Mzimu wa Jangwani

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,796
Tafsiri ya jangwa iko wazi... Ni mahali pasipomea... Sehemu kame kabisa... Jua kali pamoja na joto kali mchana... Usiku baridi kali na wakati mwingine upepo pia.. Jina la sehemu yenye jangwa huitwa Jangwani

Mfano wa majangwa ni Karahali na Sahara... Lakini je unafahamu kwamba majina huathiri na hulka na hata kuleta uhalisia?

Siandiki sasa kwakuwa timu ya Yanga inafanya vibaya kwenye medani ya soka... Pamoja na ukweli kwamba imekuwa na rekodi na matukio ya hovyo kwa ujumla wake kwa muda mrefu sana.... Kwa majumuisho ya jumla Yanga imeachwa mbali na Simba... Yanga inajulikana kama wazee wa Jangwani

Siandiki haya kwakuwa shule ya upili ya wasichana ya Jangwani imefanya vibaya sana kwenye mitihani kitaifa... Imekuwa shule ya 351 kati ya shule 353? Jangwani sekondari

Ni kipi kilishawahi kufanikiwa eneo hilo la Jangwani? Pale ni eneo oevu na tepetevu... N eneo la kidau na lina majimaji majira yote ya Mwaka... Ilikuwaje paitwe jangwani? Mbona jina haliakisi uhalisia? Kiroho kuna tafsiri pana sana

Pale sio jangwa la kimwili... Pale ni jangwa la kiroho.... Ni mapito na makazi ya wenyewe.... Ni mapito ya maji wakati wa mvua lakini pia pana muunganiko na bahari pale.. Ni kipumzikio cha watu pale.... PAACHWE kama palivyo

Hivi unaweza kuamini kuwa STRABAG walishindwaje kujenga barabara ya juu toka magomeni mpaka fire?

Hivi unawezaje kuamini kuwa kuna wakandarasi na elimu na akili zao walishauri kijengwe kituo cha UDART pale? Matokeo mmeyaona? Wanapakimbia

Mpaka leo hii serikali haiwezi kukwambia ukweli eneo lile la jangwa limekula mabilioni mangapi kila mwaka kujaribu kudhibiti mafuriko ya pale.

Ongea uliza watu walioishi pale maisha yao yalikuwaje baada ya kuhama... Wengi wanakiri walikuwa wamefungwa...

Zamani palikuwa na ahueni kwasababu ya makafara... Watu wameuliwa sana pale.... Jangwani ndio ilikuwa mabwepande ya WANA... jangwani palikuwa panatisha na kuogopeka.. Matambiko na kafara vilifanyika sana pale.... Si kila maiti iliyookotwa pale ilikuwa ni kutokana na risasi moja kisogoni

Matambiko na makafara yale vilisaidia kwa kiasi kikubwa kupoza mambo.... Siku hizi pana mataa ya kizungu usiku mzima.

Jangwani sekondari ina historia yake chafu sana... wazee wa mujini wanafahamika vema wallichoifanyia ile shule... Lakini kila jambo lina asili yake... Ya Yanga tusiyaongelee leo..... I inatosha tu kusema MZIMU WA JANGWANI UMEFUFUKA..,

Good morning Africa!
 
Mshana uko na shida rafiki yangu..! Tulio kwa Yesu hatusumbuliwi na fikra nyepesi kama hizi ziwe za kweli au za uongo siyo hoja, bali msingi wetu ni tumaini la UZIMA WA MILELE. Maandiko yanasema bado kitambo kidogo unayoyaona jangwani hutayaona, elimu haitakuwa na maana, yanga au simba, Manchester au Madrid haitakuwa story tena ila NENO/JESUS litasimama milele.
 
Aaamen kaka asante sana.... Mambo yote yatapita lakini NENO litasimama... Lakini kumbuka pia bado kitambo kidogo.... Na unabii lazima utimie kwanza
 
Avatar yako inakinzana na maneno yako, waswahili tunakuita ndumilakuwili au popo.
 
Aaamen kaka asante sana.... Mambo yote yatapita lakini NENO litasimama... Lakini kumbuka pia bado kitambo kidogo.... Na unabii lazima utimie kwanza
Shetani na mawakala wake huwa wanatutoa katika kuutafakari ukuu na utukufu wa Mungu na badala yake wanatuchepusha kujadili upupu/upuuzi km huu, kitakachofuata ni hofu kisha kuishia kutambikia na kutoa kafakara! Be strong spiritually hutajaribiwa au kutumika hovyo! Kwani wema Mungu huoni? Neema za Mungu huzioni? Mbona huzijadili unaishia kujadili habari za giza? Mungu alivyo mwema hutumia watu, malaika, Roho mtakatifu na wakati mwingine majaribu na mitego ya shetani kujipatia utukufu kwa kuwakomboa watu wake kama wewe rafiki yangu.
 
Avatar yako inakinzana na maneno yako, waswahili tunakuita ndumilakuwili au popo.
Kwanini kila unachokiona udhani rafikiii??? Hapo mwanzo Mungu alituumba akatuacha uchi huwezi tafisiri alitaka tufanye uzinzi..! What if mimi biologist tena zoologist..! your smart eyes only.
 
Back
Top Bottom