Nimeshangazwa sana, Kabisa Kabisa, Na Kauli ya aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu Ndugu Mkapa. Nimesoma Katika Mtandao wa IPPmedia, Mkapa akiwa Muleba, Alitoa madai Kwamba, wapinzani wanahitaji uzoefu wa Miaka 50 ili waweze kuaminiwa Kuongoza Nchi. Kauli hii Kusemwa na Kiongozi ambaye ni Midomo yake bado haijaisha harufu mbaya ya Kuwaita Wanzania Wapumbavu, Inanifanya Niamini Kuwa Kweli, Kiongozi Huyu anaamini Kuwa Kweli Watanzania ni Wapumbavu na Anaweza Akadhaalilisha Akili zao atakavyo kwa Uwongo n Upotoshaji.
Mimi Nina Maswali Mengi Ningeweza Kukuuliza Mheshimiwa Rais, Lakini Nitakuuliza Kumi Ukinijibu Kweli Nitaamini Kuwa angalau mimi kama Mtanzania Ni Mpumbavu Ukishidwa Uwaombe Radhi Watanzani au Kama Kiburi chako Hakikuruhusu "Ukae Kimya" Nikwambie kwa lunga ya kukuheshimu.
1) Hivi, Baba wa Taifa Mwl JK Nyerere alipokabidhiwa Uhuru wa Tanganyika akiwa na Umri Wa Miaka 39, Alikuwa na Uzoefu wa miaka 50? Au niambie Kama Hakuwa Kiongozi Mzuri, Eh Tuambie Mh. Mkapa!
2) Hivi Jomo Kenyatta Alipotoka Jela na Miaka Michache baadaye akakabidhiwa Uhuru wa Kenya alikuwa na Uzoefu wa Miaka 50? Eh Tuambie Mh. Mkapa,
3) Hivi, Kenneth Kaunda wa Zambia Kiongozi aliyeheshimika alikuwa na Uzoefu wa Miaka? Eh Tuambie Mh. Mkapa.
4) Hivi Thomas Sankara Rais mtoto, aliyeionyesha Dunia, Mfano wa Taifa la Bukina Faso, Alikuwa na Uzoefu wa Miaka 50? Eh Tuambie Baba Mkapa.
5) Hivi Kiongozi Mashuhuri Kaabisa, Kipenzi cha Afrika Nelson Mandela alipotoka Jela na Miaka miwili Baadaye Akaongoza SA kwa amani na Akawa Rais wa Mfano alikuwa na Uzoefu wa Miaka 50? hata Jela hakukaa Miaka 50 (ni 27) Kama Utatudanganya Jela Ilimfundisha. Eh Nijibu Mh Mkapa!
6) Hivi Kipenzi Cha Africa, Samora Mashell Alipopigania, akapata Uhuru na Akawa Rai wa Mozambique alikiwa na Umri Mdogo sana? Alikuwa na Uzoefu wa Miaka 50?
7) Uganda imekuwa na Vita Tangu Uhuru, Akaja Kijana Yoweri Museven, Akatwaa Madaraka Akaongoza Uganda Vizuri Tangu 1986, Uganda imekwa ni Nchi ya Mfano Africa, Yoweri alikuwa na Uzoefu wa Miaka 50? Eh Tumabie Mh. Mkapa
8) Mhe Ketumile Masire Botswana, Paulo Kagame wa Rwanda etc. Wamekuwa Viongozi Mfano, walikuwa na Uzoefu wa Miaka 50?
9) Fidel Castro alipndua serikali ya Kibeberu ya Batista ya Cuba 1959 Na Cuba ndio nchi pekee ndogo sana Imeshidha Ukandamizaji wa Kutisha wa Vikwazo vya Uchumi, kwa zaidi ya miaka 50 na sana baada ya kugundua Mafuta Mengi sana Marekani Imeipigiaa Magoti. Je Fidel Castro ambaye Dunia yote Inamtambua na Kumheshimu Alikuwa na Uzoefu wa Miaka 50, Eh Niambie Baba
10) Mapinduzi ya China, yamefanywa 1949 mika michache sana Iliopita na Mao Zedong, Na sasa China iliokuwa na Unyonge limekuwa Taifa Lenye Nguvu, Kabisa la Pili Duniani, Kiuchumi, Kijeshi na Kiteknologia. Mao alikuwa na Uzoefu wa Miaka 50? Eh Tuambie Mh Mkapa.
