Elections 2010 Mzee makamba huenda akaamua kujitosa mwenyewe bumbuli...

MtazamoWangu

JF-Expert Member
Apr 25, 2009
313
7
baada ya malalamiko mengi dhidi ya mwanae Januari na kutokubalika katika jimbo la bumbuli, Mzee Makamba amedokeza huenda akaamua kuingia mwenyewe kwenye ulingo...mzee Makamba alinukuliwa akiyasema hayo pale alipoulizwa na wazee wenzake kijijini kwake..
Kumekwa na malalamiko mengi dhidi ya Januari Makamba kutoka kwa Mh Shelukindo na baadhi ya viongozi wa chama na wananchi jimbo la bumbuli.

Mzee Makamba ambaye alishawahi pia kugombea ubunge kwenye jimbo hilo mara 2 na kukosa, ameshindwa kumsaidia mwanae kukubalika ndani ya jimbo, Mzee Makamba analalamikiwa kwa kuwadharau,kuwatukana wananchi wa jimboni mwake na kuendekeza ubinafsi, baahi ya watu waliokaribu na familia yake wamesema ni bora wasipige kura kuliko kumchagua Januari Makamba.

Hata hivyo kampeni za Januari Makamba bado zinaendelea na badhi ya viongoi wamekuwa wanaendelea kumpigia kampeni na sasa mama yake mzazi january ameamua naye kujitosa kfanya hivyo kwa kwenda kijijini kwa mzee makamba na kuonana na akina mama na kuwapa zawadi ikiwa ni pesa na khanga, mama huyu ameamua kufanya hivyo baada ya wanajimbo kusema hawamjui Januari wala mama yake, ikumbukwe mama yake Januari ni mzawa wa Kagera na hajaahi kuishi bumbuli...

bado pia Mh. Shelukindo hajaamua rasmi kama atagombea tena au la...
 
Mimi nasubiri nije nione uamuzi wa makamba juu ya Januari kuanza kampeni kabla ya muda!
 
Makamba hawezi kupata ,mwaka 1995 alijaribu akashindwa, na alichoharibu ni kuja na hoja ya udini kuwa tangu tupate uhuru jimbo hili halijawahi kupata mbunge mwislamu, hivyo yeye alitaka achaguliwe kwa vile tu ni mwislamu ndiyo maana akapigwa chini kwenye kura za maoni kwa kigezo kuwa angezigawa kura kwa misingi ya ukristo na uislamu. Makamba ni yule yule kwani dini ni jambo la rohoni,hivyo hajabadilika. Pia Makamba hakubaliki hata kijijini kwao Mahezangulu.Hata hivyo amechoka sera anayoijua sasa ni kutukana wapinzani nakumsifia JK.
 
viongozii aina ya makamba huwa wanakuwa na nguvu kwenye mfumo kama wa CCM tuu..
 
Makamba hawezi kupata ,mwaka 1995 alijaribu akashindwa, na alichoharibu ni kuja na hoja ya udini kuwa tangu tupate uhuru jimbo hili halijawahi kupata mbunge mwislamu, hivyo yeye alitaka achaguliwe kwa vile tu ni mwislamu ndiyo maana akapigwa chini kwenye kura za maoni kwa kigezo kuwa angezigawa kura kwa misingi ya ukristo na uislamu. Makamba ni yule yule kwani dini ni jambo la rohoni,hivyo hajabadilika. Pia Makamba hakubaliki hata kijijini kwao Mahezangulu.Hata hivyo amechoka sera anayoijua sasa ni kutukana wapinzani nakumsifia JK.

Wengi hawakubaliki vijijini mwao na bado wanapeta. For makamba, ni bora akapumzika ktk active politics na akaendelea kumsifu JK anapoalikwa? au anaogopa kusahauliwa kama mtangulizi wake?
 
Wananchi wa BUMBULI wana akili.......

I will prove this during CCM primaries and finally during the general election. Kama kweli wana akili, watachagua Mbunge mzuri vinginevyo ni maumivu.
 
Back
Top Bottom