Ex Spy
JF-Expert Member
- Jan 15, 2007
- 313
- 2,649
Alhaj Mustafa Songambele(aliyelala) akiwa na Waziri Simbachawene
Mwanasiasa mkongwe na miongoni mwa wapigania uhuru wa Tanganyika, Alhaj Mustafa Mohamed Songambele, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam.
Taarifa ya kifo chake imethibitishwa na binti yake Dorah Songambele, ambaye amesema maandalizi ya kuusafirisha mwili wa marehemu kwenda Songea kwa maziko yanaendelea, huku msiba ukiwa nyumbani kwake Mwananyamala.
Pia soma> Mzee Songambele: Nilinusurika kufungwa kwa kumchekesha Mwalimu Nyerere
Marehemu Songambele alitimiza umri wa miaka 100 Jumapili iliyopita tarehe 25 Mei 2025, na kusherehekewa na familia na marafiki wa karibu.
Alhaj Songambele alikuwa mmoja wa waanzilishi 30 wa TANU, na baadaye CCM, akiwa na kadi namba 27.
Aliweka rekodi ya kuwa Mkuu wa Wilaya ya kwanza nchini - alipoteuliwa kuongoza Wilaya ya Pwani (sasa llala) - kabla ya kupandishwa na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mzee Songambele pia anatajwa kuwa miongoni mwa wana Dar es salaam waliompokea Mwalimu Nyerere alipoacha kazi ya ualimu na kuongoza harakati za uhuru, na ndiye aliyemsaidia kupata kiwanja cha kujenga nyumba yake eneo la Magomeni Mikumi, nyumba ambayo sasa Makumbusho ya Baba wa Taifa.