Mzee Benjamin William Mkapa ulikosea wapi?

Karikari

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2013
Posts
250
Reaction score
41
Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mh.Mkapa uliipokea nchi 1995 ikiwa na mzigo wa madeni Hazina ya Taifa ikiwa haina kitu.


Ulitushauri tufunge mkanda lkn ukasahau kutuambia kuifungua au hata kuilegeza.Ukakusanya kodi,ukalipa madeni ya ndani na nje ukairudishia nchi yetu Heshima ya kukopesheka na pia heshima ya mfanyakazi aliyekuwa amenyang'anywa heshima hiyo na mfanyabiashara.

Pia ulidhibiti mfumuko wa bei kwa kipindi chote cha miaka kumi.Wafanyakazi wakawa wanalipwa mishahara kwa wakati.

Ulilinda heshima ya chama chako kama mwenyekiti mwenye kauli yenye kuheshimika.Hukuwa unachekacheka na wachafuzi wa hali ya hewa.

Ulijenga barabara zinazoonekana kwa macho sio zakutangaziwa kwenye vyombo vya habari kwa gharama kubwa wakati wanafunzi wanakaa chini.

Ulijenga Bunge la kisasa ambalo Wasira na Komba wanachapa usingizi huku wengine wakiimba kawimbo ka Ndiooooooooo!!!

Ulinunua Rada na Ndege ya Rais ambayo hukuitumia japo Chenge na Mramba walikuzunguka

ulijenga majengo pacha ya kutega uchumi japo kaganji kalikuwepo kiana.

Hayo yote na mambo mengine uliyoyafanya yalikufanya uzunguke nchi nzima kuwaaga watanzania ukiwa kifua mbele ukiwaaminisha unakwenda kulima ukapewa zawadi mbalimbali kitu ambacho MRITHI wako hatathubutu kabisa maana hakuna mwenye shida nae kwani hana lakuwaambia watz.


Sasa Baba Mkapa ulikosea wapi kinachokusababisha ukose heshima ya kuingilia kati matatizo yanayolikumba Taifa letu walau kumshauri Jk au vyombo vya dola na msajili wa vyama vya siasa pamoja na viongozi wa vyama vyetu vya siasa au hata Bunge letu na matamko tata ya mawaziri wetu chini ya Pinda? Au na wewe unakubaliana na kauli ya Pinda kuwa Wananchi wapiga kura WAPIGWE TU KWAKUWA CCM IMECHOKA KUONGOZA?
 
Alikosea kugawa nyumba za Serikali na kugawa mali za umma (madini, benki). Jana balozi Majaar kasema tusifanye makosa kwenye gesi kama tulivyofanya kwenye madini!
 
Pemba brothers were murdered in coldblood hapo ndipo alipokosea.
 
EPA na kumsadia kikwete kuingia ikulu kwa kutumia fedha chafu za epa. hilo ndio kosa lake na mengine anaonewa tu.
 
Mkapa sio msafi manvyoongea, kikwete amejenga barabara kuliko RAIS yeyote aliyekuwa nchini, nenda kigoma, rukwa bukoba mtwara na Tabora

Kikwete amejenga chuo kikuyu cha Dodoma

Kikwete amejenga daraja la malagarasi na sasa anajenga la kigamboni

Kikwete anajenga viwanja vya ndege vikubwa mbaya, kigoma na upanuzi wa JNIA

Kwa gharama za miradi kikwete yupo mbali. Ila kwa uchumi mkapa alikuwa nafuu. Tuwe wa kweli
 
Ingawa Sipendi hiki chama lakini Namkubali mkapa kwa baadhi ya mambo.Mkuu umesahau Daraja na Uwanja wa mpira..aliye mpokea hajafanya kitu ndio maana anatumia nafasi kumchafua zaidi ya..
 
Ingawa Sipendi hiki chama lakini Namkubali mkapa kwa baadhi ya mambo.Mkuu umesahau Daraja na Uwanja wa mpira..aliye mpokea hajafanya kitu ndio maana anatumia nafasi kumchafua zaidi ya..


To is the worst of all,kwa ajili ya kujipretend.By the way alikopa mil 500 from NBC na kufungua a/c benk ,na kusajili ANBEN akiwa rais wa JMT.

Nyerere is crying on his grave.God bless him
 
Manyerere Jackton

Kuhusu suala la gesi na mafuta, tayari makosa yamefanyika. Ingia kwenye wavuti ya Wizara ya Nishati na Madini utakuta Rasimu ya Kwanza ya Sera ya Gesi. Idownload kisha uisome vizuri.

Kwa mujibu wa "mpuliza filimbi" niliyekutana naye, kilichofanyika ni kwamba tumeingizwa mjini kwa kuingia kwenye mikataba ya kipumbavu kabisa na hawa wanaojiita wawekezaji. Hali halisi ni kwamba SISI tungeweza kabisa kukopa Dola za Kimarekani TRILIONI SITA ambazo zingetufanya SISI kuwa wawekezaji, hivyo tungewaambia hawa wenye teknolojia waje kutafuta gesi na mafuta, sisi tuwalipe kwa kazi yao. Kisha waje wengine kuzalisha, walipwe kwa kazi hiyo, teknolojia inabaki kwetu. Tunaimiliki sisi. Kisha waje watu wa kusambaza gesi na mafuta. Mabomba yetu. Waje wa kuzalisha umeme. Vinu ni vyetu. Kazi kwisha.

Kinachoendelea sasa ni USANII TENA USANII WA HALI YA JUU kwani tumeingizwa kwenye mikataba ya kifisadi kabisa.

Hivi utakubalije mtu akaja kwako, akakuambia kwamba tutachimba gesi na mafuta lakini wewe huna ruhusa ya kumiliki mitambo wala teknolojia, unabaki unakenua meno na kusema "Yes Massah!" Tutaendelea kuwa wanyonge mbele ya WAWEKEZAJI UCHWARA hawa mpaka lini?

Eti tunachoruhusiwa ni kuingia Mikataba ya Mgawanyo wa Faida (Profit Sharing Agreements - PSAs) ambayo ilikoma kutumiwa duniani kote miaka 20 iliyopita.

Kampuni kama ExxonMobil ya Marekani na StatOil ya Norway yanasifika kwa utendaji wake wa kilaghai, rushwa na mikataba ya kifisadi. Hawa wamekuja kuvuna na hawana nia njema wala maslahi na sisi.

Nawashangaa sana viongozi wabovu kama Waziri Sospeter Muhongo anayetumbua pesa za walipakodi kuwadanganya watu kupitia kipindi cha "Baragumu la Msimbati" ambacho amekuwa akikitumia kueneza uongo kwamba Tanzania haina uwezo wa kuchimba visima hivyo vya gesi na mafuta kwa kuwa ni gharama kubwa. UONGO MKUBWA TENA WA KIZANDIKI. Ninamtaka athibitishe kama sisi hatuwezi kukopa na kuimiliki teknolojia hiyo!

Watanzania wanadanganywa kwamba watu wamefaidika na mradi wa bomba la Songo Songo huku mpaka leo kuna watu bado hawalipwa fidia kutokana na ardhi yao kuchukuliwa kwenye eneo ambapo bomba hilo limepita. Ole wenu na uongo wenu. Isifike siku ambapo watu hao watachoka na kusema liwalo na liwe, kwani wataona hawana tena cha kupoteza!!!

Balozi Maajar, umechelewa sana kuwaamsha Wadanganyika wako.

Wachumi wetu, ambao waliishauri serikali miaka kadhaa nini tufanye na nini tukatae, serikali ikakataa kumiliki teknolojia huku Benki ya Dunia ikisikitika kwa nini tulikataa mkopo huo, tena ulioandaliwa kwa masharti nafuu mno, tukakubali masharti ya kifisadi ya kampuni hizi zinazojiita wawekezaji rafiki kwetu!!!

Ama kweli wajinga ndio waliwao!

Lakini iko siku ujinga wetu utabadilika na kuwa werevu. Hapo ndipo kibao kitakapogeuka. Pale dukani, badala ya kusomeka "Tumefungua" kitasomeka "Tumefunga".

Siku hiyo ipo njiani. Wala si muda mrefu itafika!
 
Last edited by a moderator:

Mzee huyu alifanya mazuri mengi kuliko mabaya! Nitamkumbuka kama Kiongozi shupavu. Mabaya yoote yanayosemwa yalifanyika ndani ya miaka 2 ya mwisho, kitu kinachonishawishi kwamba hakudhamiria bali alizungukwa na 'makanjanja' wa chama kwa 'gia' ya kuandaa fedha za uchaguzi (ni desturi ya chama chenu)!

Ni Jembe, ndio amefanikisha uhuru wa Sudani kusini.
 

Duh kunawatu mnamapointi. Ila kumbuka miaka ya mwanzo ya utawala wa jk hakuna aliyedhani jamaa anamuelekeo. Ila miaka ile ya mwisho miwili na alivyofanikiwa kumzima mrema kwa kuwaua wale waliokuwa source of info, na kutumia mamluki kuiua nccr na kumpandikiza kibaraka mbatia, pia aliwatumia wazee wenye uzoefu hakuwa na vijana walopokaji kama nape na mwigulu, hakuwa na wazee wazee waliokata tamaa kama wasira, na yeye ndiye alikuwa mtoa kauli wa mwisho, si kama jk ambapo unakuta nape analopoka hivi juu ya chama mara mwigulu anaunda kesi na kuropoka. Kwa ujumla siasa za kuangamiza upinzani zilishafika ukomo, wanatakiwa ccm wajipange waone sasa wananchi wanahitaji kusikia nini? Kwa hari ilivyo sasa kila mtu anajua ccm ni chama cha wauaji na anayeratibu ni mwigulu, je watakinasuaje?? Waliwanunua mwapamba na juliana ila wamegonga mwamba, sasa wanadamu za kunguni. Kwa ujumla ccm inahitaji mtu mwenye weledi wa kuelewa mazingira ya sasa, na si kama nape na mwigulu, ni vijana ila they are outdated!!!
 
Hakuna Rais mbovu anaetugharimu watanzania kama Benjamin William Mkapa kwa sababu zifuatazo:-
1. Alitumiwa na mataifa ya magharibi kutekeleza sera mbovu za ubinafsishaji zilizoratibiwa na WB na IMF kupitia kwa Ballali rejea JKN alivyomfokea kuhusu NBC saga na hatimae wakamuua baba wa Taifa.
2. Aliiondolea TISS meno na kuibakishia kazi ya kushauri na umbeya! Baada ya hapo ni historia maana nyara za Taifa zinatoroshwa mwendo mdundo
3. Alifanya mauaji ya kutisha Pemba
4. Alikubali sera ya madini ambayo sisi wenye mali tulikuwa tunaambulia 1% wakati 2% walikuwa wanagawana na Mramba kupitia uwakala!
5. Alifanya biashara Ikulu
6. Alituletea Netgroup solution kwa ajili ya kuidhoofisha TANESO na hatimae deals za majenerata zinatugharimu walalahoi
7.Wizi wa EPA
8. Wizi wa Meremeta
9. wizi wa kijani kilichokomaa aka deepgreen
10. wizi wa vitalu vya uwindaji
11. kugawa nyumba za serikali
12. kuwa na hisa Geita Gold Mine wakati akiwa Rais
13. Kujigawia block za gesi mtwara yeye yona na mramba
14. Kujichukulia kiwira
15. Kukubaliana na masharti ya HIPIC yenye kuigharimu nchi hususan misamaha ya kodi kwa wawekezaji wenye kutorosha rasilimali zetu
16. kuwa na kiasi kikubwa cha fedha Uswis
17. kuwaibia watanzania thru rader yeye na chenge
18. kuwaibia watanzania thru ununuzi wa jengo la ubalozi Italy akishirikiana na prof...
19.kumua baba wa taifa
20. kukandamiza demokrasia nchini
 
[h=1]Zitto: wabunge wa Tabora wameshindwa kuwaletea barabara[/h]
 
Last edited by a moderator:

Mkuu hapo kwenye 19 kuna ukweli wowote au ni maneno ya kwenye vijiwe vya gahawa?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…