Mzee ruksa awalipua viongozi mafisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzee ruksa awalipua viongozi mafisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Josh Michael, Sep 26, 2009.

 1. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #1
  Sep 26, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  • ASEMA WALIOJIPENYEZA MADARAKANI, SASA WANAUMBUKA
  Daniel Mjema, Same

  RAIS mstaafu, Ali Hassan Mwinyi amelipua kombora jingine kwa viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi, akisema kuwa walijipenyeza kwa bahati mbaya kushika uongozi, lakini sasa wanahaha.

  Mwinyi anaongoza kamati ya watu watatu iliyoundwa na Halmashauri Kuu ya CCM (Nec) kuchunguza chanzo cha wanachama na viongozi wa chama hicho tawala kuchukiana kiasi cha kurushiana maneno makali wakati wa kikao hicho na kupendekeza hatua za kuchukuliwa.

  Maneno hayo makali yalitokana na baadhi ya wanachama kutaka kulinyamazisha kundi ambalo limekuwa likijinadi kuwa linaongoza vita dhidi ya ufisadi ambayo watuhumiwa wa ufisadi waliitafsiri kuwa inakichafua chama na serikali yake.

  Lakini jana Mwinyi alirusha maneno makali dhidi ya watuhumiwa hao wa ufisadi, akisema wameshikwa pabaya.

  Mwinyi, ambaye aliongoza serikali ya awamu ya pili iliyoruhusu mabadiliko makubwa ya kisiasa, kijamii na kiuchumi kiasi cha kupewa jina la Mzee Ruksa, alisema viongozi hao sasa wanafedheheka kutokana na kushikwa pabaya.

  Ingawa hakutaka kufafanua alikuwa na maana gani, Mzee Mwinyi, ambaye alikuwa akizungumza kwenye kijiji cha Ndungu wilayani Same ambako alialikwa kuzindua wodi ya wazazi, alisema watu hao sasa wako kwenye wakati mgumu.

  Mwinyi hakutaja majina ya viongozi ambao wameshikwa pabaya lakini katika siku za karibuni baadhi ya wanasiasa, wafanyabiashara na maofisa waandamizi wa Benki Kuu (BoT) wamefikishwa mahakamani kwa makosa mbalimbali ya ufisadi, ikiwa ni pamoja na kutumia madaraka vibaya na kuisababishia hasara serikali, wizi na njama za wizi wa fedha za umma.

  Kundi la watu hao limekuwa likisakamwa na wapiganaji hao wa vita ya ufisadi ambao wanataka viongozi wengi zaidi wafikishwe mbele ya sheria kujibu tuhuma zinazowakabili.

  Mwinyi alilazimika kutoa kauli hiyo baada ya mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango, ambaye ni mmoja wa vinara wa vita ya ufisadi, kububujikwa na machozi kuonyesha jinsi anavyokerwa na tatizo la ufisadi nchini huku akiapa kuendeleza vita hiyo.

  Mwinyi alisema Kilango amekuwa akikerwa na tatizo hilo kwa kuwa anaguswa sana na maendeleo ya wananchi.

  "Hakuna mwenye shaka na uzuri na usafi wa uongozi wa Kilango... kiongozi mzuri lazima awe na sifa 10 ikiwamo huruma na hiyo ndiyo iliyomfanya Mama Kilango alie leo kuelezea machungu aliyonayo," alisema.

  "Ndio maana unamuona Mama Kilango anabwata kule Bungeni kwa nguvu zake zote akiona kuna dalili za uhaini ambao utawapokonya watu wake maendeleo... anasema sikubali na nyote mnafahamu."

  Akizungumza katika sherehe hizo Mzee Mwinyi alimwelezea Kilango kama kiongozi wa kweli mwenye kipawa adimu cha kuongoza Watanzania katika misingi ya uadilifu.

  "Aliyekosa kipawa hicho hawi kiongozi mzuri... na kiongozi wa namna hiyo akijipenyeza kwa bahati mbaya ndio hao wanaofedheheka ni waliofanya ufisadi na sasa wameshikwa," alisema Mwinyi.

