Fatma Bawazir
JF-Expert Member
- Dec 24, 2010
- 492
- 180
Mzee mmoja wa kipemba alikuwa amevaa shuka yake alisafiri na jahazi akielekea pemba walipofika katikati ya bahari mara upepo mkali ulianza kuvuma mzee akaweka mikono yake kichwani kuzuia kofia yake mara shuka ikapanda mabegani kwa upepo huku chini akawa kama alivyo zaliwa (uchi) jamaa mmoja akamwambia sasa mzee si uzuie hiyo shuka hukuchini, mzee akajibu hii kofia ni mpya nimenunua juzi tu lakini hizi mali za chini nna miaka sabini nnazo wala hazitachukuliwa na upepo