8691jakigili
Senior Member
- Mar 30, 2012
- 178
- 67
Mzee mmoja anayefanyia idara ya maji katika moja ya miji yetu, akawa anatamba mbele ya wafanyakazi wenzake juu ya mafanikio ya watoto wake kielimu na kimaisha. Akaanza: Mtoto wa kwanza yuko London anafanya kazi huko, wa pili yuko Washington Dc anachukua shadaha ya uzamivu, wa tatu yuko India anakamilisha kazi yake ya kuandika tasnifu. Mzee mwenzake mmoja akang'aka na kusema, "Una shida gani mzee mwenzangu hata kuwafanya watoto wako wote wakukimbie na kukaa mbali sana hivi na nyumbani kwako?"