  Alisema ufisadi si wa wana-CCM, lakini hutokea mmoja au wawili kama vile chuya isivyoweza kukosekana katika mchele mwingi na hiyo huwa ni hila ya chuya na si ya mchele wenyewe.

  Kwa mujibu wa mzee Mwinyi, CCM na wanachama wake ni safi na kusisitiza kuwa uongozi ni fani na kipawa na kiongozi mwenye vitu hivyo viwili hajifichi kama ilivyo kwa Kilango.

  Huku akitumia maneno ya "asante sana", "hongera sana" na "heko mama Kilango" kuonyesha anavyounga mkono msimamo wa mbunge huyo, Rais Mwinyi alimwelezea mbunge huyo wa Same Mashariki kuwa ni mtu anayeguswa na maendeleo ya Watanzania.

  Kilango, ambaye alikuwa kimya kwa muda mrefu tangu Nec imalize kikao kilichoonekana kutaka kuwafumba midomo vinara wa vita ya ufisadi, alibubujikwa machozi alipokuwa akiwahutubia wananchi waliofurika katika sherehe za uzinduzi wa wodi hiyo.

  Akizungumza kwa hisia kali, Kilango alisema hakuna jambo linalomuuma kama kuona kiongozi aliyechaguliwa na wananchi ili awatetee, anawageuka na kuwa mla rushwa na kuwaumiza wananchi waliomchagua.

  Mbunge huyo aliapa kupambana na mafisadi na wala rushwa hadi kifo na akawataka wananchi wasidanganywe kuwa CCM inakumbatia rushwa.

  "Msidanganywe na watu kuwa CCM inakumbatia wala rushwa, hiyo si kweli hata kidogo… mimi ni mbunge wenu wa CCM na siku zote nitapambana na rushwa na siku zote sijawahi kwenda nje ya katiba ya CCM," alisema Kilango.

  Kilango, ambaye ni mke wa waziri mkuu wa zamani na mbunge wa jimbo la Mtera John Samuel Malecela, alisema kiapo cha CCM inatambua kuwa rushwa ni adui wa haki na ndio maana mwanachama ni lazima aape kuwa hatatoa wala kupokea rushwa wala kutumia cheo chake au cha mtu mwingine kwa maslahi binafsi.

  Mwinyi alitumia mkutano kuwapongeza wananchi wa Jimbo la Same Mashariki kwa kupata kiongozi mwenye sifa kamili za uongozi kama Mama Kilango na akazitekeleza kwa ukamilifu bila ubaguzi wa rangi, dini, kujuana au jinsia.

  Awali akitoa taarifa ya ukarabati wa wodi ya wazazi na watoto ambayo imekarabatiwa kwa kiwango cha juu, mganga mkuu wa wilaya ya Same, Dk Charles Kifunta alisema ukarabati huo umegharimu Sh75 milioni.

  Katika mradi huo ambao wananchi wa Ndungu walishirikishwa kwa asilimia 100, nguvu za wananchi ni sawa na Sh5 Milioni na fedha nyingine zilitolewa na Mama Kilango kupitia akaunti ya maendeleo.

  Sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi wa serikali, akiwemo mkuu wa mkoa Kilimanjaro, Monica Mbega, mkuu wa wilaya ya Mwanga na kaimu mkuu wa wilaya ya Same, Athman Mdoe.

  Ingawa kauli za Mwinyi hazikuwa wazi, wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema ziliashiria kumuunga mkono Kilango na wabunge wenzake katika mapambano dhidi ya ufisadi.

  Wabunge wengine ambao tayari wameapa kula sahani moja na mafisadi ni pamoja na mbunge wa Urambo Mashariki ambaye pia ni spika wa Bunge la Jamhuri, Samuel Sita na mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro.

  Wengine wanaotajwa katika orodha ya wabunge hao ni pamoja na Lucas Selelii wa Nzega, Dk. Harrison Mwakyembe wa Kyela.
   
