Mbase1970, Ukweli ni kua Magu anashindwa afanye nn juu ya watangulizi wake wawili. Kwanza katiba ina walinda na pili wao ndo wamemkuza kwenye siasa na kumpa nafasi hiyo. Amini kama Magu angelikulia upinzani akaja kua Rais katiba ingelibadilishwa na hao wazee sijui nn kingeliwakuta. Mwinyi alivyo sema kama si katiba angelitamani Magufuri awe Rais wa milele ni kauli nzito sana ya kuwaponda Mkapa na JK japo wengi hawakuielewa wakaenda chaka. Alimaanisha hao wawili walikua wapigaji sana wa mali za wanyonge na wameipeleka nchi pabaya sana hivyo anatamani Ikulu pasiingie tena majizi. Huyo mzee alitumia fumbo kubwa sana sema wengi hatutafakari kwa kina kunakua na mihemuko ya siasa za maji taka. Kumbuka kwenye tawala za Ben na JK mzee Mwinyi hakuwahi kujitokeza kusema hayo?