Hukumwelewa
Mzee Mwinyi
Wengi hamukumwelewa mzee Mwinyi kwa ile kauli yake juu ya Raisi kutawala milele.
Yule mzee alitumia fasihi ndogo tu.
Kwanza alimsifu Raisi kama kawaida ya tabia yake ya kupongeza pale anapoona inafaa.
Pili ile kauli ilikuwa na maana kuwa.
Pamoja na uongozi mzuri wa Raisi anao uonyesha, kama kutapatikana mrithi baada yake ni vizuri akaendeleza hayo mazuri aliyoyaanzisha Raisi, (yaendelee milele hayo mazuri)
kama yale maamuzi ya kijasiri anayoyafanya.
Kuhusu vipindi vya uongozi Mwinyi aliweka wazi kuwa Raisi hata kama angependa aendelee, au wale wanaopenda aendele, jambo hilo halitawezekana kwani katiba haisemi hivyo.
Kufanya hivyo ni kukiuka katiba hivyo pamoja kuwa mtu atapenda kuendelea kuongoza haita wezekana.
Hebu angalia hii kauli.
"Kama katiba yetu isingetanabaisha ukomo wa uongozi basi ningependa mheshimiwa Rais atawale milele"
Umeona fasihi ilivyotumika hapo.
Kwamba pamoja na mazuri anayoyafanya, katiba ni lazima iheshimiwe.
Kwaherini.