Mzee wa upako na mafuriko ya dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzee wa upako na mafuriko ya dar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by FEELINGS, Dec 30, 2011.

 1. F

  FEELINGS Member

  #1
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 30, 2011
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Niliangalia kipindi cha Mch. Anthony Lusekelo almaarufu Mzee wa Upako au "Transfoma" katika Channel Ten siku ya jumatano 28/12/2011. Niliogopa sana aliposema ananguvu kuliko wingu la mvua lilotanda ambalo watu wa mamlaka ya hali ya hewa waliliona kwa vyombo vyao. Mzee wa upako alisema hakutakuwa na mvua kubwa yenye kuleta madhara ktk jiji la Dar kwani ataomba na wingu litatoweka. KWELI! nasikia jana wingu la mvua lilitanda huko Dar kisha likatoweka. Hakukuwa na mvua kubwa wala ya madhara kama ilivyotabiriwa na watu wa TMA. Mzee wa upako ameshinda. Hofu yangu ni ile kauli yake kwamba kama mvua hiyo ingenyesha kama TMA walivyosema basi angeecha kazi ya uchungaji! kweli ingetokea angeacha? Maanake kuna Askofu wa Full Gospel mwaka fulani wa uchaguzi aliwahi kusema MUNGU keshamwonyesha rais ajaye akamtaja. Lakini aliaibika kwani aliyemtaja hakuambulia hata nafasi ya pili nafikiri. Watumishi wa Mungu tuepuke kujiapiza mbele ya waumini wetu, ni vyeme kusema mambo hayo makubwa hata kama ni Mungu wako amekuonyesha lakini musijiapize mtaumbuke mshindwe kutekeleza yale mliyojiapiziya. Itakuwa aibu kwenu na kwa waumini wenu. Kwani hamkumbuki yuele kiongozi wa dini fulani aliyekuwa anzuiya nguzo za umeme zisipite karibu na kanisa lake! Liwafanya waumini wake kuwa walinzi wa eneo hilo huku wakiwa na sare za T-shirt. Kiongozi wao alivyoshindwa hoja zake na serikali aliapa kuwa umeme huo hautawaka! sasa unawaka anajisikiaje? waumini wake waliomakini wanamuonaje sasa? hata wasiokuwa waumini wake lakini wanamfuatilia katika vipindi vyake walimdharau. Na sasa simuoni tena kwenye luninga.
   
 2. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,075
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  eh! kwa hiyo aliomba wingu litoweke na likatoweka...!?:lol::lol::lol: kazi kwelikweli..
   
 3. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Hii ilipostiwa tangia jana hukuwewe!!!!
   
Loading...