Mzee Benjamin Mkapa avichana Vyombo vya Habari Afrika

Mzee Benjamin Mkapa avichana Vyombo vya Habari Afrika

Utapeli na Wizi sio dalili ya ukosefu wa akili na Kama unadhani hivyo umepotoka

Kwa hiyo kuuza viwanda vya nchi yako kwa bei ya kutupa huku ukitengeneza unemployment rate kubwa kwako ndio akili? Huyo anavichukia vyombo vya habari kama huyu aliyepo kwani wote wana udhaifu wa kutokupenda kukosolewa bali kusujudiwa. Kwa taarifa yako kama ni udhaifu viongozi wa kiafrika akiwepo Mkapa ndio wadhaifu kuliko udgaifu wa vyombo vya habari. Tena wala asiongee bali atuonyeshe mafanikio tuliyotapata kama nchi kwa yeye kuuza viwanda.
 
Huyu mzee mstaafu bichwa kubwa akili kijiko.siasa ndio kila kitu huwezi kuongelea uchumi bila kuhusisha siasa kwa sababu siasa ina impact kwenye uchumi, jamii,kila kitu ni siasa.

We ndo pumbavu. Elewa mada. Pima. Tumia akili yako sio matako
 
Mzee mkaa hapa anavichukia vyombo vya habari kwa sababu anaelewa nguvu iliopo ktk hivyo vyombo kurekebisha tabia ya viongozi wenye tabia chafu kama kujilimbikizia Mali. Na yeye ni mmojawapo. Habari kama za escrow na Richmond dowans na meremeta zimekaa kisiasa lakini zinagusa uchumi kwa kiasi kikubwa. Mwanafalsafa mmoja aliwahi kusema kuwa " Man is a political animal" na hivyo huwezi kutenganisha siasa na maisha ya kila siku ya mwanadamu.
 
Fungia makanjanja wote...na sasa hivi wafungiwe waandishi husika
 
mkapa huyu mwizi wa almasi na dhahabu au mkapa aliyekuwa mchezaji wa Klabu ya Yanga?
 
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mzee Benjamin Mkapa amevikosoa vyombo vya habari barani Afrika na haswa kusini mwa Jangwa la Sahari kwa kile alichosema vingi vimejikita katika kuripoti habari za kisiasa na matukio ya nani kafanya nini au kawa nani, badala ya kuripoti habari za uchumi za kuwasaidia wananchi.

Mzee Mkapa aliyasema hayo alipokuwa akifanya mahijiano na na Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle (DW) ya nchini Ujerumani ambapo alisema kwenye vyombo vya habari vya Afrika kuna upungufu mkubwa wa wa habari za uchumi na maendeleo zilizofanyiwa utafiti wa kina.

“Tatizo moja kubwa la vyombo vya habari vya nchi za Afrika hasa hasa Kusini mwa Jangwa la Sahara ni kwamba habari nyingi zinazopewa kipaumbele ni zile za kisiasa na zinazohusu nani ni nani na kafanya nini.”

“Kuna upungufu mkubwa wa habari za kiuchumi na maendeleo zilizofanyiwa utafiti wa kina na zinazochochea maendeleo. Kuna habari kidogo sana za utetezi wa kimaendeleo na kujipanga ili tupige hatua.”

Kufuatia hali hiyo, Mzee Mkapa alisema kuwa uhuru wa vyombo vya habari unaodaiwa kuwa umebanwa, unahusu vyombo vya habari ambavyo havina mchango kwenye maendeleo ya uchumi wetu zaidi ya kuzungumzia matokeo badala ya uchambuzi.

“Kwa hiyo, huo uhuru wa vyombo vya habari unaosema unabanwa unahusu kundi la vyombo vya habari ambavyo havina mchango wowote katika uchambuzi wa masuala ya uchumi utetezi wa maendeleo wala kwenye kujipanga kujitafutia maendeleo. Nasi ni taifa masikini linalohitaji kuendelea. Nadhani ni uamuzi sahihi.” alisema Mzee Mkapa.

Kauli hii ya Mzee Mkapa ilikuja baada ya kuulizwa kuhusu madai ya kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli inabana uhuru wa vyombo vya habari hali ambayo haikuwapo miaka ya nyuma.
hataki kuambiwa yeye. mwizi. maendeleo yatakuja vipi kama wezi kama yeye wamesaini .mikataba ya kinyonyani
 
Mzee mkaa hapa anavichukia vyombo vya habari kwa sababu anaelewa nguvu iliopo ktk hivyo vyombo kurekebisha tabia ya viongozi wenye tabia chafu kama kujilimbikizia Mali. Na yeye ni mmojawapo. Habari kama za escrow na Richmond dowans na meremeta zimekaa kisiasa lakini zinagusa uchumi kwa kiasi kikubwa. Mwanafalsafa mmoja aliwahi kusema kuwa " Man is a political animal" na hivyo huwezi kutenganisha siasa na maisha ya kila siku ya mwanadamu.
Huyu ni mshenzi, hata kwao Lupaso hakubakiki.
 
Back
Top Bottom