Mzee Mwinyi asamehewe kwani ameteleza

Mkumbwa Jr

JF-Expert Member
Mar 23, 2016
2,370
3,148
Eid Mubarak kwa wanajukwaa wote
Hakuna mtanzania anayejielewa ambae hamjui mzee wetu Alhasan Mwinyi ambaye anayoheshima kubwa ndani na nje ya nchi yetu hii pendwa

Nimepatwa na mfadhaiko mara baada ya kuona kwenye vyanzo mbalimbali vya habari vikiripoti kwamba mzee wetu angetamani Raisi John Magufuli atawale milelele ila katiba inamkataza.

Ukisema mtu atawale milele nikwamba hata akiwa hayupo kivuli chake kitakuwepo(utawala wa kifalme kwa mtazamo wangu)

Mzee wetu anaendelea kutia tiki ule utafiti wa TWAWEZA uliowasilishwa sikuchache zilizopita maana wazee,wanawake na wale wasiokua na kiwango kikubwa cha elimu wanaunga mkono utawala uliopo

Angesema mwingine ambae hajui ladha,majukumu ya uraisi nisingepata ukakasi sana.Hata kuna wananchi kibao wametoa maoni kama hayo lakini sijayapa uzito wowote kwani ninajua wanaongeaongeatu bali mzee wetu hatutarajii afike huko.

Mzee wetu ninakushauri ufiche hisia zako kwani zina madhara makubwa kwa taifa letu.Lipo kundikubwa la watu linakuheshimu,kukutegemea na kukuamini

Kauli yako sio mbaya sana kama ingesemwa hata na Kinana kuliko we we

Nakuombea msamaha babu najua umeteleza

E i d M u b a a r a k
 
Amesema anatamani!kuna kizuri kakiona kwa mtawala wa sasa! Ni wishful thinking hakuna shida hapo !
 
Ile kauli yake juu ya soka letu kama nchi inatutafuna mpk kesho!
 
Mzee Ruksa namheshimu saana ,Mzee Ruksa ana upendo wa dhati kwa familia,majirani na WATANZANIA kwa ujumla.
Ila kwa hili mhhhhhhh mhh Mzee uliongoza. Inatosha.
 
Mimi huwa nashangazwa na watu wasio pendezwa na maoni ya wengine kana kwamba tuna fikra zinazofanana....!!!

Kwa hiyo mzee Mwinyi hana tena uhuru wa kutoa maoni au uhuru upo kwenye kutoa maoni yanayowapendeza nyinyi.....!!??

Kama ambavyo wewe unapenda maoni yako yaheshimike ingawa wakati mwingine hayapendezi basi na wewe jitahidi kuyaheshimu maoni ya wengine hata kama hayapendezi masikioni mwako...na huo ndio ukomavu........

Uhuru upi wa kutoa maoni unaopiganiwa hapa nchini hali ya kuwa hao wanaopigania huo uhuru hawaheshimu ya wengine.......!??
 
Mzee Ni Wa Kupuuzwa Tu Ikumbukwe Kauli Hizi Zinaivunja Katiba Ya Nchi Taratibu!
Yaani Wataozaliwa Na Uwezo Zaidi Hajawaza Hilo
 
Eid Mubarak kwa wanajukwaa wote
Hakuna mtanzania anayejielewa ambae hamjui mzee wetu Alhasan Mwinyi ambaye anayoheshima kubwa ndani na nje ya nchi yetu hii pendwa

Nimepatwa na mfadhaiko mara baada ya kuona kwenye vyanzo mbalimbali vya habari vikiripoti kwamba mzee wetu angetamani Raisi John Magufuli atawale milelele ila katiba inamkataza.

Ukisema mtu atawale milele nikwamba hata akiwa hayupo kivuli chake kitakuwepo(utawala wa kifalme kwa mtazamo wangu)

Mzee wetu anaendelea kutia tiki ule utafiti wa TWAWEZA uliowasilishwa sikuchache zilizopita maana wazee,wanawake na wale wasiokua na kiwango kikubwa cha elimu wanaunga mkono utawala uliopo

Angesema mwingine ambae hajui ladha,majukumu ya uraisi nisingepata ukakasi sana.Hata kuna wananchi kibao wametoa maoni kama hayo lakini sijayapa uzito wowote kwani ninajua wanaongeaongeatu bali mzee wetu hatutarajii afike huko.

Mzee wetu ninakushauri ufiche hisia zako kwani zina madhara makubwa kwa taifa letu.Lipo kundikubwa la watu linakuheshimu,kukutegemea na kukuamini

Kauli yako sio mbaya sana kama ingesemwa hata na Kinana kuliko we we

Nakuombea msamaha babu najua umeteleza

E i d M u b a a r a k
Nimaoni yako uko huru kutoa maoni na mh alhj Mwinyi naye yuko huru kutoa maoni usituletee uchochezi bwana kasema namnukuu (kama katiba ingekuwa inaruhusu)
 
Mimi huwa nashangazwa na watu wasio pendezwa na maoni ya wengine kana kwamba tuna fikra zinazofanana....!!!

Kwa hiyo mzee Mwinyi hana tena uhuru wa kutoa maoni au uhuru upo kwenye kutoa maoni yanayowapendeza nyinyi.....!!??

Kama ambavyo wewe unapenda maoni yako yaheshimike ingawa wakati mwingine hayapendezi basi na wewe jitahidi kuyaheshimu maoni ya wengine hata kama hayapendezi masikioni mwako...na huo ndio ukomavu........

Uhuru upi wa kutoa maoni unaopiganiwa hapa nchini hali ya kuwa hao wanaopigania huo uhuru hawaheshimu ya wengine.......!??
Unashangaa nini uhuru gani unaousemea? Kukosoa na kukosolewa, kupongeza na kupongezwa... Mtoa mada amekosoa wewe pia hukupenda mawazo yake umemkosoa ndio uhuru huo unaousema ndugu.... Au unasema usichokielewa? Tatizo mnataka kumsifu 'yeye' siku zote hata kama anapotoka.
 
Kateleza?hapana bro kwenye siasa hamna ajali.hili jambo halijaanza leo,walianza wakina butiku,wakafatia wale wa geita na mabango juu leo mzee mwinyi na natarajia kauli ikizidi kutajwa na kurudiwa kuipa uhalali na kuwaanda kisaikolojia.
 
Mzee wetu ninakushauri ufiche hisia zako kwani zina madhara makubwa kwa taifa letu.Lipo kundikubwa la watu linakuheshimu,kukutegemea na kukuamini

Kauli yako sio mbaya sana kama ingesemwa hata na Kinana kuliko we we

Nakuombea msamaha babu najua umeteleza

E i d M u b a a r a k

Jamani kibaya kipi amekisema Rais Mstaafu? Ameelezea hisia zake lakini pia ametambua hayo ni mapenzi yake ambayo hayawezi kuivuka Katiba ya nchi. Zamani Wananchi walimsalimia Mfalme kwa salamu ya "Mfalme uishi Maisha marefu". Maisha marefu kwa maana atawale maisha yake yote. Milele iliyotumika hapo ni kwa maana ya muda mrefu wa maisha yake. Lakini amesema Mheshimiwa kuwa hilo kamwe halitawezekana kwa sababu ya utaratibu wa kikatiba uliopo ambao ni mzuri tu na hata yeye anaukubali.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom