Uchaguzi 2020 Mzee Shomari: Uchaguzi wa mwaka huu ni kama wa mwaka 1995 ila mwaka huu mgombea wa CHADEMA ameingizwa chaka

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Wahenga wanasema usimdharau mtu usiyemjua. Sababu huwezi kujua huyo mtu anajua nini au ana maarifa gani kukuzidi wewe. Mzee Shomari japo ni muuza kahawa anajua mambo mengi. Ni mzee darasa la nne la mkoloni lakini ana uwezo wa kudadavua mambo.

Mwaka 1995 mgombea wa NCCR mageuzi Lyatonga Mrema aliichachafya Ccm kwenye awamu ya kwanza ya uchaguzi. Lakini Ccm ilipo jitafakari na kujirekebisha alijuwa wazi awamu ya pili hawezi tena kuwasumbua Ccm hivyo alikuwa mpole na Ccm ikachukua ushindi.

Ni wazi kabisa CCM mwaka 2015 Lowassa aliwachachafya CCM, lakini ukweli ni kuwa wamejirekebisha na sasa hakuna chama ambacho kinaweza kuwapa presha au jambajamba. Maana ni wazi kuwa CCM itashinda kwa 96% wabunge, madiwani na urais.

Mzee Shomari anasema ni wazi kuwa Tundu Lissu ameingizwa mkenge kuwania nafasi ambayo CHADEMA walijua fika kwa awamu hii hawawezi kuipata hata kwa udi na uvumba.

Lissu ameingizwa mkenge na Mbowe ndio maana hata badala ya kunadi sera na ilani ya chama chake amebaki kuleta siasa za kishamba za uropokaji majukwaani. Mfano mgombea urais unaweza eti utaruhusu wakulima wa korosho kuuza nchi yoyote wanayoitaka! Yaani mkulima wa korosho akauzie Msumbiji, na Tanzania unayoiongoza isipate mapato.

Ni aibu mgombea urais kuzua ufisadi ambao hauna ushahidi, kama kudai uwanja wa ndege Chato na ndege za ATCL zimenunuliwa kifisadi bila kuweka ushahidi. Sisi wapiga kura tulitarajia Lissu aweke nyaraka za ukweli juu ya ufisadi.

Ukweli ni kuwa Mbowe ulijuwa Lissu alitakiwa kugombea Ubunge au udiwani,ila umemuingiza chaka. Na mbaya zaidi umemuacha peke yake afanye kampeni,ndio maana anaropoka hovyo.
 
Maana ni wazi kuwa CCM itashinda kwa 96% wabunge, madiwani na urais.
.

Ushindi wa zaidi ya 90% unatamkwa sana na wana-ccm wakiongozwa na katibu wao. Inaelekea ushindi umeshapangwa kabisa, kinachosubiriwa ni kutangazwa tu. Kwamba iwe mvua liwe jua, lazima Magufuli atangazwe kwa zaidi ya 90%.

Lengo ni kutaka kuvunja kwa lazima record ya JK (2005).
 
Ingia field, kuna upinzani? Kama hata wabunge wa upinzani hawana pesa ya kampeni. Nini kinafuata?
 
Kitu ambacho watu wanashindwa kuelewa ni kuwa kwa sasa mambo mengi yanabadilika kutokana na elimu ya watu, teknolojia na hivyo kufanya mambo mengi yayanayodhaniwa kuwa yataenda kwa mazoea inakuwa ndivyo sivyo.

Chama tawala kilijua kimeua upinzani ila kinachotokea hivi sasa kinaonyesha tofauti kubwa. Nina uhakika fulani kuwa machafuko hayatatokea ila uchaguzi huu utabadili sura nzima ya mtazamo wa watanzania wengi
 
Kuna wakati mzee Slaa alikua anakuja na hoja za ufisadi na ushahidi Ukiwa kamili mezani. Zito alikua anakuja na hoja Za ufisadi wa serikali na uthibitisho Ukiwa mezani kabisa. Angalia ishu ya Escrow ya akina Kafulila Unakuta watu wanakuja na vielelezo wazi kabisa.