 2. H

  Haki JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2009
  Joined: Jan 14, 2009
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu ndiye G. Washington wa TZ. Thank you Baba wa Taifa "Mzee Ruksa" kwa uhuru uliotupa. God Bless you.
   
 3. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Yah! Ila wadau nahisi ile michango iliyotolewa kule Same ni muhimu sana hasa katka kipindi hiki cha kulekea kwenye uchaguzi. (Hope nitakuwa nimeeleweka).
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Sep 26, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  G. Washington hakuwa rais wa pili wa Marekani. Au unajaribu kuandika historia upya?
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Sep 26, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Haki amejaribu kumfuta Nyerere katika historia ya Tanzania; kwake Tanzania imeanza baada ya Mwinyi.
   
 6. h

  hutwa Member

  #6
  Sep 26, 2009
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ubunge wa bongo mtamu, huyo mama mpaka kulia ili wampe kura aendelee kula, kazi kweli hapa. Kwa upande wangu naona ni maneno tu, hizo pesa zinazorudishwa BOT mbona wahusika hawatajwi? Siasa ya bongo mizengwe tu! nawasilisha.
   
 7. K

  Keil JF-Expert Member

  #7
  Sep 26, 2009
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mimi nitaamini kwamba CCM haikumbatii mafisadi iwapo itawatema viongozi wote wanaotuhumiwa na ufisadi na wengine ambao tuhuma zao ziko wazi mno. Kwenye hilo kundi ni pamoja na akina RA, EL, Vijisenti na akina Karamagi.

  CCM inatuhumiwa kukumbatia ufisadi kwa kuwa viongozi wengi wa juu ama wamekununuliwa na mafisadi ama wao wenyewe ni mafisadi na hivyo siku zote kazi yao ni kuwatetea mafisadi na ndio maana wananchi wanashangaa.

  Hivi Mama Kilango hajiulizi ni kwanini kwenye NEC ya juzi asilimia zaidi ya 75 ya wajumbe waliosimama kuchangia hoja walikuwa wanatetea mafisadi? Bado hapo utasema kwamba CCM haikumbatii mafisadi? NEC ni chombo cha juu cha kufanya maamuzi, na wajumbe wake wanasimama kutetea ufisadi kwa nguvu zao zote, bado tuamini kwaamba CCM haikumbatii mafisadi?
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Sep 26, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Je chupa yaweza kuwa na maji yenye sumu bila yenyewe kuwa na sumu?
   
 9. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #9
  Sep 26, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,661
  Likes Received: 1,503
  Trophy Points: 280
  Ukishatoa yale maji una fanya rinsing chupa inakuwa 'imesafishika'...si sumu haiwezi kupenya chupa?
   
 10. H

  Haki JF-Expert Member

  #10
  Sep 26, 2009
  Joined: Jan 14, 2009
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nazungumzia foundation aliyotuachia; kama Freedom, nk. Hakuna hata sera moja ya Nyerere inaoyofuatwa TZ. Hii system tunaoitumia (free market, democracy) TZ imeanzishwa na Mwinyi aka "Mzee Ruksa". Kwa hiyo, ukiangalia kiundani Mwinyi ndiyo G. Washington hata kama alikuwa rais wa pili.
   
 11. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #11
  Sep 26, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Ungesema hivyo na kuongezea kuwa alifungua milango kwa ufisadi.
  Baba wa taifa ni mmoja tu. Upende usipende. BTW unaweza kunitajia rais wa pili wa Marekani ni nani?
   
 12. J

  JokaKuu Platinum Member

  #12
  Sep 26, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,801
  Likes Received: 5,090
  Trophy Points: 280
  ..CCM imejaa mafisadi.

  ..huyu mama anapoteza credibility yake anapojaribu kuwazuga wananchi kwamba CCM haikumbatii mafisadi.
   
 13. K

  Keil JF-Expert Member

  #13
  Sep 26, 2009
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Inategemea ni sumu ya aina gani, kali kiasi gani na imekaa kwenye chupa kwa muda gani.

