SubiriJibu
JF-Expert Member
- Jun 26, 2009
- 1,803
- 1,863
Inawezekana kweli lakini bado kuna makandokando kibao, tuliingia mkataba na Barrick lakini mlipa kodi anayejulikana TRA ni Acacia na aliyesajiliwa soko la hisa ni Acacia. Mkuu inahitaji uchambauzi makini wa wasomi wetu watusaidie kututoa kwenye hili giza binafsi napongeza juhudi za Mh Rais hata kama tusipopata kitu tumeionesha dunia kuwa tunaweza kuunguruma kama nchi.
Wanasheria mnaosoma uzi huu naomba msaidie ili tuelewe jambo hili. Wote tumesikia lugha nyingi lakini walau kuna maneno mawili yanatamkwa kwenye mgogoro huu nayo ni BARICK na ACACIA.
Kama umezoea kusoma thread fupifupi basi ni bira kabisa usisome uzi huu kwa sababu jambo lenyewe si rahisi kama wengi wanavyoepnda iwe kulingana na mkondo wa kisiasa wanaoutaka.
Imeshaelezwa mara kadhaa kwamba BARICK ndiyo wenye hisa 63.9 ndani ya ACACIA kule kwao na hivyo wanahisa wengine wanamiliki asilimia 36.1. Hii maana yake ni kwamba BARICK na ACACIA ni kampuni mbili tofauti. Walahu hadi hapa wengi wanaelewa.
Sasa kama ni kampuni mbili tofauti, hata kama wanategemeana kivyao, utofauti uko palepale, hauondoi kwamba hizi ni kampuni mbili tofauti hata kama zote zingekuwa pale London bado zingejisajili kwa utofauti.
Unapoufungua kampuni katika nchi yoyote lazim huko ujisajili. Kujisajili kunakufanya uwe na haki za kibinadamu ziitwazo "legal personality", yaani uingie mikataba, ushitakike, ushitaki.
Hivyo, kama kampuni haijajisali hapo nchini Tanzania, maana yake kwamba haitambuliki, mikataba yake ni fake, haishitakiki na haiwezi kukushitaki. Kwa kifupi ni kampuni hewa. Nadhani hapo hata kama hukuwa unajua utajua.
Taabu inakuja kwamba ni sheria ipi inatambua kampuni. Kama ni madaktari ingawa si kampuni nadhani wizara ya afya ina jinsi ya kuwatambua madktari wanaokuja nchini. Kama ni ma-injinia kuna Engineers Registration Board (ERB) ili ufanye kazi za uinjinia au engineering consultant hapo nchini.
Kama ni wakili huwezi kuna namna ya kujisajili ili ufanye kazi mahakama za hapo nchini, kama sikosei kuna advocate act. Kama ni benko nadhani unajisajili BoT.
Narudia, ukishajisajili unapata ile "legal personality" yaani unashitakika, unashitaki unaingia mikataba ikiwemo ya kuajiri wafanyakazi.
Tuje sasa kwenye sakata hili la BARICK na ACACIA. Je, zilistahili kusajili wapi?
Kwa sababu zote ni kampuni ungedhani zote zingesajiliwa kwa mujibu wa sheria ya makampuni yaani The Companies Act, (Cap 212, R.E. 2002). Lakini ni wazi kwamba moja (BARICK) imesajiliwa BRELA kwa mujibu wa The Companies Act, (Cap 212, R.E. 2002). na nyingine (ACACIA) imesajiliwa kwenye soko la hisa, kama sijakosea kwa mujibu wa sheria za soko la hisa, ambayo mimi kw aujinga wangu ninaijua moja tu, Capital Markets and Securities Act, Chapter 79 R.E. 2002 na mnaoelewa zaid mtaongezea.
Nimeleta thread nikiwa nina hisia hizo nikijua kwamba jambo hili linahitaji uelewa na humu wamo wenye uelewa na inawezekana siko sahihi.
Lakini ninaona kwamba ni kwa jinsi hiyo tu ambapo unaweza kuiona ACACIA ni kampuni halali na ndiyo maana inaonekana hata TRA.
Kama ni hivyo, basi ni kwa namna hiyo basi ACACIA inatakiwa kuonekana kwamba ni kampuni halali kama kuna moja ya sheria inayoitambua, yaani sheria zinazohusiana na soko la hisa kama moja niliyoitaja yaani Capital Markets and Securities Act, Chapter 79 R.E. 2002 .
Kw alugha ya kisheria, kama kusajiliwa pale DSE kunatosha kuifanya ACACIA ionekane ndiyo biashara yake, yaani hisa tu, basi lilikuwa ni kosa la ufundi kueleza uma kwamba ACACIA haionekani BRELA kwa mujibu wa The Companies Act, (Cap 212, R.E. 2002). wakati waliosema hivyo hawakutueleza mahitaji ya sheria za hisa ikiwemo Capital Markets and Securities Act, Chapter 79 R.E. 2002.
Matokeo yake sasa hivi Waziri ametoka kushughulika na BARICK kwa siku zaidi ya 80, tukadhani tumemaliza lakini hapohapo ACACIA ni kama ametuweka kisaikolojia kwamba tusishangae ukizok mgogor mpya yaani ngoma bado ni mbichi.
Huwezi kumaliza mgogoro kwa njia ya makubaliano yanayosaniwa mbele ya Rais, halafu kampuni inasema bado ni "subject to approval" yaani kumbe kuna kipande cha kampuni kinasema hayo mliyosainiana huko Dar hawayatambui hadi watakapokaa na kuona kama yanafaa au la na yasipofaa wanajua hatua watakazochukua.
Narudia, nimeanzisha tread kwa minajiri ya kutaka kujua yaani curiosiry tena hasa baada ya msimamo mpya wa ACACIA baada ya mazungumzo.
Mnaoelewa tiririkeni.