Mzee Sumaye azidi kuteseka. Je, atarudi CCM?

Mzee Sumaye azidi kuteseka. Je, atarudi CCM?

Sioni sababu ya kuwatesa wenzio.
Shamba la mama Anna mkapa pale vikawe ni mapori tu.mbona hajalichukua?
watanzania hatuna roho hyo.
Ni roho ya kinyarwanda.
kikwete ULITUKOSEA SANA 2015.
hya machozi na damu vitakulilia WEWE NA WENZIO.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unamlilia Fredrik leo?

Vuta kumbu kumbu hilo ni zao hilo hilo mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu haya yanayotokea ni bahati mbaya, lkn kama kuna mtu anadhani atsingia upinzani halafu asalimike naomba hilo adahau. Hii ni miongoni mwa nchi za Afrika. Wengi wa viongozi wake wanatafuta uongozi ili wawe wakoloni.weusi. TZ haikusalimika. Si dhani kwamba hilo litamrejesha Sumaye kule alikotoka.
 
Haijalishi.
Ila kutofautiana itikadi za vyama .sio sababu ya kuwatesa wenzio.
Ikitokea chadema tukachukua nchi Ipo siku chadema itaingia ikulu..
naamini hatutamtesa adui yetu..

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijaona kama ameteswa ni kurudisha kile alichowaibia watanzania alivyokuwa madarakani.

Kumbuka alikuwa waziri mkuu kwa miaka kumi kwenye utawala wa awamu ya tatu.

Kila la kheri CDM kama mtaingia ikulu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Instagram%20media%20-%20Bup8K11AIvx.jpeg
 
"Sisi tuliowazoefu wa siasa tumekuja huku ili kusaidia upinzani kujenga misingi ya kiuongozi, na hili naamini tunaisaidia CCM yenyewe, ili upinzani wakishinda Urais kusihangaike kutojua la kufanya" - Sumaye

Kama kweli malengo yalikuwa ni hayo, kuna cha kujiuliza atafanikiwa bila mwenziwe? Chadema wameng'atwa na nyoka, je? ataendelea kuaminiwa? na taasisi?
 
"Mmeamkaje? Kwangu mambo siyo mazuri. Mtakumbuka baada tu ya kuingia upinzani serikali ilitishia muda mrefu kuchukua mashamba yangu bila sababu za msingi, hata wakati wa kampeni baadhi ya viongoz wa ccm walitamka hadharani kuwa huyu dawa yake ni kumnyang'anya mashamba yake. Shamba la mabwepande ekari 33 wameagiza wiki hii halmashauri iligawe kwa wavamizi na wengineo.

Jana nimepokea barua kuwa shamba la mvomero ekari 326 limetwaliwa na rais na sitakiwa kukanyaga hapo. Shamba hilo lina majengo, mazao, mashine mbali mbali, visima virefu vya maji, umeme na mifugo mchanganyiko zaidi ya 200. Kisingizio shamba halijaendelezwa! Shamba lenye vitu vyote hivyo halijaendelezwa??

Mbaya zaidi katika kupinga dhamira hizo nilifungua kesi mahakama kuu kwa mashamba yote na mahakama zimeweka zuio la kutokuingiliwa mashamba hayo mpk mashauri ya msingi yatakapoamuliwa.

Lakini wameshaamua kwa hiyo mahakama hazina kazi. Utawala huu haufuati sheria ni udikteta mtupu! Kuna mwana ccm moja alisema "tutamfilisi mpk atakapotembelea ndala ndo atakumbuka kurudi ccm."

Hilo litawezekana kama Mungu huyu ni wa ccm. Ccm sirudi pamoja kuwa najua nitateseka na familia yangu! Kisasi hiki mimi sitakiweza namwachia Mungu ndiye atakayetufuta machozi mimi na familia yangu."

Fredrick Tluway Sumaye.
Waziri Mkuu Mstaafu
August 12, 2017

Note: Jana niligusia Kuhusu hujuma, dhuluma na madhila mbali mbali wanayopitia Viongozi na wanachama wa Upinzani. Nilieleza namna gani Viongozi wetu akiwamo Freeman Mbowe wanavyoteswa kwa namna mbali mbali kuanzia kwenye kuharibiwa au kunyang'anywa mali zao na hata kuwekwa gerezani.

Nilisema Unapoamua kuwa mpinzani Tanzania ni lazima kwanza ujikane nafsi yako kisha ujitwishe msalaba wako. Mbowe angekuwa ana roho ya ubinafsi ya kuangalia maslahi yake na familia yake leo angekuwa CCM.

Hebu leo TUJIKUMBUSHE kidogo na kutafakari DHULUMA ambazo amefanyiwa Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye tangu alipoondoka CCM na kujiunga na CHADEMA.

Jipeni moyo ulimwenguni mnayo dhiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
Dhuluma hulipwa kwa dhuluma kama ulinyanyasa watu bas nawe utanyanyasika waombe msamaha wale ulio wanyanyasa mwenyezmungu atafungua kila jambo je? Sumaye anakumbuka aliyoyafanya akiwa waziri mkuu? Je? Hzo mali kazipata kwa pesa halali na njia halali? Tusijitwishe unafki watanzania ukifanya dhuluma nawe utadhulumiwa
 
Itakuwa vema kwa mzee Sumaye kuamua kustaafu siasa hasa hizi siasa zetu zisizo na ustaarabu akiwa upinzani ili kulinda hadhi yake.

Si kwa sababu ya kuupenda zaidi upinzani bali kwa sababu kuu 2.
#1.Maisha siyo lazima uwe chama fulani. Ingawa kuna wanaofuata usalama wao,sifa,kumbo na maslahi.
#2.Masuala ya hamahama yanadharirishabutu wa mtu na kushindwa kumtathmini umahili wake na msimamo kisiasa.

Historia na heahima ni mambo muhimu ya kuenziwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu anasema atakua kiongozi wa malaika,atabaki kua kiongozi wa bashite

Sent using Jamii Forums mobile app

Ni kwel atakua kiongozi wa malaika maana hata freemason nao wana malaika wao nadhani atakua upande huo na sio kwa mungu tunaeamini kua kua upendo na furaha

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Waache watesane. Kipindi Sumaye alipokuwa kiongozi kuna watu walipata tabu sana. Hata kuwapora hayo mashamba. Mwache nae akinywee maana nae aliwatesa sana wananchi.
Lakini akirudi CCM mateso yatakoma kwake,wananchi wataendelea kuteseka vilevile chini ya mkono wa CCM.
 
Malipo ni hapa hapa duniani jiwe atajidai sana lakini atafikia mwisho wa aibu na mbaya sana hamtaamini .
 
"Mmeamkaje? Kwangu mambo siyo mazuri. Mtakumbuka baada tu ya kuingia upinzani serikali ilitishia muda mrefu kuchukua mashamba yangu bila sababu za msingi, hata wakati wa kampeni baadhi ya viongoz wa ccm walitamka hadharani kuwa huyu dawa yake ni kumnyang'anya mashamba yake. Shamba la mabwepande ekari 33 wameagiza wiki hii halmashauri iligawe kwa wavamizi na wengineo.

Jana nimepokea barua kuwa shamba la mvomero ekari 326 limetwaliwa na rais na sitakiwa kukanyaga hapo. Shamba hilo lina majengo, mazao, mashine mbali mbali, visima virefu vya maji, umeme na mifugo mchanganyiko zaidi ya 200. Kisingizio shamba halijaendelezwa! Shamba lenye vitu vyote hivyo halijaendelezwa??

Mbaya zaidi katika kupinga dhamira hizo nilifungua kesi mahakama kuu kwa mashamba yote na mahakama zimeweka zuio la kutokuingiliwa mashamba hayo mpk mashauri ya msingi yatakapoamuliwa.

Lakini wameshaamua kwa hiyo mahakama hazina kazi. Utawala huu haufuati sheria ni udikteta mtupu! Kuna mwana ccm moja alisema "tutamfilisi mpk atakapotembelea ndala ndo atakumbuka kurudi ccm."

Hilo litawezekana kama Mungu huyu ni wa ccm. Ccm sirudi pamoja kuwa najua nitateseka na familia yangu! Kisasi hiki mimi sitakiweza namwachia Mungu ndiye atakayetufuta machozi mimi na familia yangu."

Fredrick Tluway Sumaye.
Waziri Mkuu Mstaafu
August 12, 2017

Note: Jana niligusia Kuhusu hujuma, dhuluma na madhila mbali mbali wanayopitia Viongozi na wanachama wa Upinzani. Nilieleza namna gani Viongozi wetu akiwamo Freeman Mbowe wanavyoteswa kwa namna mbali mbali kuanzia kwenye kuharibiwa au kunyang'anywa mali zao na hata kuwekwa gerezani.

Nilisema Unapoamua kuwa mpinzani Tanzania ni lazima kwanza ujikane nafsi yako kisha ujitwishe msalaba wako. Mbowe angekuwa ana roho ya ubinafsi ya kuangalia maslahi yake na familia yake leo angekuwa CCM.

Hebu leo TUJIKUMBUSHE kidogo na kutafakari DHULUMA ambazo amefanyiwa Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye tangu alipoondoka CCM na kujiunga na CHADEMA.

Jipeni moyo ulimwenguni mnayo dhiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yanayoendelea ni miongoni mwa ubaguzi, kitu ambacho ni kibaya sana katika dunia ya sasa.
 
Back
Top Bottom