Mzee Mwanakijiji, Tafadhali...


Huyo Kibaraka wenu Zitto Kabwe kwanini msimchukue kuhamia CCM!?
 
Hao ndo watanzania, Kama Dr.Slaa hafai kuwa kiongozi ni vigezo gani wanatumia kuonyesha kuwa Lowasa anafaa kuwa Rais wetu, ndo maana huwa napenda kulieleza hili kwamba watanzania sijui tumerogwa na nani, basi hakuna haja ya kuwepo upinzani kwa sababu hawana viongozi ambao wana uwezo, kama hadi tuvizie kutoka ccm, nadhani tuendelee kuwa na imani na ccm, kwanza ni taasisi kubwa sana.
 

Wandugu sasa safari imeiva, ndio tunaelekea mtoni tukilikaribia kabisa lile daraja, siku zimekwisha!, jee tutavuka salama? au tutaishia kuzama?, sometimes inawezekana kenge ndio wako very right kuwepo kuwepo tuu kwenye msafara wa mamba, lakini kabla ya kufika mwisho wa safari huingia mitini kwa sababu wameiona hataei ya mbele?!.

Kwa sababu hata viumbe wanatofautiana uwezo wa uelewa wa dalili za hatari zijazo, ndio maana, hata maeneo ya volcano, kabla haijalipuka, wanyama wa mwituni, hukimbia mbali na eneo la hatari, lakini masikini binadamu, ng'ombe, mbuzi, kondoo na wanyama wafungwao, hubakia na kuishia kuteketea!.

Hivyo inawezekana kabisa hata uwepo wa hawa kenge kwenye msafara wa mamba, lengo lake ni kuwaalert mamba kuwa mbele kuna hatari?!, na ndio maana hawa kenge husepa zao kabla ya hatari?!.

Jumapili njema.

Pasco
 
Well said brother! mimi binafsi nimesha acha kusoma uzi wowote wa mzee mwanakijiji kwa sababu najua nilazima atamponda Lowassa.
No turning back ccm ni lazima iondoke..
 

Mmeuzana wenyewe, unachezea mangi. Anakula huku na huku.
 

unfortunately ulidhani kuwa MMM ni leader, we he has never been a leader, leaders dont run/step, they stay!!

He is a critic, and he is doing his job well... trying to perfect the imperfect, and try to straighten the impossibles

Zitto, Kitila, Mzee Mwanakijiji na wengi walio camp ya upinzani are not leaders, most of them ni protesters, they fall very far behind mtu kama Bakari Mwapachu.... because kuwa leader kunahitaji busara which is above principles, ukweli na norms....

Anyways, it is too late now, we are in a circus and the more you look at it, the more you believe that we may have lost a golden opportunity

Listening to magufuli is something very entertaining, ni kama tumekubali clueless arudi ili akina January wawe the thinktanks

Sijui kama huyu "commando kipensi" analijua hilo
 

Mkuu utaasisi wa ccm sioni, nje ya dola ccm ina tofautiana na vyama vingine kwa jina tu.
 
we kubwajinga , hivi unasema lowasa ndo papa wa mafisadi ktk nchi hii, toa takwimu za ufisadi wake nje na sakata la Richmond lenye mlolongo mlefu ndani ya ccm.
 
Mmeuzana wenyewe, unachezea mangi. Anakula huku na huku.
Usemayo ni kweli
, baadhi yetu wenye jicho la tatu, hili waliliona siku nyingi na waliisha wahi kulizungumza humu ili hakuna aliyewasikiliza!. Soma tarehe ya uzi huu, [h=3]Kilichomkuta Zitto: Kuna mkono wa Mtu! [/h]nenda kasome nilisema nini

 
...exactly brah...me do concur with you....wengi wanashindwa kuona huu uchaguzi ni opportunity kubwa kwa upinzani kuchukua dola...napata simanzi sana kuwaona na kuwasikia wanaojiita wapinzani (the likes of zitto, kitila, MMJ, slaa et al) wakiwazodoa na kuwadhihaki wenzao wa ukawa usiku na mchana....wameshindwa hata ku initiate kuungana na wenzao ukawa ili kuongeza nguvu ya upinzani....eti kisa lowassa kajiunga ukawa....sasa nashindwa kuelewa hivi wanafikiri ccm itaondoka hivi hivi madarakani???....wanashindwa kuona nguvu ya ujio wa lowassa na sumaye ukawa...na wanaonekana ni watu wasioelewa maana ya reconciliation kwenye siasa....kwa kweli kwa mtindo huu kama mwaka huu upinzani watashindwa basi sioni upinzani wa nguvu huko tuendako....watanzania ni wabinafsi sana hakika...hawa wanajifanya wazalendo lakini hakuna kitu...ni ubinafsi tu...
 

wewe mnazi wa lowassa usingeweza andika tofauti na ulivyoandika sasa....kama unaamini dr slaa hakuwa mpinzani basi tuache na sisi tuamini lowassa alichofuata cdm sio kuitoa ccm madarakani ila ni yeye kuwa rais full stop....

lowassa sio mpinzani na kamwe hawezi kuja kuwa mpinzani hata siku moja, hata ungeandika kwa wino wa asali kumpamba lowassa...kubali kutokubaliana
 
I hear you Rev.

