Mzee Majuto akanusha kustaafu kuigiza

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,495
Mzee-Majuto-akifurahia-ushindi.jpg.pagespeed.ce.3PmMLx9yd9.jpg


Msanii wa filamu za kuchekesha, King Majuto amekanusha taarifa ambazo zilizagaa katika mitandao ya kijamii kwamba amestaafu kuigiza.

Akiongea katika kipindi cha Clouds E cha Clouds TV Jumatano hii, Mzee Majuto amedai sio kweli kwamba amestaafu kuigiza ila kuna baadhi ya filamu ambazo hatafanya tena.

“Watu wameniwekea maneno mdomoni, sijasema nimeacha kuigiza,” alisema Majuto.“Wakati nipo Hija mwaka jana nilikuwa nafikiria niache kabisa kuigiza, lakini baada ya kurudi nikaona nalazimika kuendelea kuigiza ili nipate pesa za kuendesha maisha yangu, kwa sababu bila filamu nitakufa njaa,”

Pia muigizaji huyo amesema hafanyi tena stand up comedy kwa kuwa wakati anafanya kuna matukio ambayo yatakuwa yanaendelea katika ukumbi ambayo dini yake hayaruhusiwi.

Pia Majuto amewataka mashabiki wa filamu zake kuendelea kusubiria kazi zake ambazo atakuwa anaandaa mwenyewe.
 
mmh tumeshawazoea leo mnasema hiv kesho mnabadilika sasa sijui mnamtishaga nan
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom