Mzee Benjamin Mkapa avichana Vyombo vya Habari Afrika

igp

JF-Expert Member
Feb 16, 2015
839
543
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mzee Benjamin Mkapa amevikosoa vyombo vya habari barani Afrika na haswa kusini mwa Jangwa la Sahari kwa kile alichosema vingi vimejikita katika kuripoti habari za kisiasa na matukio ya nani kafanya nini au kawa nani, badala ya kuripoti habari za uchumi za kuwasaidia wananchi.

Mzee Mkapa aliyasema hayo alipokuwa akifanya mahijiano na na Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle (DW) ya nchini Ujerumani ambapo alisema kwenye vyombo vya habari vya Afrika kuna upungufu mkubwa wa wa habari za uchumi na maendeleo zilizofanyiwa utafiti wa kina.

“Tatizo moja kubwa la vyombo vya habari vya nchi za Afrika hasa hasa Kusini mwa Jangwa la Sahara ni kwamba habari nyingi zinazopewa kipaumbele ni zile za kisiasa na zinazohusu nani ni nani na kafanya nini.”

“Kuna upungufu mkubwa wa habari za kiuchumi na maendeleo zilizofanyiwa utafiti wa kina na zinazochochea maendeleo. Kuna habari kidogo sana za utetezi wa kimaendeleo na kujipanga ili tupige hatua.”

Kufuatia hali hiyo, Mzee Mkapa alisema kuwa uhuru wa vyombo vya habari unaodaiwa kuwa umebanwa, unahusu vyombo vya habari ambavyo havina mchango kwenye maendeleo ya uchumi wetu zaidi ya kuzungumzia matokeo badala ya uchambuzi.

“Kwa hiyo, huo uhuru wa vyombo vya habari unaosema unabanwa unahusu kundi la vyombo vya habari ambavyo havina mchango wowote katika uchambuzi wa masuala ya uchumi utetezi wa maendeleo wala kwenye kujipanga kujitafutia maendeleo. Nasi ni taifa masikini linalohitaji kuendelea. Nadhani ni uamuzi sahihi.” alisema Mzee Mkapa.

Kauli hii ya Mzee Mkapa ilikuja baada ya kuulizwa kuhusu madai ya kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli inabana uhuru wa vyombo vya habari hali ambayo haikuwapo miaka ya nyuma.
 
Mkapa anasahau kwamba vyombo vya habari vinaangalia habari gani inauza, afrika tutafika huko anapotaka baada ya muda kwa sasa tunaendelea vyema siasa 59% uchumi 11% udaku 30%

Tutafika tuu, kwanza hatuitaji kufiria kibepari kama yeye, hatujawahi kuwa katika sehemu yake kwa tz ni watu 5 tuu wamefika hapo, amwambie swaiba wake achange vitu tukae sawa
 
hahaha
angeona huko USA kina CNN wanavo ripot siasa asinge ongea, siasa ni maisha, USA uchumi wao unakua, ila wala siyo habari ya kipaumbele wanajitangazia Trump ka tweet nini, ki ujumla huwez vipangia vyombo vya habari vitangaze kitu, uchumi ukiwa mzuri si mpaka tutangaziwe tutajua tu wenyewe, sijaona kama point yake ina maana sana
 
Mkapa ametuingiza mikataba inayoitesa nchi wa mrahaba 3% na hizi habari watawala hawazipendi.

Mkapa anazungumzia habari za kiuchumi je uelewa wa wananchi ktk hili ukoje?! Si kwamba wao watawala wamehakikisha wananchi wanakuwa mbumbumbu kama alivyosema yeye na hivyo kubaki kushabikia wanasiasa na matukio?! Hali hii wameiandaa na kuijenga wao ni faida kwao watawala.
 
Kama kutangaza kumsusia Makonda,sijawahi ona uamuzi wa kupumbavu kama huo
Halafu wanalilia uhuru wa habari,wanataka uhuru wakati wao wanawaminyia habari wananchi,kisa wamegombana na mtu mmoja tu.Mwanasiasa haanguki kwa kususwa na vyombo vya habari
Unataka wamwandike jambazi bashite kwa faida gani? Ajiandike mwenyewe si alijiona mjanja kuvamia clouds TV. Ng'ombe nyie
 
Kama kutangaza kumsusia Makonda,sijawahi ona uamuzi wa kipumbavu kama huo
Halafu wanalilia uhuru wa habari,wanataka uhuru wakati wao wanawaminyia habari wananchi,kisa wamegombana na mtu mmoja tu.Mwanasiasa haanguki kwa kususwa na vyombo vya habari
Bashite mnamuhusudu kama Mungu wenu huko CCM.

Amefanya kosa aombee msamaha acheni mahaba yaliyopitiliza na ya kutilia shaka kijinsia.
ndafu inatetea matendo ya mteule wake, anataka waandishi wa habari kwenye vichwa vya habari waandike mapambio ya Tanzania ya Uchumi wa Viwanda ambavyo havipo
 
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mzee Benjamin Mkapa amevikosoa vyombo vya habari barani Afrika na haswa kusini mwa Jangwa la Sahari kwa kile alichosema vingi vimejikita katika kuripoti habari za kisiasa na matukio ya nani kafanya nini au kawa nani, badala ya kuripoti habari za uchumi za kuwasaidia wananchi.

Mzee Mkapa aliyasema hayo alipokuwa akifanya mahijiano na na Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle (DW) ya nchini Ujerumani ambapo alisema kwenye vyombo vya habari vya Afrika kuna upungufu mkubwa wa wa habari za uchumi na maendeleo zilizofanyiwa utafiti wa kina.

“Tatizo moja kubwa la vyombo vya habari vya nchi za Afrika hasa hasa Kusini mwa Jangwa la Sahara ni kwamba habari nyingi zinazopewa kipaumbele ni zile za kisiasa na zinazohusu nani ni nani na kafanya nini.”

“Kuna upungufu mkubwa wa habari za kiuchumi na maendeleo zilizofanyiwa utafiti wa kina na zinazochochea maendeleo. Kuna habari kidogo sana za utetezi wa kimaendeleo na kujipanga ili tupige hatua.”

Kufuatia hali hiyo, Mzee Mkapa alisema kuwa uhuru wa vyombo vya habari unaodaiwa kuwa umebanwa, unahusu vyombo vya habari ambavyo havina mchango kwenye maendeleo ya uchumi wetu zaidi ya kuzungumzia matokeo badala ya uchambuzi.

“Kwa hiyo, huo uhuru wa vyombo vya habari unaosema unabanwa unahusu kundi la vyombo vya habari ambavyo havina mchango wowote katika uchambuzi wa masuala ya uchumi utetezi wa maendeleo wala kwenye kujipanga kujitafutia maendeleo. Nasi ni taifa masikini linalohitaji kuendelea. Nadhani ni uamuzi sahihi.” alisema Mzee Mkapa.

Kauli hii ya Mzee Mkapa ilikuja baada ya kuulizwa kuhusu madai ya kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli inabana uhuru wa vyombo vya habari hali ambayo haikuwapo miaka ya nyuma.
Hivi Dw walitegemea Mzee Mkapa akosoe maamuzi ya JPM ????!!!!!

Kwa hakika ningemshangaa kama angefanya hivyo, zaidi ya ambavyo sikubaliani na majibu yake..
 
Huyu mzee mstaafu bichwa kubwa akili kijiko.siasa ndio kila kitu huwezi kuongelea uchumi bila kuhusisha siasa kwa sababu siasa ina impact kwenye uchumi, jamii,kila kitu ni siasa.
 
Back
Top Bottom