Richmond iliiangusha serikali kwasababu Watu walikua na ushahidi wa wazi na wananchi wanakubali na serikali inakabwa koo. Sasa wapinzani sasa hivi Wamepwaya sana kwenye hoja zaidi unasikia mazungumzo Kama yakwenye vijiwe vya Kahawa yanazungumzwa na mpaka wagombea urais.

Tuombe Tupate upinzani imara kabisa Kama nyakati zilizopita ili serikali ichangamke. Kukiwa na upinzani wenye hoja, vithibitisho tutarudi enzi za upinzani unaoichachafya serikali na wananchi tunapata burudani ya Siasa na maendeleo juu.
 
Wahenga wanasema usimdharau mtu usiyemjua. Sababu huwezi kujua huyo mtu anajua nini au ana maarifa gani kukuzidi wewe. Mzee Shomari japo ni muuza kahawa anajua mambo mengi. Ni mzee darasa la nne la mkoloni lakini ana uwezo wa kudadavua mambo.

Mwaka 1995 mgombea wa NCCR mageuzi Lyatonga Mrema aliichachafya Ccm kwenye awamu ya kwanza ya uchaguzi. Lakini Ccm ilipo jitafakari na kujirekebisha alijuwa wazi awamu ya pili hawezi tena kuwasumbua Ccm hivyo alikuwa mpole na Ccm ikachukua ushindi.

Ni wazi kabisa CCM mwaka 2015 Lowassa aliwachachafya CCM, lakini ukweli ni kuwa wamejirekebisha na sasa hakuna chama ambacho kinaweza kuwapa presha au jambajamba. Maana ni wazi kuwa CCM itashinda kwa 96% wabunge, madiwani na urais.

Mzee Shomari anasema ni wazi kuwa Tundu Lissu ameingizwa mkenge kuwania nafasi ambayo CHADEMA walijua fika kwa awamu hii hawawezi kuipata hata kwa udi na uvumba.

Lissu ameingizwa mkenge na Mbowe ndio maana hata badala ya kunadi sera na ilani ya chama chake amebaki kuleta siasa za kishamba za uropokaji majukwaani. Mfano mgombea urais unaweza eti utaruhusu wakulima wa korosho kuuza nchi yoyote wanayoitaka! Yaani mkulima wa korosho akauzie Msumbiji, na Tanzania unayoiongoza isipate mapato.

Ni aibu mgombea urais kuzua ufisadi ambao hauna ushahidi, kama kudai uwanja wa ndege Chato na ndege za ATCL zimenunuliwa kifisadi bila kuweka ushahidi. Sisi wapiga kura tulitarajia Lissu aweke nyaraka za ukweli juu ya ufisadi.

Ukweli ni kuwa Mbowe ulijuwa Lissu alitakiwa kugombea Ubunge au udiwani,ila umemuingiza chaka. Na mbaya zaidi umemuacha peke yake afanye kampeni,ndio maana anaropoka hovyo.
Mwaka hiyo na 2020 ni tofauti kabsa, mwaka 2020 watanzania wameamka vyema wanataka mabaliko hawataki ngojera za CCM, acha kuwafananisha watanzania wa kipindi hicho na sasa
 
Hii yote ni kwanini?
Vipaumbele vya watawala sio Vipaumbele vya wananchi.
Ndio maana sasa maccm wakiongozwa na Meko wanafoka jukwaani. Wananchi wanataka maji unanunua ndege, wao wanataka hospitali unajenga flaiova, wao wanataka shule unajenga SGR fupi.

Maccm badilikeni
 
Lissu anachangamsha uchaguzi, mwache aendelee kubwabwaja.
Hii yote ni kwanini?
Vipaumbele vya watawala sio Vipaumbele vya wananchi.
Ndio maana sasa maccm wakiongozwa na Meko wanafoka jukwaani. Wananchi wanataka maji unanunua ndege, wao wanataka hospitali unajenga flaiova, wao wanataka shule unajenga SGR fupi.

Vipaumbele vya watawala sio Vipaumbele vya wananchi.
Maccm badilikeni
 
Kama tulivyo kubaliana kwenye kikao sie tusio na vyama,mdahalo upo pale pale kwa ccm kuja wote ila tundulisu yeye peke yake.
 
Back
Top Bottom