  Tatizo ninaloliona kwenye CCM ni kwamba over 80% ya viongozi wa juu (from NEC na kupanda juu) wana itikadi ya ufisadi (impliedly ni mafisadi ama wana mawazo yaliyotawaliwa na ufisadi na wakipata opportunity ya kufisadi hawafanyi makosa na ndio maana wanaogopa kutoa hukumu ya kuwatema mafisadi).

  Kwa hiyo hoja ya kuwatema mafisadi itakiua chama, na sidhani kama CCM wako tayari kuua chama. The only way ya CCM ku-survive ni wao kuendelea kubebana mpaka pale watanzania watakaposema kwamba chupa ile yenye sumu haifai kwa matumizi ya aina yoyote, maana hata kama ukiisafisha sumu yake imebaki kwenye plastic ama bati la container na haitoki. Kwa hiyo chochote kitakachowekwa kwenye hiyo container kitakuwa contaminated na kuleta madhara. Ili kukwepa madhara ya sumu inabidi kuitupa chupa. Hilo la kuitupa ni sawa na kuitoa CCM madarakani.

  Je, watanzania wote wana macho kama ya kwetu kwamba tunaona ile chupa ina sumu na haifai kwa matumizi ya aina yoyote?

  Hapa ndipo CCM na serikali wanapolia na waraka wa Kanisa Katoliki kwa kuwa una lengo la kuwafungua macho watanzania wengi mpaka vijijini ambako vyama vya upinzani haviendi. Waraka huu ukihubiriwa kwa mwaka mzima nina hakika wananchi wataelewa kwamba ufisadi ni adui namba moja na umeendelea kuwaongezea umasikini ilhali wengine wachache wanazidi kuneemeka na kuwa matajiri zaidi na zaidi at the expense ya wananchi ambao ndio wapiga kura.

  Bado tunahitaji huduma ya wanaharakati ili waweze kuwasaidia wanasiasa wa upinzani kufikisha hoja kwa wananchi ili wafunguke macho na waweze kuelewa kwanini wanazidi kuzama kwenye lindi la umasikini, kwanini barabara hazifiki kwao, kwanini hawapati maji, kwanini hawapati huduma za jamii zilizo nzuri? Kwanini usafiri wa reli siyo wa kuaminika tena? Kwanini wananchi waliopitiwa na mtandao wa umeme hawapati umeme wa kuaminika na mengineyo. Ukiingia kwa undani sana kiini cha hayo yote ni ufisadi unaofanywa na wachache ambao serikali inagwaya kuwachukulia hatua na inaishia kuhangaika na waganga njaa.
   
 14. K

  Keil JF-Expert Member

  #14
  Sep 26, 2009
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ninakubaliana na wewe hapo kwamba CCM imejaa mafisadi na ndiyo maana vita inakuwa ngumu.

  Sina hakika kama amepoteza credibility jimboni kwake, ila anaweza kuwa kwenye maandalizi ya kampeni za mwakani ili arudi mjengoni. Pia kwa njia moja ama nyingine anaisaidia CCM ili iendelee kuonekana iko safi na ilhali haiko safi. Nilishasema hao "wapambanaji" hawawezi kutemwa hata iweje. Ndiyo maana akina Chiligati siku hizi wanajibu hoja za akina Mwakyembe kwa nidhamu na ustaarabu na siyo kwa kutumia kauli za kejeli na jeuri.

  Malecela alishawaambia kwamba CCM itakuwa na hali ngumu come 2010 na kitakachofanya wawe na hali mbaya ni ufisadi. Alikuwa anajua alichokuwa anakisema kwa kuwa ameshiriki kwenye chaguzi ndogo ameshuhudia kwa macho yake ikiwa ni pamoja na kuzomewa na hata kama walishinda kwa haki aliona jasho lilivyowatoka. Tangu lini uliona Mama Kilango anakwenda kwenye kampeni, alienda Busanda baada ya kuona hali inakuwa ngumu.

