Idugunde
JF-Expert Member
- May 21, 2020
- 6,273
- 6,637
Wahenga wanasema usimdharau mtu usiyemjua. Sababu huwezi kujua huyo mtu anajua nini au ana maarifa gani kukuzidi wewe. Mzee Shomari japo ni muuza kahawa anajua mambo mengi. Ni mzee darasa la nne la mkoloni lakini ana uwezo wa kudadavua mambo.
Mwaka 1995 mgombea wa NCCR mageuzi Lyatonga Mrema aliichachafya Ccm kwenye awamu ya kwanza ya uchaguzi. Lakini Ccm ilipo jitafakari na kujirekebisha alijuwa wazi awamu ya pili hawezi tena kuwasumbua Ccm hivyo alikuwa mpole na Ccm ikachukua ushindi.
Ni wazi kabisa CCM mwaka 2015 Lowassa aliwachachafya CCM, lakini ukweli ni kuwa wamejirekebisha na sasa hakuna chama ambacho kinaweza kuwapa presha au jambajamba. Maana ni wazi kuwa CCM itashinda kwa 96% wabunge, madiwani na urais.
Mzee Shomari anasema ni wazi kuwa Tundu Lissu ameingizwa mkenge kuwania nafasi ambayo CHADEMA walijua fika kwa awamu hii hawawezi kuipata hata kwa udi na uvumba.
Lissu ameingizwa mkenge na Mbowe ndio maana hata badala ya kunadi sera na ilani ya chama chake amebaki kuleta siasa za kishamba za uropokaji majukwaani. Mfano mgombea urais unaweza eti utaruhusu wakulima wa korosho kuuza nchi yoyote wanayoitaka! Yaani mkulima wa korosho akauzie Msumbiji, na Tanzania unayoiongoza isipate mapato.
Ni aibu mgombea urais kuzua ufisadi ambao hauna ushahidi, kama kudai uwanja wa ndege Chato na ndege za ATCL zimenunuliwa kifisadi bila kuweka ushahidi. Sisi wapiga kura tulitarajia Lissu aweke nyaraka za ukweli juu ya ufisadi.
Ukweli ni kuwa Mbowe ulijuwa Lissu alitakiwa kugombea Ubunge au udiwani,ila umemuingiza chaka. Na mbaya zaidi umemuacha peke yake afanye kampeni,ndio maana anaropoka hovyo.