11) Uhuru wa Marekani wa July 4 1776 Ulipatakana kwa Kuongozwa na Askari Mkulima George Washington, na Mpaka sasa Miaka 300 baadaye Marekani ni Taifa Kuu kuliko yote Ulimwenguni, Je Washington alikuwa na Uzoefu wa Miaka 50?
12) Abraham Lincoln baba wa demokrasia ya leo,ambaye ajifundisha kila kitu mwenyewe bila kusoma shule yoyote, Alianzisha Chama cha Upinzani cha Republican, Akashinda Uraisi na hatimaye akakomboa Watumwa kabisa. Alikuwa na Uzoefu wa Miaka 50?
Mh, Raisi Mkapa, Acha Kudhalilisha akili za Watanzani, Watanzani Ni Waelewa, waliobaki wapumbavu ni wale ambao wanafikiri Dunia ya Leo na Tanzania ya leo Ni Business as usual, (Biashara kama Kawaida)
Mh. Rais, Kama Uzoefu Unaozungumzia Ni wa akina Jean Bedel Bokassa wa Afrika ya Kati wa Kujifanya Kabisa wafalme kama Ujionavyo wewe Hatuutaki.
Mh. Rais Kama Uzoefu unaouzungumzia wa Miaka 50 Ni kama wa Akina Daniel Arap Moi, Aliyetawala Kenya kama Shamba lake la mifugo Hatuutaki.
Mh. Rais Kama Uzoefu Unaozungumzia Ni kama wa Akina Suharto Ambaye Nusu aliangamize Taifa la Indonesia, Hatuutaki. Asante Mungu sasa kwa wale ambao Ungewaita Novice, sasa Indonesia ni Nchi ya Mfano.
Mh. Rais Kama Uzoefu ambao Unausema wa mika 50 Ni Kama wa Robert Mugabe, ambaye wakati alipoanza, japo kwa kiwango cha Uwongo wako Ungesema alikiwa hana Uzoefu, lakini alifanya Vizuri sana. Lakini kama Uzoefu Unaotaka ni huu wake wa sasa hatuutaki.
Mh. Rais Kama Uzoefu Unaouzungumzia ni wa Watu kama, Agusto Pinochet wa Chile, au Blaise Compeore wa Bukina Faso au Idd Mubarak wa Misri, au Nicolae Ceausescu wa Romania au Mobutu Kuku Nbendu Seseseko wa Zabanga wa iliyokuwa Raire, Hatuutaki. Eh Mheshima Rais. Tuheshimu angalau Kidogo.
Na Mwisho Kama Uzoefu unaosema Ni Uzoefu wa CCM wa Kusema Mtachoma Kunguni Vitandani (Mafisadi) tena Mkizungumzia Kunguni Vitanda vya Wengine, Huku Kunguni wa Uhakika, Wa hatari, waliothibitika kuwa Kunguni, Mkiwabeba sio Vitandani bali Nguoni mwenu, Kama Vile Kunguni wa Escrow, Andrew Chenge (anagombea Ubunge) Ngeleja, Anna Tibaijuka (Mnamnadi Ubunge, sio?) Pr. Sospeter Muhongo (Mnamnadi Ubunge sio? Na hata Zile za Viroba na Sandarusi Kuna Madai hata wewe Ulipata Rumbesa hilo siju, na Pia Makongoro Nyerere na Porojo zake naye alichukua sandarusi na Viroba vya Escrow. Kama Uzoefu Ni Huo kaeni nao na Kwa lugha ya heshima, Nendeni Mkahifadhi uzoefu huo kule" sehemu sehemu" Unakostahili.