ushahidi kabisa, kusomea Chuo cha Mzumbe ni rahisi mno mtu kufaulu ukilinganisha na vyuo vingine.
Wale tuliosoma vyuo tunajua kwamba Degree nyingi zina semester sita, kila semester ina masomo yake na kila semester mtu anapata GPA kulingana na ufaulu wake katika masomo aliyosoma kwenye semester nzima.
Vyuo vingi somo la field training huwa linakuwa limeunganishwa kwenye semester ya nne ya mwaka wa pili, semester hii ya nne inaweza ikawa na masomo ya darasani matano na la sita ndio field work inayofanyika chuo kikifungwa. Hivyo nayo field work inajumuishwa na masomo hayo matano ili kupata GPA.
Cha ajabu wenzetu semester nzima inatumika kufanya hiyo field work pekee, yaani hii semesta haina masomo yoyote zaidi ya field, mtu akipata A ya field basi kachukua marks 5 zote za kwenye GPA ya semester tofauti na vyuo vingine ambavyo hata ukipata A ya field work unaweza kujikuta umeambulia GPA ya 3.7 ikijumuishwa na masomo mengine.
Kupata A ya field work Mzumbe ni sawa na mtu aliesoma UDSM, IFM, IAA Arusha, TIA, n,k kupiga “A” masomo yote matano kwenye semester nzima kitu ambacho ni nadra sana.
Hali hii inachangia mhitimu apate GPA ya juu kuliko wa vyuo vingine na hata kuwa na uhakika zaidi wa kupata Second Upper Class kuliko wa vyuo vingine kama uonavyo hapa chini.
Nadhani suluhisho la kuleta haki ni kukifanya hiki chuo kiwe na semester tano, hio field ijumuishwe na masomo mengine ya semester ya nne, Haiwezekani mtu anakula GPA ya 5 kirahisi rashi yupo field wakati wenzake wanapambania hio GPA darasani.