Twende kazini sasa mavuno ni Mengi. tutashinda, tutarekebisha..

Lakini kwanza tutashinda!!

Comrade,

Umejiona ulivyo kilaza, just imagine wring all those words!!! halafu hamna content yoyote ya maana

nilifikiri utaweza kumjibu Rev, hujaweza

kwa kifupi futa thread yako Rev ameifuta kimantiki

haikuwa na sababu katika dunia ya wanaosema wanataka mabadiliko ....ila lazima wawe na muono au mawazo sawa! it cant be
 

Mpinzani ni nani? Tuanzie hapo.
 

Kwa Mara ya kwanza naungana nawe gamba ubarikiwe
 

Jambo pekee la kujifariji ni kuwa hawa wabinafsi (Slaa, Zitto etc) uhai wao wa kisiasa pia unakwisha baada ya uchaguzi, come what may!
 
Waliokutuma kawaambie umekuta tumetoka kidogo ila umekuta ujumbe mlangoni umeandikwa 'wenye mji wametoka ila ujio wako tunaujua jiondokee tu'.
 
Kuna watu walijiandaa kuwa wapinzani mpaka kufa ndio maana wakikaribia kushika nchi wanateleza maksudi ili wasishike msitari wa ushindi!! Huwezi kumweleza mtu aliyekuwa vitani muda mrefu aache kutumia silaha nzuri ili amuangamize adui kisa ile silaha imetengezwa kwenye taifa la adui!
Ukiona ugomvi umekolea na adui anakaribia kuingia mtaroni kisha mpambe wako anamudokeza adui arudi pembeni kwan anaingia mtaroni! Ujue uyo sio mpambe ni MPA.mbwa!!

Ukimuita fundi akuzibie paa ila akawa anatoboa bati badala ya kuziba eti ili upate hewa, hata kama fundi katoka Russia! Mshushe juu ya paa pandishe mwenyewe!!

Kwa sasa hata mbowe na lowasa wakijitoa, UKAWA haifii apo!! Tutawashusha tusonge mbele! Hii ni vita kati ya maskini na tajiri! Na kwa ivi tunaona tajiri kavimbiwa , hatutasubiri ushauri, lazma tumsukume mtaroni ndio turudi kusikiliza ushauri wa MPA.mbwa! Haturudi nyuma kamwe!!
 
Kwa Mara ya kwanza naungana nawe gamba ubarikiwe

Tatizo la CHADEMA ni jinsi Mbowe alivyomkumbatia Lowassa bila kuangalia jinsi ya kuzima mabaya yake kwenye njia isiyokiumiza CHADEMA. Alitakiwa ampe masharti ya kujisafisha madhambi yake ili ashabihiane na kauli mbiu ya CHADEMA dhidi ya ufisadi.

Badala yake Mbowe akamkumbatia Lowassa pamoja na dhambi zake na yeyote aliyekwazwa na hilo, k.m. Dr. Slaa, akafanywa kuwa ndiye mchawi.

Kwa hiyo ingawa, ingawa Lowassa alikuwa ni muhimu na ameweza kuwaongezea mvuto CHADEMA, lakini pia ameweza kukipaka CHADEMA matope ya UFISADI ambayo itakuwa vigumu sana kwao kuyaondoa.

Hivi sasa chama pekee kinachoweza kupigia kelele ufisadi ni ACT ingawa CCM nao wamepata uhai wa kuliongelea hilo kwa sababu ya Lowassa, aliyejulikana kuwa FISADI #1, amejiunga na CHADEMA na kuzima moto wao dhidi ya ufisadi.

LOWASSA ni kama KINYESI; kinaweza kuwa MBOLEA nzuri shambani, lakini pia kinaweza kukuletea KIPINDUPINDU.
 

Ni hoja yenye mashiko kwa kiasi fulani. Ni kweli CCM wamepata pa kujishikizia si kwa sababu nyingine ile bali ni kwa sababu waliishajitengeneza uwanja wa kuchezea - kuwafanya watanzania kuwa na welewa wa chini (nikitumia neno 'wajinga' mtasema nami ni mfuasi wa mzee wa 'ukweli na uwazi') kwa sababu wakiambiwa kuwa ufisadi wote mliokuwa mkisikia ukipigiwa kelele na CDM ni LOWASSA, wanaamini. Mbowe na waliomuunga mkono, wanastahili pongezi kwa sababu walifanya maamuzi magumu yanayopaswa kufanywa na jemadari ambaye yuko katikati ya uwanja wa vita na kikosi chake kimezingirwa na maadui. Yaani, wakati mwingine unaachana na systemic principles na badala yake unaenda na pragmatic actions ili uokoe angaa nusu ya kikosi! Dr Slaa (na wenzake aina ya MM) ni jemadari ambaye ana-surrender kwa kusikilia systemic principles za mapigano. Ni mwoga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…