Uchaguzi 2020 Mzee Shomari: Mgombea urais wa CHADEMA hana nia njema na Watanzania wa kipato cha chini, hastahili kupata kura hata moja

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
1,304
2,000
Mimi mzee Shomari nasikitika sana kuwa CHADEMA wanaweka mgombea urais ambae hana huruma kwa watu masikini na tusio na uwezo kama mimi. Mimi nauza kahawa,kuna mama mama ntilie, kuna wamachinga na wengi tu ambao kipato ni cha hali ya chini.

Serikali ya CCM imetujali kwa kudhibiti uuzwaji wa nafaka nje ya nchi ili watanzania masikini kama mimi mzee Shomari nisipate tabu ya kupata kununua nafaka kama mahindi na mchele kwa bei ya juu. Maana huko miaka ya nyuma nafaka zilikuwa zinasafirishwa na kuuzwa holela nchi za nje, kitendo ambacho kilfanya unga na mchele uwe na bei kubwa. Leo hii unga hapa nchini una bei ya wastani ya sh 1300, lakini kabla ya serikali ya Ccm kudhibiti uuzwaji holela wa mazao kwenda nje ya nchi ulifikia hadi bei ya sh 2000.

Sasa basi kama mgombea wa CHADEMA akiwa mkoani Rukwa anasema ataruhusu wakulima wauze nje mazao kama wanavyotaka,hajui kuwa kuna madhara kwa watumiaji wa ndani. Maana anajinadi ataruhusu wauze nchi yoyote wanayotaka bila kujali mahitaji ya ndani.

Je, Mgombea urais kama huyu anapaswa apewe kura hata moja? Kama anakuwa hajali watu wenye shida na kipato duni kama mzee Shomari! Maana kiogozi bora lazima ujali raia wako kwanza kuliko kujali manufaa ya kisiasa. Maana ukiruhusu wakulima kuuza nafaka wanavyopenda,je wanachi wako watatapa chakula kwa bei rahisi!
 

stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
22,015
2,000
Hiyo nchi itayoongozwa na Lisu ni ya kusadikika.

Maajabu matupu.

Yaani jamaa hakusanyi kodi lakini atatoa huduma za afya bure , elimu bure, tutajua kingereza kama wazungu, atapandisha mishahara kila mwaka na hatajenga hata sentimita moja iwe ya daraja au bara bara.
 

Wyatt Mathewson

JF-Expert Member
Dec 22, 2017
9,520
2,000
Tunarudi kule kule kwenye kuendekeza umasikini.

Dawa ya umasikini ni mali.

Na mali inapatikana kwa kufanya kazi kwa juhudi.

Umasikini hauondoki kwa serikali kutoa mkate na chai za bure mle bure.

Masikini anasaidiwa kwa kuachiwa huru atafute mali kadiri anavyoweza kwa nguvu zake bila kuingiliwa na yeyote...

Ndio Tundu Lissu anataka kuhakikisha hilo linatokea!
 

Uwazitu

JF-Expert Member
Aug 19, 2019
1,332
2,000
Hiyo nchi itayoongozwa na Lisu ni ya kusadikika.

Maajabu matupu.

Yaani jamaa hakusanyi kodi lakini atatoa huduma za afya bure , elimu bure, tutajua kingereza kama wazungu, atapandisha mishahara kila mwaka na hatajenga hata sentimita moja iwe ya daraja au bara bara.

Acha basi KUPOTOSHA WATANZANIA.

NI WAPI NA LINI ALISEMA HATAKUSANYA KODI?

ALISEMA "UTOZAJI KODI UTAFANYWA KUWA RAFIKI, NA SIYO KAMA ILIVYOSASA AMBAPO KODI HUTUMIKA PIA KUKOMOA WAFANYABIASHARA KWA NGO YA KISIASA AU CHUKI BINAFSI"

UKWELI UTAKUWEKA HURU.
 

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
1,304
2,000
Acha basi KUPOTOSHA WATANZANIA.

NI WAPI NA LINI ALISEMA HATAKUSANYA KODI?

ALISEMA "UTOZAJI KODI UTAFANYWA KUWA RAFIKI, NA SIYO KAMA ILIVYOSASA AMBAPO KODI HUTUMIKA PIA KUKOMOA WAFANYABIASHARA KWA NGO YA KISIASA AU CHUKI BINAFSI"

UKWELI UTAKUWEKA HURU.
Kwa hiyo sasa hivi kodi zinawakomoa watanzania? Unajua kanuni za kukusanya kodi zipo vipi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom