Mzizi wa Mandela Tanzania - haya ndio maisha yake mkoani kilimanjaro

malenga wetu

JF-Expert Member
Jan 31, 2013
283
170
Zipo taarifa kwamba kabla ya kufungwa jela, Marehemu Nelson Mandela aliwahi kuishi nchini Tanzania na familia moja ambapo wakati anaondoka aliacha baadhi ya vitu, vikiwemo viatu .

Katika mwaka wa 1962 Nelson Mandela aliondoka Afrika kusini kisirisiri na kwa muda wa miezi saba alikuwa akitembelea mataifa mengi ya bara la Afrika.Chama cha African National Congress, ambacho kilikuwa ndio kimepigwa marufuku na utawala wa ubaguzi, kilikuwa kimeanzisha mapambano ya kijeshi kupitia jeshi lake la Umkhonto we Sizwe.

Kazi ya mandela ilikuwa ni kutafuta uungwaji mkono wa hali na mali kutoka mataifa mengine ya Afrika na pia kutafuta mataifa yaliyo tayari kuwapa mafunzo ya kijeshi makurutu wake akiwemo yeye mwenyewe.Alipata mafunzo ya kijeshi nchini Morocco, kutoka kwa wanajeshi wa Algeria waliokuwa wanatumia ardhi ya Morocco kama kituo chao kupigana dhidi ya utawala wa kikoloni wa Ufaransa.Mafunzo mengine yalifanyika Ethiopia.

Katika kuangalia safari ya maisha ya Nelson Mandela zipo taarifa kwamba kabla ya kufungwa jela, Marehemu Nelson Mandela aliwahi kuishi nchini Tanzania katika familia moja ambapo wakati anaondoka aliacha baadhi ya vitu, vikiwemo viatu .

John Solombi aliitembelea familia hiyo iliopo Kilimanjaro kaskazini mwa Tanzania na kutuandalia taarifa ifuatayo.

Bofya hapa kusikiliza sauti ya mama wa kichaga akieleza jinsi Mandela alivyofika na kukaa kwake.

Mizizi ya Mandela Tanzania - BBC Swahili - Medianuai
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom