Sipendi Washabiki ambao hawajui nini kinaendelea huko Ofisini. Huyu Mzee anaangushwa na OWNER wa timu kwa sababu hawampi hela.
Ukisikia kufanya kazi kwenye mazingira magumu basi ndiyo huku. Siku akiondoka na Arsenal ishuke daraja ndiyo mtakuja kumkumbuka na kumpa heshima ila tayari itakuwa too late. Jifunzeni kupekuwa ukweli na si kulalama tu.
kinachoudhi kwa huyu mzee ni kuwa mnafiki!siku zote anadai pesa ya kusajiri ipo lakini hajaona mtu au haoni haja ya kufanya hivyo!hata pale mwanahisa ambae sio board member(usmanov)alipomtetea kuwa board inamwangusha kwa kutompa sapoti alikuja juu na kudai kila kitu kipo sawa.sasa ni kutetea kibarua au nini sijui.
Ni wazi majority shareholder(kraonke)yupo pale kuvuna kpato sio vikombe!!!
Kwani UONGO? Pesa ipo ila kiasi gani? Halafu unafikiri atakuja na kusema tatizo ni OWNER?
Kwani Mkuu una miaka mingapi hadi jambo la kitoto namna hii kutokulifahamu? Wenger angelikuwa chini ya Waarabu wenye PESA ndefu, angelikuwa na wachezaji wazuri sana. Sasa hivi wenzake wanasubiri na wakiona ananyemelea mchezaji fulani, basi wanaenda kumnunua maana wanajua Babu ana PUA KUBWA. Babu anabaki kusubiri MASALIA kama akina Podolski ambao hakuna anayemtaka.
kasomea uchumi huyo anauza mbuzi 70,000 halafu ananunua kamba ya 60,000 sijui hiyo kamba anamfungia nani wakati mbuzi ameshauza
Kwa hiyo tuendelee kuwa na pressure tu !
Mkuu, nivigumu kujua. Tatizo jamaa ni Mfanya biashara zaidi na si mpenzi wa Mpira. Boss wa Chelsea ndiyo mpenzi wa mpira yule ingawa pia ni mfanya biashara. Nasikia anataka kuuza Share zake, huyu Stan Kroenke basi labda akiuza, wanaweza kuja watu wenye mapenzi kweli na wakaweka hela bora na siyo Bora hela kwa kununua wachezaji.
Kwa hiyo tuendelee kuwa na pressure tu !
Arsene Wenger bonge la kocha. Sisi wana Arsenal damu, bado tunamuhitaji na tutapenda kuona akiongezewa mkataba wa muda mrefu baada ya muda wake kuisha hiyo 2014. Wana arsenal ni kama familia, tunavumiliana kwa shida na raha.. IN ARSENE WE TRUST