Muigai Jr
JF-Expert Member
- Jun 3, 2020
- 1,529
- 2,969
Ukweli mtupuNi vipaumbele tu, JPM aliwekeza kwenye miradi mikubwa mfano Stiglers na SGR, JK ndio akawekeza kwenye elimu nakumbuka kuna wakati ikasemekana hata lile wazo la shule za kata aliyelileta alikuwa Lowassa akiwa PM.
Samia licha ya kuwepo madarakani kwa muda mfupi bado haeleweki mipango yake, ila hali ya mambo inavyoonesha, naona wameshaanza kula kwa urefu wa kamba zao.
- Bwawa la Nyerere ni kama limeshawashinda, sioni cha maana wanachofanya zaidi ya kufanya ziara kuangalia maendeleo ya ujenzi wake watuzubaishe lakini baada ya hapo ni kimya. Ile habari ya winchi ya tani 24 iliyoagizwa nayo sijui iliishia wapi.
- Umeme kukatika hovyo bila sababu za msingi, mwanzo walisema chanzo kilikuwa ukame, lakini hata baada ya mvua kuanza kunyesha bado umeme unasumbua, tatizo ni nini? kama ni maintanance kwa nini tatizo bado liwe endelevu? hapa ndipo JPM anapokumbukwa.
- Tozo; walisema zitaenda kujenga madarasa na vituo vya afya matokeo yake wakatumia pesa za Covid kwa ajili ya kazi hiyo, sasa sijui hizi tozo wanazotoza mpaka leo zinatumika kwa kazi gani wala hatuambiwi tena kwa mwezi wamekusanya ngapi na zinaelekezwa wapi? mambo yanajiendea tu.
- Mfumuko wa bei, bidhaa kupanda bei kila siku wakiulizwa wanasema tatizo ni soko la dunia, nashangaa hata nyama ya n'gombe nayo kupanda imesababishwa vipi na soko la dunia wakati Tz tuna n'gombe wengi tu?.
Wengine wanasema "soko huria" kwa hiyo hili soko ndio limeachwa limuumize mlaji kama vile hakuna serikali ya kusimamia mambo? kumbe sasa Tanzania wafanyabiashara wako juu ya serikali.
Hapa tatizo ni usimamizi na ufuatiliaji, kuna uzembe umerudi serikalini.