  The bottom ni kwamba wanatakiwa kukisafisha chama, je wako tayari?
   
 15. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #15
  Sep 26, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hana lolote huyu mzee ni mtu wa maslahi tu na ni mjanja wa kupindukia anatafuna kama panya huku anakupuliza, kwani unafikiria ni kipi kilicho mpelekea Rais Kambarage Nyerere kumwambia kuwa ikulu haiogozi na mama siti yaani mke wa Ali hassan mwinyi?
   
 16. H

  Hekima Ufunuo JF-Expert Member

  #16
  Sep 26, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 220
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  NIliwahi kupost hapa kuwa wanaojiita wapambanaji wajiandae. kwanini nilisema hivyo? leo mmoja wa wajumbe wa kamati ya NEC ambaye anatakiwa kuunganisha wapambanaji na mafisadi anakuja na kauli inayoonyesha wazi kuungana na wapambanaji. Je hii kauli in udhati ndani yake?

  Nilisema wajiandae kwa sababu niliona mgeuko mkubwa wa viongozi wa juu wa CCM, katibu mkuu, katibu mwenezi, Mwenyeki wa CCM na sasa mwenyekiti wa kamati ya upatanisho. Kwa hekima na busara ya kwaida hii si dalili nzuri kwa wapambanaji, hii ni mbinu ya kuwashaulisha wajibu wao.

  Sasa come 2010 hili litatokea.
  Chama kitawapitisha wapambanaji wote kugombea, lakini majimbo yao yatakuwa sadaka kwa upinzani kwa kutumia mbinu ileile ya ushindi wa kishindo wa 2005. na baada ya hapo wataonekana kuwa wananchi wamewakataa kumbe majimbo yametolewa sadaka.

  Nawashauri viongozi wa upinzani kuwasimamisha watu makini katika majimbo hayo ya wambanaji kwani baada ya uchaguzi ushindi utakuwa wao kwa ridhaa ya Kamati Kuu na NEC ya CCM.


  Kataa CCM Okoa kizazi chako
   
 17. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #17
  Sep 27, 2009
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Naona huyu mzee kile kibao hakijamtosha......lol
  Natamani sasa hivi apatemtu wa kumpiga ngumi.
   
 18. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #18
  Sep 27, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kilicho mliza Kilango sio Ufisadi, Kilango anajua Sangara wanamwagwa Moshi na Sangara watagawanywa Same wiki ijayo anajua utamu wa Sangara wa Chadema kwa wananchi ulivyo.

  Kilango alichuana vikali sana na Mziray ambaye alikuwa na vitendea kazi duni, Je atamweza Sangara na Chopa juu ya hiyo milima ya Pare. Kilango anakaa Dar es salaam na kwenda Same kusalimia tu na kutoa machozi.

  Badala ya kulia aeleze ametimiza vipi ahadi zake, ili wananchi wajue mtaji wao. Uchungu wa mumewe kupigwa chini unamtoa machozi kila siku.
   
  Last edited: Sep 27, 2009
 19. A

  Atanaye Senior Member

  #19
  Sep 27, 2009
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 153
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  ..Huyu Mh Kilango atabadilisha sehemu kubwa tu ya uchaguzi mkuu hapo baadae kama sio hivi karibuni I think ataweza kuvunja ceiling nyingine kwa mamilioni 2015

  ..pamoja na kuwa na ruksa nyingi(moja ya chochezi cha ufisadi nchini) there was intergrity amongst waheshimiwa hii sasa hivi ni adimu.

  ..amewalipua?:D
   
 20. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #20
  Sep 27, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ameanza kusoma alama za nyakati, labda anasubiri Ripoti yao na Kinana ili watoe na kuona kama kuna jipya, Lakini hakusikika siku za nyuma sijui ni kwanini? Labda baada ya kusoma upepo akabadili mawazo yake na kambi yake, Sasa Mafisadi ni wakinani?? Mbona wako nao huko kwenye chama chao
   
Loading...