Mzee karume mpima ardhi bora wa kuiga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzee karume mpima ardhi bora wa kuiga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kingadvisor, Dec 24, 2011.

 1. kingadvisor

  kingadvisor Senior Member

  #1
  Dec 24, 2011
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kila nikiuliza kwa nini Dar es salaam na miji mingine watu wanaishi viwanja visivyopimwa naambiwa gharama za upimaji wa ardhi kubwa bajeti haipo.Nilikwenda Zanzibar nikauliza ni mpima ardhi gani alipima yale maghorofa ya michezani nikaambiwa ni mzee Karume.Aliamua kupima kwa hatua za miguu na kamba baada ya kuona maafisa wa ardhi wanaleta longolongo zisizozalisha viwanja vya kupima.Akasema shika kamba nyoosha hesabu hatua kadhaa toka hapa upana na urefu kiwanja cha ghorofa moja hicho tayari ,twende kwingine.Leo hii maghorofa yale pale.

  Nimechoka uongo wa kisomi wa maafisa ardhi mara utakuta migogoro ya viwanja wanasema kuna mgongano kati ya ramani ya ardhi iliyopigwa na ndege za ramani za angani na mpimaji yule wa ardhini mara oh bajeti haitoshi ili mradi tu miaka mingi ipite viwanja havipimwi.

  Nadhani ni wakati muafaka wa kutupa majalani vyombo vyote vya kisasa vya kupima ardhi na kuammuru maafisa wote wa ardhi wapewe kamba za katani na waambiwa kila kiwanja kinabidi kiwe hatua ngapi urefu na upana wa hatua ngapi za miguu wapelekwe maporini wapime viwanja Kila siku kwa miguu na kamba kwa kuwalipa mishahara yao tu.Kwani kila siku wanafanya nini ofisini? kamba za kuanzia kupimia kama serikali haina waombwe wananchi wenyewe watanunua.Utaalamu huo mwingine na porojo zake zifuate baadaye.Kama hawataki kazi hizo za kupima viwanja zipewe serikali za mitaa na vijiji kama kuna eneo liko wazi waaambiwa kila kiwanja ni hatua ngapi upana na urefu wapewe kamba waanze upimaji wa hatua badala ya kushinda majiji na miji inakua kwa kasi ya ajabu maafisa ardhi wamekaa maofisini wanapiga porojo za bajeti haitoshi na kushinda wanajifanya wanasolve migogoro ya viwanja ambayo huwa wameitengeneza wenyewe.

  Kama kuna technolojia ya kisasa ya upimaji laklni haitusaidii kwenda kasi kimaendeleo ya upimaji wa ardhi tunaing`ang`ania ya nini.

  Mkoa wa pwani wameamua kujipimia mashamba mengi kienyeji na kuweka mipaka na barabara wanaita mikuza kila baada ya eka moja na sehemu nyingi zenye hiyo mikuza zinaingilika kwa gari kila upande bila wasiwasi hata viwanja inawezekana.Si kila cha mzungu ni superior tusiidharau miguu yetu yaweza kutusaidia kutumika kupima ardhi kwa kutumia hatua zetu.Na tusiudharau mkonge wetu waweza tupa kamba za kunyooshea size za viwanja vyetu.

  Ikiwezekana serikali impe nishani ya juu ya upimaji wa ardhi bora wa kitanzania Sheikh Abeid Amani Karume.Nawasilisha.

  kingadvisor@yahoo.com
   
Loading...